Virusi vya corona : Hatari ya kuwepo kwa dawa bandia katika nchi za Afrika

Idadi kubwa ya dawa bandia zinazohusishwa na virusi vya corona zinauzwa katika nchi zinazoendelea, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa tahadhari.
Uchunguzi wa BBC ulipata dawa bandia zinazouzwa Afrika, na wafanyabiashara bandia wakitumia mianya iliyo kwenye soko.
WHO imesema kutumia dawa hizi kunaweza kuwa na "athari mbaya".
Mtaalam mmoja alionya kuhusu "janga la bidhaa za chini ya kiwango na za bandia".
Ulimwenguni kote, watu wanahifadhi dawa za msingi. Hatahivyo, pamoja na wazalishaji wawili wakubwa zaidi wa vifaa vya matibabu duniani na India- wakati huu wa kutotoka nje, mahitaji sasa yanazidi usambazaji na mzunguko wa dawa bandia unaongezeka.
Katika wiki hiyo hiyo Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza ugonjwa wa ugonjwa wa corona kuwa janga, Operesheni Pangea, kitengo cha kupambana na uhalifu wa dawa ulimwenguni cha Interpol, kikamatawatu 121 katika nchi 90 ndani ya siku saba, na kukamata dawa hatari zenye thamani ya zaidi ya pauni milioni 11.
Kuanzia Malaysia hadi Msumbiji, maafisa wa polisi walikamata maelfu ya barakoa bandia na dawa bandia, ambazo nyingi zilidaiwa kuwa na uwezo wa kutibu virusi vya corona.

Chanzo cha picha, Getty Images
''Biashara haramu ya vifaa vya tiba wakati huu wa janga, inainesha hali ya kutojali maisha ya watu'', anasema Katibu mkuu wa Interpol Jurgen Stock.
Kwa mujibu wa WHO, biashara hii pana ya dawa bandia, ambayo inahusisha dawa ambazo zinaweza kuharibiwa na vijidudu, ambazo hazina viambato vinavyofanya kazi, au kuwa na viambato visivyofaa ni ya thamani ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 30 katika nchi zenye kipato cha kati na cha chini.
''Dawa hizi bandia zitashindwa kutibu ugonjwa kama inavyotarajiwa'', alisema Pernette Bourdillion Esteve, kutoka kitengo cha WHO kinachoshughulika na udhibiti wa vifaa tiba bandia.
''Lakini hatari kubwa ni kuwa zinaweza kusababisha madhara, kwa kuwa zinaweza kuwa na viambata vyenye sumu.''
Usambazaji dawa
Soko la dawa la dunia lina thamani ya zaidi ya dola trilioni moja za Marekani.
Kuanzia kwa atengenezaji wakubwa katika maeneo kama China na India, kuelekea kwa wafungashaji barani Ulaya, Afrika Kusini au bara Asia, kwenda kwa wasambazaji wanaozituma dawa hizo kwenda kwenye kila nchi duniani.
''Pengine hakuna kitu kingine kinachoigusa dunia nzima kwa pamoja kama dawa'' alisema Esteve. Hatahivyo, wakati dunia ikiwa imejifungia ndani, mlolongo wa usambazaji sasa umeanza kukatika.
Kampuni za dawa nchini India zimeiambia BBC kuwa kwa sasa zinazalisha asilimia 50-60 ya uwezo wao wa kawaida.
Kampuni za India zinasambaza asilimia 20 ya dawa muhimu kwenda Afrika. Mataifa mengi yameathirika barani humo.

Mwanafamasia mjini Lusaka, nchini Zambia,Ephraim Phiri anasema amekuwa akikiona kikwazo hicho.
''Dawa zimeanza kuisha na hatuna nyingine .Hakuna tunachoweza kufanya. Imekuwa vigumu kupata dawa….hasa dawa muhimu kama antibiotic na za kupambana na malaria.''
Wazalishaji na wasambazaji wanapata tabu kwa kuwa viambata ghafi kwa ajili ya dawa kwa sasa ni ghali mno, baadhi ya kampuni hawawezi kukabiliana na gharama ya kuendelea na uzalishaji.
Mzalishaji mmoja nchini Pakistan anasema alikuwa akinunua viambata ghafi kwa ajili ya dawa za kutibu malaria iitwayo hydrochloroquine kwa gharama ya dola 100 kwa kilo moja .Lakini hii leo imeongezeka hadi dola za Marekani 1,150 kwa kilo moja.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kutokana na ongezeko la nchi zinazotekeleza amri ya kutotoka nje, si tu kupungua kwa uzalishaji ni tatizo, bali pia ongezeko la mahitaji, watu wakinunua dawa hizo kwa wingi duniani kwa ajili ya kuzihifadhi.
Kupungua kwa usambazaji wa dawa na ongezeko la mahitaji, WHO imeonya hatari ya ongezeko la hatari la uzalishaji na uuzaji wa dawa bandia.
''Ikiwa usambazaji hautakidhi mahitaji,'' alisema Esteve, kutoka WHO, ''husababisha kuwepo kwa mazingira ya kuwepo kwa dawa bandia zisizo na viwango bora kuanza kukidhi mahitaji ya watu.''

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:
Dawa bandia
Akizungumza na wanafamasia na kampuni za kutengeneza dawa duniani, usambazaji wa dawa za kupambana na malaria duniani uko kwenye tishio.
Tangu rais wa Marekani, Donald Trump alipoanza kuhusisha chloroquine na Hydroxychloroquine na virusi vya corona kumekuwa na ongezeko kubwa la uhitaji wa dawa hizi ambazo kwa kawaida hutumika kupambana na malaria.
WHO imeeleza mara kwa mara kuwa hakuna ushahidi kuhusu dawa hizi kutumika kupambana na covid-19.
Hata hivyo Rais Trump alisema'' utapoteza nini? Tumia.''
Wakati mahitaji ya dawa yakishika kasi, BBC imebaini uwepo wa dawa nyingi bandia aina ya chloroquine zikiwa zinasambazwa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na Cameroon.
WHO pia imegundua dawa bandia zikiuzwa nchini Niger.
Kwa kawaida chloroquine huuzwa kwa dola za Marekani 40 kwa vidonge 1,000. Lakini wanafamasia nchini DRC walikuwa wakiuza kwa dola 250.
Dawa zilizokuwa zinauzwa zinadaiwa kutengezwa nchini Ubelgiji na kampuni ya "Brown and Burk Pharmaceutical limited". Hata hivyo kampuni hiyo iliyosajiliwa nchini Uingereza imekana kuhusika na dawa hizo. ''Hatutengenezi dawa hii, ni bandia.''












