Coronavirus: Aliyekuwa rais wa Liberia akiri kufanya makosa kama ya China

Chanzo cha picha, Getty Images
Ellen Johnson Sirleaf aliingia katika historia kama mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kuwa rais barani Afrika.
Ellen aliiongoza Liberia kwa miaka 12 ikiwemo miaka ambayo mlipuko wa Ebola uliibuka mwaka 2014 mpaka 2016 na kuua watu takribani 5000 nchini mwake.
Shirika la BBC lilimuliza mshindi huyo wa tuzo ya Nobel mawazo yake kuhusu janga hili la virusi vya corona.

Ndugu wananchi wenzangu wa dunia,
Mnamo tarehe 19 oktoba 2014 kwenye kilele cha mlipuko wa ebola Afrika Magharibi, ambapo wananchi wangu 2000 walifariki na maambukizi yalikua maradufu.
Niliandika barua kwa dunia kuomba msaada wa watu na mali.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nilitaka dunia ichukukue tahadhari maana jambo hili lingeweza kuwa mlipuko wa dunia nzima.
Leo hii, nachukua nafasi hii kupaza sauti yangu kutoa Ujumbe wa mshikamano.
Takribani miaka sita iliyopita, nilielezea namna uchumi wa Liberia ulivyokuwa mbaya na namna mfumo wa huduma za kiafya ulivyokuwa dhaifu.
Hali iliyofanya ugonjwa kusambaa kwa kasi zaidi,na nikataka kujua namna dunia itachukulia tatizo hili la Afrika ya magharibi , ambayo mfumo wa Afya si salama
Nilisema kuwa ugonjwa usioweza kudhibitiwa, bila kujali ni wapi duniani hata kama ni ndani kiasi gani ni tishio kwa binadamu wote
Uwezeshaji mkubwa wa mali ukiongozwa na Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani pamoja na Marekani ulikuja.

Tuliushinda ugonjwa huu kwa pamoja na matokeo yake leo hii kuna chanjo thabiti zilizofanyiwa utafiti na dawa za kupambana na virusi hivyo ilitokana na ushirikiano wa vichwa vya wanasayansi bora duniani.
Kwenye suala hili la mlipuko wa virusi vya corona, natoa wito uleule kwa wananchi wenzangu duniani. Nafanya hivi nikiwa na uelewa mkubwa kuwa mataifa ya Afrika yamenusurika na makuu. Ni jambo la muda tu ambapo maambukizi haya yatazuru bara ambalo halipo tayari kupambana na virusi hivyo
Inatubidi tuchukue hatua kupunguza kasi ya maambukizi, msululu wa maambukizi pamoja na kusawazisha hali ya sasa.
Ni wazi kuwa kuwa kuna hali ya kujisahau ilikuwepo katika hatua za awali za kuzuia maambukizi ya virusi hivi kutoka Asia, Ulaya na Marekani
Tiba ilikosekana na muda ulipote.
Taarifa zilifichwa, uaminifu ulikosekana.
'Nilifanya makosa hayo hayo'

Chanzo cha picha, Getty Images
Hofu ilisababisha watu kukimbia na kujificha ili kulinda usalama wao wakati suluhisho la pekee linabaki katika jamii.
Najua.nilifanya makosa hayo yote mnamo 2014 lakini tulijirekebisha na tukashirikiana.
Tusitazame janga hili kwa jicho baya.
Haimaanishi kuwa tupo wenyewe na kila nchi kivyake. Zaidi ni kuwa kuna dalili za muitikio wa kijamii wa kufungwa mipaka ambao unaleta mabadiliko.
Nikitazama kutoka nyumbani kwangu Monrovia, kinachotia moyo leo hii ni uwazi wa wataalamu na suala la kuwa elimu, uvumbuzi wa kisayansi, vifaa, dawa na wataalamu vinatumiwa kwa pamoja
Inatokea katika mataifa na zaidi katika mipaka ya kimataifa. Inatakiwa hatua madhubuti zilichukuliwe ambapo kila mtu na kila taifa linatakiwa kufanya kazi yake
Utambuzi huu ulitufanya tupate udhibiti wa Ugonjwa huo Magharibi mwa Afrika
Matokeo hayo yalituimarisha kuwa na jamii ya kukabiliana na magonjwa.
Bi.Ellen anaamini kwa dhati kwamba hii ndio njia ambayo sisi sote tupo.
Nina imani katika roho ya mtu binafsi ambayo viongozi huibuka wakati wa shida katika kila ngazi ya jamii na kwamba tofauti zetu za kidini na kijamii zinaonekana kulinganisha na umoja wetu imani kali ya sala zetu na imani yetu kwa Mungu.
Sisi sote tusikateta tamaa katika wiki chache zijazo, anaomba afya na ustawi wa raia wote na ulimwengu na naomba kila mtu akumbuke kuwa ubinadamu wetu sasa hutegemea ukweli, muhimu kwamba maisha yaliyo Sawa ni maisha katika huduma kwa wengine.












