Raia mwenye ulemavu wa Kenya ameilaumu Ethiopian Airlines kumpuuza

Chanzo cha picha, Harun Hassan /Twitter
Mkenya aliye na ulemavu , amelilaumu shirika la ndege la Ethiopia, baada ya aliachwa na wafanyakazi wa uwanja wa ndege ambao walikataa kumsaidia kupanda ndege kutoka uwanja wa Jomo Kenyatta, Nairobi, kwenda Marekani.
Katika ukurusa wake wa twitter na Facebook, mwandishi na mwaharakati na haki za walemavu Harun Hassan alisema alidhalilishwa "bila kujali", huku mfanyakazi mmoja akimwambia: "Tafadhali, hatuna msaada kwa mtu mwenye mlemavu anayesafiri peke yake . "
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Bwana Hassan amesema kuwa tikiti yake inaonyesha wazi kuwa yeye ni mtumiaji wa kiti cha magurudumu ambaye alikuwa akisafiri peke yake.
"Waliniacha peke yangu na kunitekeleza," aliandika.
"Kwa kweli hii inakwenda kinyume na sera na miongozo ya Mamlaka ya Uwanja wa Ndege wa Kenya na sheria zingine za kusafiri za walemavu za kimataifa ambazo ndege hii inatakiwa kuzifuata," alisema.
Karibu saa 10 baada ya kuposti maoni yake, ndege ya Ethiopian Airlines ilimfikia, ikaomba msamaha na kumuomba aendelee na safari yake ya economy class. Lakini alisema kuwa shirika hilo la ndege lilimtaka atoe maadhishi yake kwenye mitandao ya kijamii ya Twitter na Facebook kuhusu tukio hilo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Bwana Hassan alisema kuwa ameamua kusafiri kwa ndege nyingine kwenda Washington DC.
Mwanaharakati alisema hii ni mara ya kwanza kwake kuchapisha hadharani juu ya "ukosefu wa haki" ambao mara nyingi amekuwa akikabilina nao.
"Kwa kweli kila siku mimi hukutana na changamoto na ubaguzi - nyingine zenye kusikitisha zaidi ya hii. Lakini , ujumbe huu nimeutuma kwa ajili ya mamilioni ya watu wengine ambao hhubaguliwa sababu 'muonekano' wao ni tofauti na sisi." aliogeza.

Chanzo cha picha, Harun Hassan / Twitter
Alisema kuwa anapenda kuunda jamii yenye umoja zaidi: "Ulimwengu unaojumuisha ni ulimwengu bora kwa wote, amesema.
Baadae Shirika la ndege la Ethiopia kupitia ukurasa wa Twitter lilimuomba msamaha kwa masaibu aliyoyapitia, na kuahidi kuwasiliana na kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3