Coronavirus: Changamoto zilizopo Afrika

Chanzo cha picha, AFP
Mlipuko wa virusi vya corona si tishio kwa mataifa ya Afrika, kwa sasa ni uhalisia tu kulingana na mataifa mengi duniani kuendelea kuathirika na ugonjwa huo.
Mataifa ya Afrika mashariki yamekuwa ya mwisho kuthibitisha kuwa na maambukizi ya corona: Sudan imethibitisha kuwa mwanaume mmoja mwenye miaka 50 amefariki kutokana na virusi vya corona, huku Ethiopia imesema kuwa raia wa Japan aliyekuwa nchini humo amekutwa na maambukizi ya Covid-19.
Taarifa siku ya Ijumaa zilieleza kuwa mwanamke mmoja nchini Kenya , ambaye alikuwa ametoka safari Marekani na Uingereza alifika jijini Nairobi akiwa na virusi hivyo.
Picha na video ziliwekwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha namna watu walivyofurika madukani kununua sabuni za kunawia mikono na chakula.

Chanzo cha picha, AFP
Shirika la afya duniani limetoa tahadhari kuwa nafasi ya kujitayarisha kukabiliana na janga hili haupo tena wakati mianya ya inayochangia kutokea kwa tatizo bado ipo.
"Kila nchi inaweza kubadili chanzo cha maambukizi haya kwa kuimarisha hatua za dharura ambazo wanaweza kuchukua," alisema Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa shirika duniani kwatika ukanda wa Afrika.
Huu ni wakati ambao kila taifa linapaswa kuwa tayari kwa mapokeo ya kukabiliana na janga hili.
Wataalamu bado wanaumiza vichwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Kesi za maambukizi zilizothibitishwa zinahusisha watu kutoka Ulaya mpaka Amerika ya Kaskazini.
Shirika la afya duniani limesema kuwa wakati maambukizi ya ndani yakiwa bado yako chini, kwa watu ambao hawana historia ya kusafiri, dunia inapaswa kutafuta mikakati bora zaidi kukabiliana na janga hili.
Hii ikiwa ina maanisha kuwa ili kupunguza kesi za corona watu wanapaswa kugunduliwa kwa haraka kuwa wana maambukizi, kuwatibu kwa kufuatilia watu waliotangamana naye wakati amepata maambukizi na kuwatenga .
Ingawa kuna idadi ndogo ya maambukizi barani Afrika lakini wataalamu pia ni changamoto.
Baadhi wanadhani kuwa hali ya hewa ya Afrika ni vigumu kwa wao kupata maambukizi hayo mapya.
John Nkengasong, kiongozi wa kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa anasema kuwa takwimu za kuthibitisha hilo ziko kwenye maelezo tu na hakuna uthibitisho wowote.
"Lakini tunafahamu kuwa Covid-19 ni sehemu ya virusi vya corona ambapo husababishwa na mafua," aliiambia BBC.
Hii ni vyema kufahamu kuwa virusi vya corona huwa vinaweza kuzuilika kwenye maeneo ya hali ya joto kali.
Lakini Dkt. Nkengasong aliainisha kuwa matokeo ya mlipuko wa ugonjwa wa corona katika nchi zenye hali ya kitropiki kama Thailand.
Kama virusi hivi vikifuatiliwa na kuhusishwa na virusi vingine vya wakati wa msimu wa baridi, hii inahusisha upande wa Afrika kusini ambao huwa ni msimu wa baridi ", Dkt. Moeti aliiambia BBC.
Kitu kimoja ambacho kinaiweka Afrika kuwa mbele zaidi ya mataifa mengine ya dunia ni kuanza kupima watu wanapoingia uwanja wa ndege na maeneo mengine ya kuingia ndani ya nchi.
Hii ni kwa sababu ya miundo mbinu ya kukabiliana na hali hii ilikuwa tayari kwa sababu ya mlipuko wa Ebola nchini DRC ambao unaonekana kumalizika sasa.
Kisa cha kwanza cha corona Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kiligunduliwa namna hii.


Lakini dalili nyingi zinazojitokeza siku chache baada ya kuwasili, mfano mgonjwa wa kwanza wa corona Nigeria: Muitaliano alivyowasili mjini Lagos. Ambaye alitembelea jimbo la Ogun kabla hajawasili na kuanza kuumwa.
Watu aliohusiana nao walitafutwa na kila mmoja alikutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Bara la Afrika pia limepata muda wa kuona jinsi nchi nyingine zilivyokabiliana na virusi hivi vipya vya corona na kujiandaa.
Wakati wa janga hili, imeelezwa kuwa baadhi ya dalili za maambukizi zimeainishwa.
Hili ndio jambo ambalo wizara ya afya ya Afrika Kusini, imewaweka karantini watu ambao walikutwa na maambukizi na kushauri wengine ambao wanajiona kuwa na dalili za namna hiyo kutafuta tiba.
Mpaka sasa, nchi ambazo zimethibitisha kuwa na kesi hizo zinaonekana kufanikiwa kukabiliana na tatizo hilo.
Misri, Algeria na Tunisia zimeripotiwa kuwa na maambukizi ya ndani ya nchi.
Pia unaweza kutazama namna sahihi ya kunawa mikono:
Kuenea kwa kasi kwa maambukizi hayo kati ya mtu na mtu, ni jambo ambalo wataalamu wa afya barani Afrika wana hofu nalo kwa sababu kunaweza kufanya tatizo kuwa kubwa zaidi na kuzidi uwezo wa mfumo wa afya.
Duniani kote, kuna uwiano wa kati ya umri na makali ya maambukizi ya corona .
Wazee wako kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi.
"Kuna uwezekano kuwa idadi kubwa ya vijana Afrika inaweza kuachwa kwenye kasi ya maambukizi haya," alisema Dkt Nkengasong, kwa sababu bara la Afrika lina idadi ya vijana wengi zaidi ya wazee.
Maambukizi ya virusi vya Ukimwi Afrika
Lakini wasiwasi umeibuka kuhusu watu wenye upungufu wa kinga mwilini, wakiwemo watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.
VVU tayari imepunguza kinga ya mwili, na kuacha mwili kupata maambukizi kiurahisi na kumfanya mtu kuwa na UKIMWI.
Zaidi ya watu milioni 32 wamekufa kutokana na virusi vya Ukimwi tangu virusi hivyo vibainike mapema mwaka 1980, kwa mujibu wa UNAids.
Karibu watu milioni 38 wanaishi na virusi na wengi wao wakiwa wametokea barani Afrika.
"Ni muhimu kusisitiza kuwa hakuna uthibitisho kuwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi wako kwenye hatari zaidi ya kupata virusi vya corona au wakipata watakuwa katika wakati mgumu zaidi," alisema mkuu wa UNAids Bi. Winnie Byanyima.
Aliainisha kuwa kuna hofu kwamba watu wanaoishi na Ukimwi wanapaswa kuchukua hatua za tahadhari kama watu wengine.
Ingawa alitoa tahadhari kuwa watu wenye virusi vya ukimwi wanapaswa wasisahaulike wakati mataifa yanazingatia namna ya kukabiliana na corona.
Tafiti ya UNAids imebaini kuwa wakati mlipuko wa virusi vya corona ulipotokea nchini China, watu walioathirika ambao walikuwa wanaishi na virusi vya Ukimwi walibaini kuwa ni vigumu kwa wao kukabiliana na hali hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vilevile alitaka tafiti zaidi kufanyika ili kujua uhusiano wa VVU na virusi vipya vya corona.
Dkt Nkengasong alisema kuwa wasiwasi wake upo kwenye mchanganyiko wa maambukizi hayo na magonjwa mengine.
"Si virusi vya Ukimwi tu bali kuna kifua kikuu na malaria pia," alisema.
Nina matumaini kuwa wakati dunia ikikabiliana na Covid-19, basi magonjwa makubwa yanayoathiri Afrika yasisahaulike.
Magonjwa hayo matatu hatari barani Afrika yanaweza kupelekea kuwa na vifo vingi zaidi.
Corona si kama Ebola, hili ni janga la dunia ikumbukwe.
Hivyo mataifa yanayoendelea yanapaswa kupambana yenyewe maana kila nchi inakabiliana na tatizo la upande wake pia.













