Ni kwanini watu 95 hufa kila siku katika nchi hii?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaharakati nchini Mexico watatembea mwendo wa zaidi ya kilomita 130 'wakifanya matembezi ya amani' kupinga ghasia katika nchi hiyo
Mauaji yamefikia viwango vya hali ya juu nchini Mexico, huku watu 95 wakiuawa kila siku nchini humo- hii ikimaanisha kuwa mtu mmoja huuawa kila baada ya dakika 15.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, kulikuwa na mauaji ya watu 34,582 mwaka 2019, ikiwa ni idadi ya juu zaidi ikilinganishwa na wakati rekodi za mauaji hayo zilipoanza kuchukuliwa mnamo mwaka 1997.
Idadi hiyo ikilinganishwa na mauaji ya mataifa mengine , wapiganaji wapatao 11,000 na raia waliuawa katika vita vilivyotokea nchini Syria mwaka 2019, kwa mujibu wa taasisi ya uangalizi ya Haki za binadamu nchini Syria.
Lakini Mexico ni hatari kwa kiwango gani na ikoje ukilinganisha na mataifa mengine ?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mitandao ya wauzaji wa madawa ya kulevya nchini Mexico imekua ikilaumiwa kwa kuchafua sura ya nchi inayoifanya kuwa moja ya mahala hatari zaidi duniani.
Mapema mwezi huu, wanamuziki wazawa walipigwa risasi na kuchomwa moto magharibi mwa Mexico katika shambulio ambalo linaaminiwa kufanywa na mtandao wa walanguzi wa dawa za kulevya.
Waathiriwa, walikua na umri wa kati ya miaka 15 na 42, walikua wakirudi kutoka katika sherehe wakati waliposhambuliwa katika mji wa Chilapa katika jimbo la Guerrero.
Mwezi Novemba watu tisa wa familia ya yenye asili ya Mexico na Marekani kutoka dini ya Mormon - akina mama watatu na watoto sita - waliuawa katika shambulio lililofanywa na mtandao wa magenge yenye silaha- jambo lililoibua hisia kali na raia wa nchi hiyo wa ndani na nje walitoa wito wa kufanyika kwa mageuzi.
Kufuatia tukio hilo, wanaharakati wawili maarufu - Javier Sicilia na Julian LeBaron - walitoa wito wa kufanyika kwa matembezi ya amani siku ya Alhamisi tarehe 23 katika mji wa Merelos na kuendelea kwa siku tatubaadae katika mji mkuu , Mexico City.

Chanzo cha picha, Getty Images
Je mauaji ni mabaya kiasi gani ikilinganishwa na nchi nyingine?
Licha ya takwimu za kutisha, kiwango cha mauaji nchini Mexico bado ni cha chini ikilinganishwa na mataifa mengine.
Imewekwa katika nafasi ya 19 duniani miongoni mwa mwa mataifa yenye kiwango cha juu cha vifo, kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Benki ya dunia, ikiwa na mauaji ya kukusudia 25 kati ya wakazi 100,000 mwaka 2017.
Nchi iliyo juu kwenye orodha ya mauaji ni El Salvador - kiwango chake kilikua ni zaidi ya Mexico mara dufu ikiwa na vifo 62 vya makusudi kwa wakazi 100,000 mwaka 2017, licha ya kwamba idadi hiyo ilishukla kwa kiwango kikubwa , kwa mujibu wa data rasmi.

Chanzo cha picha, AFP
Katika mzozo ulioikumba Venezuela, vifo vilikua ni vya juu zaidi vikiwa ni 60 kwa watu 100,000 mwaka 2019, kwa mujibu wa Shirika lisilo la kiserikali linalofuatilia usalama wa nchi la Venezuela Observatory of Violence.
Takwimu za mauaji nchini Nigeria haziko wazi , lakini Umoja wa Matifa unakadiria kuwa viwango vya mauaji ya watu kuwauwa watu wengine kati ya 2013-2016 vilikua ni 34 kwa watu 100,000.
Afrika Kusini iliwekwa katika nafasi ya tisa - na pia pia mahala pabaya sana kwa ghasia dhidi ya wanawake.
Jedwali linaloonyesha viwango vya mauaji katika baadhi ya nchi:
Samuel Gonzalez Ruiz, mkuu wa ofisi ya Mexico inayoratibu juhudi za usalama wa umma alielezea mauaji katika nchi hiyo kama "tatizo la kimaeno , na wala si tatizo la kitaifa".
Takwimu zinaonyesha kwamba nyingi kati ya ghasia hizo ziko latika maeno fulani yaliyokithiri kwa uhali ambako magenge yanaendesha harakati zake au yanapigania eneo fulani.
Kinyume na matarajio, meneo yenye shughuli za utajiri ya Yucatán na Baja California Sur yalirekodi viwango vya chini vya uhalifu.
Unaweza pia kusoma:
Mauji nchini Mexico yamekua yakiongezeka tangu wakati huo. Rais Felipe Calderón alianzisha " vita dhidi ya mihadarati " mwaka 2006, na kuwapeleka wanajeshi zaidi ya 50,000 na vikosi vya majini na pia polisi kukabiliana na mitandao ya magenge ya madawa ya kulevya.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika kipindi cha miaka sita ya urais wake, takwimu rasmi za watu waliouawa katika matukio yaliyohusisha ghasia za dawa za kulevya ilikua ni 60,000. Wengi wanakadiria kuwa idadi inaweza kuwa ya juu zaidi.
Rais wa sasa Andrés Manuel López Obrador aliahidi " kurejesha amanina kumaliza vita " juu ya mihadarati.
Lakini mkakati wake wa kubuni kikosi cha kitaifa cha ulinzi kwa ajili ya vita umekosolewa kwa kukosa mwelekeo na kwamba hauna tofauti sana na sera ya mtangulizi wake.
Wakosoaji wake wanadai kwamba suala la rais kushindwa kuwa na mkakati wa wazi wa kukabiliana na makundi ya uhalifu kuwa na ghasia zaidi.












