Mwaka mmoja wa Tshisekedi: Changamoto katika sekta ya afya DRC, Je hali ikoje?

Chanzo cha picha, Reuters
- Author, Byobe Malenga
- Nafasi, BBC Swahili, DRC
DRC imezongwa na majanga mengi ikiwemo homa ya Ebola ambayo imeua maelfu ya watu na kuyumbisha sekta ya afya nchini humo. Hata hivyo, rais Tsishekedi aliahidi kwamba atapambana na kufanya kila awezalo kuimarisha afya nchini DRC.
Ebola imekuwa changamoto kubwa katika utawala wa rais Felix Tshisekedi, ugonjwa huu wa virusi vyenye maambukizi mabaya na kusababisha kifo, sasa umekithiri kwa zaidi ya mwaka bila kupata ufumbuzi, kulingana na mwandishi wa BBC, Byobe Malenga ambaye amekuwa akifuatili akwa kina hali ilivyo.
Changamoto katika sekta ya afya DRC
Usalama
Mratibu wa kupambana na ugonjwa wa Ebola jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Dr. Muyembe anasema, ''Tulikuwa tunakaribia kumaliza ugonjwa huo wa Ebola, lakini masikitiko ni kwamba usalama mdogo ulituvuruga maana timu za madaktari pamoja na vituo vya kutoa tibu na chanjo dhidi ya Ebola vilishambuliwa mara kadhaa na kusababisha hata vifo vya watu. Kwa hiyo shughuli zilisimama kwa muda na hio ilisababisha maambukizi zaidi kwa sababu akukuwa tena na uchunguzi.''
Kwasababu ya ukosefu wa usalama, chanjo, tiba na hata uchunguzi vimekosekana na bila shaka ugonjwa huu umesambaa.
Watu wanaofanya kazi ya kukabiliana na Ebola, mara kwa mara wamekuwa wakilengwa na na makundi ya watu wanaopinga juhudi zao.
Mhariri wa BBC, Will Ross aliwahi kusema, katika kipindi cha mmoja, wahudumu kadhaa wa afya walishambuliwa na watu wanaopinga kampeini ya kukomesha Ebola.
Inasemekana kwamba hilo lilitokana na imani ya baadhi ya raia kwamba virusi vya Ebola ni njama ya uwongo, hali ambayo imechangia baadhi ya raia kutowaamini wahudumu wa sekta ya afya.

Mwaka mmoja tangu rais Felix Tshisekedi achukuwe hatamu za uongozi wa Jamhuri ya Kidemokrsaia ya Congo, leo tunapiga darubini swala la afya. DRC imezongwa na majanga mengi ikiwemo homa ya Ebola ambayo imeuauwaua maelfu ya na kuyumbisha sekta ya afya nchini humo.
Hata hivyo, rais Tsishekedi aliahidi kwamba atapambana na kufanya kila awezalo kuimarisha afya nchini DRC.
Ukosefu wa usalama umehatarisha hata vyombo vya habari vinahamasisha watu kuhusu ugonjwa huo. Mfano, mwanahabari Bw. Mahamba aliyekuwa akiendesha kipindi cha kuhamasisha watu kuhusu kuhusu Ebola katika kituo cha redio cha kijamii alishambuliwa na watu wasijulikana na kuuawa katika kijiji cha Lwemba mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa DRC.
Aidha wahudumu wa afya pia wamekuwa wakiuawa kama sehemu ya kupinga juhudi zao. matokeo ambayo yamekuwa yakilaaniwa vikali na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu na hata mashirika ya kimataifa.
Siasa
Siasa pia nimoja ya sababu zinazotajwa kuchochea pakubwa ugonjwa huo kutodhibitika, Omar Kavota ni mkurugenzi wa shirika la Amani na kutetea haki za binadamau mjini Beni, ''Leo kuna wale ambao wameteuliwa wabunge wa taifa ama wabunge wa jimbo sababu aliwaambia wananchi kwamba maradhi ya Ebola ni siasa ya rais mstaafu Joseph Kabila...'',
Inasemekana kwamba hotuba za ina hiyo zilikuwa zinaendeshwa katika sehemu mbalimbali wakati wa kampeni
''Hotuba za hizi zilileta uchochezi ya kuwa ni uzushi ama ni namna ya kujitajirisha'', kwa mujibu wa Omar kavota.
Baadhi ya watu wanafikiri muda umewadia kwa wanasiasa kubadili hotuba zao ili kwamba vita dhidi ya ugonjwa huo viweze kufanikiwa.
Surua ama Ukambi

Chanzo cha picha, AFP/Getty
Wakati Ebola ikizidi kuleta shida katika sekta ya afya, kumekuwa na mlipuko mkubwa pia wa ugonjwa wa Ukambi.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa mlipuko huo wa ukambi, ambao unaua kwa haraka zaidi kuliko ugonjwa mwingine duniani, ni tishio kubwa kwa DRC.
Inasemekana kwamba ugonjwa wa ukambi ama Surua umewaua takriban watoto 5000 katika taifa la Jamhuri ya KidemokrasIa ya Congo mwaka 2019, kulingana na mamlaka baada ya ugonjwa huo kusambaa hadi mikoa yote.
Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa ugonjwa huo ndio janga linalosambaa kwa kasi mno.
Miundombinu mibovu inatajwa kuwa moja ya sababu ya vifo vingi kutokana na ukambi. Bi Sela Lulonhga ni daktari katika hospitali ya panzi mjini Bukavu.
''Kwanza watu hawajui ugonjwa wa ukambi ni nini na watu wengi wanakimbilia tiba ya asili badala ya kuja mapema kwenye vituo vya afya ili wapate matibabu kwa haraka. Pia chanjo inakuja lakini inakuja kidogo na watu wote hawapati chanjo hiyo, pia hakuna mahabara na dawa katika sehemu za vijijini.
Je surua ni nini?
Surua ni virusi vinavyosababisha mtoto kuwa na mafua , kuchimua mara kwa mara na kuwa joto mwilini.
Siku chache baadaye mgonjwa anapata vipele mwili mzima ambavyo vinaanza usoni na kusambaa mwilini.
Wengi hupona , lakini surua inaweza kusababisha ulemavu wa muda mrefu. Inaweza kusababisha kifo hususan iwapo utasababisha homa ya mapafu ama uvimbe katika ubongo.
Inakadiriwa kwamba jumla ya watu 110,000 duniani hufariki kutokana na ugonjwa huo kila mwaka.
Nini kifanyike kutibu Surua/ Ukambi
''Kwanza serikali ihakikishe watu wote wamepata chanzo, hata vijijini kutengenezwe maabara na kupeleka dawa ili watu wapate huduma ka haraka na mapema,'' amesema Bi Sela Lulonhga.
Pia inasemekana kwamba kuna sehemu ambapo wahudumu wa afya wamegoma kwasababu ya ukosefu wa mshahara wao. Aidha, Serikali inachangamoto ya kungeza idadi ya wadumu kwendana na idadi ya wagonjwa ili wapate kuelimishwa na kupata huduma stahiki kwa wakati unaofaa.
Matambiko

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni ada ya waafrika kushiriki mazishi kwa wingi, na endapo watazuiwa kuwazika wapendwa wao, hasira ama ghasia zinaweza kuzuka.
Hali hiyo ndiyo iliyokuwa ikiendelea katika maeneo ya mashariki mwa nchi ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo yamekumbwa na ugonjwa hatari wa Ebola.
Mazishi ya mtu yeyote aliyefariki kutokana na ugonjwa huo ambao unaambukiza kwa kasi yanafanyika chini ya ulinzi mkali, ikiwa ni sehemu ya kujaribu kupunguza maambukizi.
Mazishi yenyewe huhusisha watu wachache, ndugu na jamaa wa marehemu huwekwa mbali na kaburi. Wanazuiwa kumuona ama kumgusa mpendwa wao.
hata hivyo hatua hiyo ilikuwa ikizua hadhabu miongoni mwa jamii.
"Tunasikitishwa kuona anazikwa namna hii," Dennis Kahambu amenukuliwa akisema na shirika la habari la AFP wakati akiangalia kwa mbali mazishi ya binamu yake, Marie-Rose katika eneo la Butembo.
Wakati huo huo, wataalamu wa afya wakiomba watu kukomesha matambiko ya jadi wakati wa mazishi ili kuhakikisha mtu hajiweki katika hatari ya maambukizi.












