Mlemavu wa macho adhalilishwa ukumbini, atolewa kwenye kiti kwa nguvu

Chanzo cha picha, PA
Mwanafunzi mmoja asiyeona ambaye aliondolewa katika ukumbi wa majadiliano amefutiwa mashtaka yote kuhusu ya makosa aliyotuhumiwa.
Ebenezer Azamati alizuiliwa na mlinzi alipojaribu kurudi kwenye kiti chake ambacho alikishikilia kabla ya majadiliano kuanza tarehe 17 Oktoba.
Viongozi wa mkutano huo waliombwa kutoa maoni kuhusu tukio hilo.
Mwanafunzi huyo wa shahada ya uzamili kutoka Ghana amesema kitendo alichofanyiwa kimemfanya ahisi kutokaribishwa katika majadiliano hayo, Chuo cha Oxford na hata nchi yenyewe.''
Uongozi wa umoja huo , ambao hautegemei chuo hicho, una mtindo wa kutengeneza hafla za kujadiliana, na wazungumzaji huzungumzia mambo ya tangu mwaka 1823.
Kikundi cha jamii ya watu weusi kimesema Bwana Azamati ambaye ana matatizo ya kuona alizuiliwa kwa nguvu kuingia katika majadiliano hayo, muda mchache kabla ya mjadala kuanza.
Kimeendelea kueleza kuwa alifika katika jengo la Frewin mapema ili kujihifadhia nafasi ndani ya chumba hicho, na baadaye alirudi chuoni.
Mlinzi alimfuata mwanafunzi huyo pale alipojaribu kurudi katika kiti chake, hivyo Azamati alikaa kwenye kiti kingine ambacho alipewa na mtu mwingine, kabla ya mwalimu kujaribu kumuondoa.
Kikundi cha jamii hiyo kilisema ''hata kama angeingia baada ya majadiliano kuanza, bado hakustahili kufanyiwa vitendo kama hivyo''
Nwamaka Ogbonna, ambaye ni rais wa Chama cha watu weusi katika chuo kikuu cha Oxford amesema mlinzi alimwambia bwana Azamati kuwa hawezi kuingia ndani ya chumba hicho kwasababu kilikuwa kimejaa, licha ya kuwa wanafunzi walikuwa na viti walivyoshikilia.
Bi Ogbonna amesema ''kusema kwamba alitakiwa kuondoka kisa hamna viti si kitu cha kubishana nacho kwasababu watu wanaruhusiwa kusimama.''
'' Nafikiri kila mtu ameshangazwa''
'Sio kitu cha uungwana '
Kipande cha video kilichosambaa mitandaoni kinaonyesha majibishano kati ya mlinzi na Bw. Azamati ndani ya ukumbi huo kabla ya walimu kwenda kumkamata.
Bw Azamati alikuwa amefika kusikiliza mjadala kuhusu mada iitwayo ''Nyumba hii haina imani na serikali ya malikia'' ambayo wanachama kutoka vyama na wanasiasa mbali mbali walijadili.
Mwanafunzi huyo kutoka shule ya mtakatifu John, ambaye anasomea masomo ya mahusiano ya kimataifa, amesema ''alitendewa kama mwanadamu asiyestahili haki.''
Baada ya makosa ya Bw Azamati kkatiwa rufaa siku ya jumamosi, Rais wa kikundi cha majadiliano hayo ya Oxford Brendan McGrath, aliomba msamaha kikundi cha jamii ya watu weusi kwa ''usumbufu na uchafuaji wa jina wa namna yoyote'' kwa mwanafunzi huyo.
Mwanasheria anaemwakilisha Bw. Azamati, Helen Mountfield amesema kuna mazungumzo yanayoendelea kuhusu hatua zitakazochukuliwa kuhusu makosa yaliyojitokeza kwenye tukio hilo.
Chuo hicho kiliandika katika ukurasa wake wa twitter kikionyesha kumuunga mkono Bw Azamati na kusema ilisambaza malalamiko yaliyooneshwa na watu kuhusu video ya mwanafunzi huyo.''














