Virusi vya corona: Je virusi vya corona ni majaribu kiasi gani kwa Afrika?

Chanzo cha picha, Reuters
Afrika imethibititsha visa zaidi ya 10,000 vya virusi vya corona pamoja na vifo zaidi ya 500 kulingana na Kituo cha Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa (ACDC).
Huku idadi ya wanaoambukizwa ikiongezeka kila siku, baadhi wanahofia kwamba kitovu cha virusi hivyo huenda kukahamia barani Afrika.
Licha ya juhudi za kufunga miji nan chi kadhaa, licha ya ufadhili wa kununua vifaa vya kujikinga, vifaa vya kupimia virusi hivyo, na mashine za kupumilia kutoka china, kitu kimoja kilichowazi ni kwamba Afrika bado haijafanikiwa kupunguza maambukizi haya na uwezo wa kufikia hilo unaendelea kupungua.
'Hatua kuchukuliwa kuchelewa'
"Kile kinachoonekana ni kwamba fursa hii ni sawa na kusema haip tena au kwa baadhi ya nchi inaendelea kutoweka," amesema Dr Michel Yao, msimamizi wa huduma za dharura katika Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Afrika.
"Pia kinachotia wasiwasi zaidi kwasasa ni kwamba wanaendelea kushindwa kudhibiti virusi hivyo na sasa imefikia hatua ya maambukizi ya wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa wenyeji. Lakini pia baadhi ya nchi zinachelewa kuchukua hatua…kuhakikisha wengi zaidi wanajumuishwa katika kukabliana na maambukizi, kufunza wengine zaidi, fikiria kuhusu uwezekano wa kukabiliana na virusi hivyo."

Chanzo cha picha, AFP
Ni vigumu sana kulinganisha maeneo yenye utamaduni uchumi usafiri na miundi mbinu tofauti, lakini ulinganisho mwengine ni muhimu sana kwa wakati uu.
Zingatia idadi ya wale wanaothibitishwa kuambukizwa kila siku kote duniani, Afrika inaonekana kufanikiwa kukabili maambukizi ikilinganishwa na Marekani na Ulaya hadi kufikia sasa.
Lakini ikilinganishwa na Asia, ambako baadhi ya nchi zinaonekana kupunguza maambukizi kila siku tena kwa haraka, ni kwamba Afrika haiko vizuri.
Usambaaji wa maambukizi katika jamii
Pengine ulinganisho mzuri unaweza kuwa Mashariki ya kati. Katika eneo hilo maambukizi yameongezeka kwa idadi ya juu mno pamoja na wale wanaokufa kila siku, pia limerekodi visa zaidi ya 78,000, kulingana na Shirika la Afya Duniani.
Karibu kila nchi ya Afrika imeripoti kupata maambukizi hayo ambayo kwa nchi nyingi yalianza na wale waliotoka nchi za nje lakini kwasasa yameenea katika jamii mabimbali.
Mambo mengi yanafanya kuwa vigumu kutabiri kitakachotokea, lakini vile vinavyoweza kubainiwa kama visa vibaya zaidi bado havijatokea. "Visa hivyo vinaweza kuongezeka," amesema Dr Yao, "hata mara tatu zaidi, au kuongezeka mara 7 hadi 10 kulingana na vile tulivyo kwa wakati huu".

Katika kipindi cha wiki mbili za mwisho wa Machi, Afrika Kusini ilishuhudia ongezeko la visa hivyo mara 20. Ili kukabiliana na hali hiyo, Rais Cyril Ramaphosa alitangaza amri ya kutotoka nje kwa wiki tatu kuanzia Machi 27.
Na amri hiyo imeongezwa hadi mwisho wa Aprili wakati ambapo visa vipya vya maambukizi vimeanza kupungua kila siku ingawa ni mapema mno kuhitimisha kuwa amri ya kutotoka nje ndo imesadia kukupunguza idadi hiyo.
Cha msingi ni kuongeza uwezo wa kupima watu virusi hivyo nchini Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, EPA
Hadi kufikia sasa nchi hiyo imepima watu 60,000 kubainisha ikiwa wana Covid-19, ugonjwa unaosababishwa na virusi hivyo na kwasasa shughuli ya kupima imefikia karibu watu 5,000 kwa siku, kwa mujibu wa Waziri wa Afya Zweli Mkhize.
Lakini ukilinganisha na nchi zingine zilizoathirika zaidi na virusi hivyo, kiwango hicho cha upimaji wa watu kwa siku bado kiko chini. Italia moja ya nchi zilizoathirika zaidi duniani - ina idadi sawa ya watu na Afrika Kusini ilikuwa inapima watu zaidi ya 700,000 kwa siku.
Na cha kusikitisha zaidi, idadi ya wanaopimwa kwa siku katika nchi zingine barani Afrika ni ya chini hata kuliko Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, AFP
Nigeria na Kenya zote zimekuwa zikipimwa angalau watu 5,000 kwa siku. Linganisha idadi hiyo na Korea Kusini ambayo ina idadi karibia 6000,000 ambayo wengi wanaichukulia kama miongoni mwa zilizofanikiwa katika kukabiliana na virusi vya corona.
"Idadi ya wanaopimwa inaongezeka lakini naona kwamba tunaweza kuongeza idadi hiyo hata zaidi," amesema Dr Abdhallah Ziraba, mtafiti wa sayansi na mtaalamu wamagonjwa ya maambukizi katika Taasisi ya Utafiti wa masuala ya Afya barani Afrika.
Changamoto za upimaji
Nchi za Afrika zimekuwa zikipigania kuongeza uwezo wao wa kupima virui vya corona.
Mawaziri wa afya wamekuwa wakijitahidi kubadilisha maabara za kibinafsi hadi vituo vya kupimia ugonjwa wa Covid-19 pamoja na maabara zingine kubwa kubwa kama vile Taasisi ya Pasteur mjini Dakar ambayo kupitia kituo cha udhibiti na uzuiaji wa magonjwa ACDC imefanikiwa kuandaa warsha za kutoa mafunzo ya kukabiliana na Covid-19 kwa wafanyakazi wa maabara katika eneo hilo.
Lakini bado juhudi hizo hazitoshi.
Changamoto nyengine ambayo imekuwa ikishuhudiwa ni usambazaji wa vifaa muhimu katika upimaji wa virusi vya corona.


Hivi karibuni bilionea wa China Jack Ma alitangaza kutoa ufadhili wa zaidi ya vifaa milioni moja vya kupimia kwa nchi za Afrika. Bado haijafahamika ikiwa hilo linajumuisha vifaa kamili vya kufanyia kipimo cha virusi vya corona lakini ikiwa ni hivyo, ufadhili huwa utakuwa muhimu sana uimarishaji wa shughuli ya kupima ugonjwa wa Covid-19 barani humo.
"Tunajua kwamba kuna changamoto katika utengenezaji wa vifaa vya kupimia, gharama ya kupimwa na usafirishaji lakini hatuwezi tu kuridhika na kufikiria tu kwamba sasa watu hawatakufa," amesema Dr Ziraba.
Kulingana na utafiti ulioandikwa na wataalamu wa magonjwa ya kuambukizwa London na Johannesburg, kifo kimoja kinaweza kumaanisha kwamba nchi tayari ina visa vya vifo mia au hata elfu kadhaa

Idadi kubwa zaidi ya vipimo inayoweza kufanywa, hilo litafanya bara la Afrika kujiamini zaidi kwa data zake na mifuo iliyopo ya kukabiliana na janga hilo la corona.
Moja ya matatizo makubwa Afrika katika wiki zijazo ni namna hasa ya kukabiliana na virusi hivyo.
Hadi kufia sasa, mkakati wa Afrika Kusini wa kutekeleza amri ya kusalia ndani umeonesha matumaini. Na pia nchi zingine zimeigiza mkakati huo.
Nchi ya Afika yenye idadi kubwa ya watu, Nigeria, imetangaza amri kama hiyo kwa mji wa Lagos, na kuzuia watu kuanzia kusafiri hadi kutekeleza shughuli zingine za msingi.

Chanzo cha picha, Reuters
Moja ya mji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa, pia nao umetangaza kutekeleza amri ya kusalia ndani.
Dakar nchini Senegal na Nairobi nchini Kenya zimetangaza amri ya kutotoka nje usiku na kuruhusu watu kuendelea kufanyakazi mchana lakini zimezuia shughuli zinazoruhusu kutangamana kwa watu na usafiri wa nyakati za usiku.
Hatahivyo, tishio kubwa la kutangaza amri ya kusalia ndani kabisa ni hatari ya kusitisha shughuli za kiuchumi kote barani humo.
Zaidi ya theluthi moja ya watu barani Afika ni umaskini.
Huku wengi ya wale wanaoishi maeneo ya vijijini wakiwa na uwezo wa kufanya ukulima lakini karibu asilimia 20 wanaishi mijini na wanategemea vibarua kulisha familia zao.












