Wafanyakazi wa kampuni ya Feronia wapata ugumba kutokana na dawa za wadudu - HRW

Chanzo cha picha, Human Rights Watch
Wafanyakazi wanaoathirika na dawa hiyo ya wadudu katika kampuni ya Uingereza inayofadhiliwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo wamelalamikia kuwa na ugumba, kulingana na kundi moja la haki za kibinadamu.
Feronia , ambayo inatawala sekta ya mafuta ya mawese nchini Dr Congo ilikuwa imeshindwa kuwapatia wafanyakazi vifaa vya kujilinda, kulingana na HRW.
Benki ya Uingereza ya CDC inamiliki asilimia 38 ya hisa za kampuni ya Feronia nchini DR Congo. Inasema kwamba Feronia ilikuwa imewekeza pakubwa katika vifaa na kwamba wafanyakazi wake wote walitakiwa kutumia.
Feronia ambayo ni kampuni ya Canada ilisema kwamba inataka kufanya kazi kulingana na viwango vya kimataifa.
Kampuni hiyo iliongezea kwamba imetumia $360,000 kununua vifaa vya kujilinda katika kipindi cha miaka mitatu iliopita , ambavyo wafanyakazi wamefunzwa kutumia, na kwamba iliidhinisha sera inayotaka vifaa hivyo kutumika katika maeneo ya kazi.
Feronia na mshirika wake Plantations et Huileries du Congo (PHC), inaajiri maelfu ya wafayakazi katika mashamba ya mafuta ya Mawese nchini DR Congo.
PHC imepokea mamilioni ya dola kutoka kwa benki ya Ubelgiji , Ujerumani , Uholanzi na Uingereza.
Benki hizi zinaweza kuchukua jukumu muhimu kuchochea maendeleo, lakini wanakandamiza ujumbe huo kwa kushindwa kuhakikisha kuwa kampuni hiyo wanayoifadhili inaheshimu haki za wafanyakazi na jamii katika mashamba hayo, hii ni kulingana na mtafiti wa HRW Luciana Tellez Chavez.
Je HRW lina ushahidi gani?
Katika ripoti kwa jina mchanganyiko wa unyanyasaji kuhusu mashamba ya mawese , HRW imesema kwamba imehoji zaidi ya wafanyakazi 40 na thuluthi mbili kati yao imesema kwamba wamekuwa na ugumba tangu walipoanza kazi hiyo.

Chanzo cha picha, Human Rights Watch
Ugumba - pamoja na ukosefu wa hewa , kichwa kuuma na upungufu wa uzani ambao wafanyakazi wamelalamikia - ni matatizo ya kiafya ambayo husababishwa na dawa za kuuwa wadudu kwa jumla kama inavyoelezewa na wanasayansi , shirika la haki za kibinadamu la HRW limesema.
Wengi pia walikabiliwa na kuwashwa na ngozi , kufura, matatizo ya macho ama hata kukosa kuona - ishara ambazo zinafanana na kile ambacho wanasayansi wanaelezea kuwa athari za kiafya zinazosababishwa na dawa hizo, kundi hilo limeongezea.
Bi Tellez Chavez alisema kwamba wafanyakazi ambao walikuwa wamehojiwa walikuwa wamevalia magwanda yanayopenyeza dawa hizo na sio yale ambayo yanazuia dawa hizo kuingia mwilini.
Iwapo dawa hiyo ya wadudu itamwagika , maji hayo yenye sumu yana uwezo mkubwa kushikana na mwili, aliongezea.
Je ni nini chengine ambacho HRW inasema?
Katika mashamba ya Yaligimba, kampuni hiyo ilimwaga uchafu kutoka kwa kiwanda chake cha mawese karibu na nyumba za wafanyakazi.

Chanzo cha picha, Luciana Téllez-Chávez/Human Rights WAtch
Maji taka ya uchafu huo yalisababisha harufu mbaya na kuingia katika kidimbwi ambapo wanawake pamoja na watoto wanaoga na kuosha vyombo vya kupikia.
Kijiji kilicho eneo hilo na mamia ya wakaazi walisema kwamba mto huo ulikuwa chanzo chao cha pekee cha maji ya kunywa.
HRW inasema kwamba benki hiyo ya maendeleo inapaswa kuhakikisha kwamba biashara wanayowekeza inalipa mishahara ya wafanyakazi
Je benki hiyo ya Uingereza inasema nini?
Katika taarifa , CDC ilsema: Uchafu wa Mafuta ya mawese ,Pome, ni mchanganyiko wa uchafu wa mafuta na yamekuwa yakimwagwa katika mto tangu shamba hilo lilipoanza 1911 na sio hatari kwa maisha ya binadamu.
Kiwanda cha Pome kinawakilisha uwekezaji wa mamilioni ya dola - fedha ambazo kampuni hiyo imechagua kutumia katika makaazi, maji safi, afya na vifaa vya elimu, familia zao na wanachama wengine wa jamii za eneo hilo.
Je Feronia inasemaje?
Kampuni hiyo imesema hali imeimarika tangu kuhusika kwa benki ya Ulaya 2013.
Wafanyakazi sasa wanalipwa vizuri ikiwa ni zaidi ya matumizi ya kilimo nchini DR Congo na kwamba mfanyakazi wa wastani anapokea $3.30 kwa siku - ikiwa ni zaidi ya ya kile ambacho mwalimu wa kawaida hupokea, ilisema.
Pia ilisema kwamba imewekeza pakubwa katika maji safi ya kunywa.













