Mwanamfalme Andrew yuko matatani kwa kujihusisha na mtu anayeshutumiwa kufanya biashara ya ngono

Mwanamfalme Andrew akizungumza na BBC

Chanzo cha picha, Mark Harrison/BBC

Maelezo ya picha, Mwanamfalme Andrew akizungumza na BBC

Mwanamfalme wa York nchini Uingereza ametakiwa kuomba msamaha kwa kuwa na urafiki na Jeffrey Epstein ambaye ni mtuhumiwa, wakili wa washtaki alisema.

Spencer Kuvin, ambaye anawakilisha waathiriwa kadhaa ambao hawajatajwa kwa majina, na kudai kuwa , ''mamlaka ya kifalme imewaangusha''.

Aliyaita mahojiano ya mwanamfalme Andrew na BBC News Night yaliyorushwa siku ya Jumamosi "ya kusikitisha" na "ya kufedhehesha''.

Mwanamfalme alisimamia maamuzi yake kwa uamuzi wake licha ya wakosoaji kuelezea uamuzi huo kuwa kama "ajali ya gari".

Mwanamfalme Andrew kwa sasa ametakiwa kueleza mamlaka za Marekani kuhusu urafiki wake na Epstein- ambaye katika umri wa miaka 66, alijiondoa uhai wakati akisubiri kushtakiwa kwa makosa ya usafirishaji binaadamu kwa ajili ya biashara ya ngono nchini Marekani.

Siku ya Jumatatu, Bwana Kuvin alisema: ''ilikua inasikitisha kuwa yeye (Mwanamfalme Andrew) kutotambua ukubwa wa mahusiano yake na mwanaume huyo mbaya na kuomba msamaha.

''Kuwa na urafiki na mtu aliyetuhumiwa kujihusisha na makosa ya biashara ya ngono na kuamua kuendeleza mahusiano naye, kunaonyesha kutokuwa na ufahamu ni kwa namna gani mtu huyu (Epstein) alichowafanyia wasichana hawa.''

Mwanamfalme Andrew, kushoto, na Jeffrey Epstein

Chanzo cha picha, News Syndication

Maelezo ya picha, Mwanamfalme Andrew amesema kukutana kwake na Epstein mwaka 2010 ilikuwa kusitisha uhusiano wao

Mwanamfalme Andrew aliiambia BBC hajawahi kushuku tabia ya jinai ya Epstein wakati alimpokuwa akimtembelea mfadhili huyo kwenye nyumba zake tatu nchini Marekani

Lakini Bwana Kuvin alisema "hakufikiria kuna njia yoyote" mwanamfalme angeweza kukwepa kujua kinachoendelea, mkuu angeweza kuzuia kuona kinachoendelea, "na wasichana wadogo wakiwa wamefungiwa ndani na nje ya nyumba hizo".

Bwana Kuvin alisema mwelekeo wa washtaki wa Epstein sasa ulikuwa umegeuka kuwa muhimu kwa watu wenye njama dhidi yake.

Imesababisha maswali kuulizwa kuhusu ni jukumu gani alilokuwa nalo mpenzi wa zamani wa Epstein, Ghislaine Maxwell, kwa wasichana wadogo kwa ajili ya mfadhili.

Bi Maxwell amekanusha kuwa na makosa yoyote.

Wakili Lisa Bloom - anayewawakilisha washtaki wengine watano - aliunga mkono wito uliotolewa kutaka mwanamfalme Andrew ahojiwe na mamlaka za Marekani baada ya mahojiano na BBC.

Alikiiambia kipindi cha BBC cha Derbyshire : "Nadhani amefanya mambo kuwa mabaya kwake katika mahojiano haya na nadhani kuna uwezekano mkubwa mamlaka zikataka kuzungumza naye sasa - na wanapaswa kufanya hivyo."

Mwanamfalme Andrew ,Virginia Giuffre na Ghislaine Maxwell

Chanzo cha picha, Virginia Roberts

Maelezo ya picha, Mwanamfalme akiwa kwenye picha na mwanamke anayemshtaki Ghislaine Maxwell jijini London mwaka 2001

Gloria Allred - wakili mwingine, ambaye pia anamwakilisha mmoja wa washtaki wa Epstein - alikiambia kipindi cha ITV cha Morning Britain kuwa: "Sasa yuko katika mahakama ya maoni ya umma, anapaswa kutoa ushuhuda kwa FBI."

Wakati huo huo, waziri kivuli wa biashara kwa tiketi ya chama cha Labour, Barry Gardiner, alisema mwanamfalme Andrew anapaswa kufanya kila awezalo kusaidia waathirika wa Epstein.

Alisema: "Kwa kusema kile anachokijua wakati ambao walikuwa marafiki, inaweza tu kuwa jambo pekee sahihi la kufanya."

Lisa Bloom
Maelezo ya picha, Mwanasheria Lisa Bloom pia amehoji kwanini mwanamfame hakuomba radhi kuhusu mahusiano yake na Epstein

Mwanamfalme Andrew amesema alitaka kuzungumzia masuala haya kwa dhati alipozungumza na BBC.

Katika mahojiano marefu alisema yafuatayo:

Katika siku ambayo Virginia Giuffre nasema alifanya naye mapenzi tarehe 10 mwezi Machi mwaka 2001, alimpeleka binti yake kwenye sherehe kisha wakarejea nyumbani .

Akizungumzia mahusiano yake na mfadhili amesema sasa limekuwa kama ''matatizo ya kiakili'' kwake

  • Atatoa ushuhuda kuhusu uhusiano wake na bi Giuffre ikiwa atalazimika kufanya hivyo, na mawakili wake wamemshauri kufanya hivyo.
  • Hakuwa akifahamu kuhusu hati ya kukamatwa Epstein alipomualika rafiki yake huyo kwenye sherehe ya kuzaliwa ya binti mfalme Beatrice katika kasri la Windsor
  • Hajutii mahusiano yake na Epstein kwa sababu ya fursa aliyoipata ya kujifunza kutoka kwake kuhusu masuala ya biashara