Mwana mfalme: Meghan ajifungua mtoto wa kiume, Harry atangaza

Chanzo cha picha, Reuters
Mke wa mwanamfalme Harry wa Uingereza ajifungua mtoto wa kiume.
Mwanamfalme Harry amesema kuwa yeye na mke wake Meghan "wanafuraha isiyokuwa na kifani" baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa.
Amewashukuru wote waliowaombea na kujiunga nao kipindi cha ujauzito wa mke wake.
Amesema Meghan na mtoto wako katika ''hali nzuri'' na kwamba jina la mtoto halijatolewa.
"Bado tunafikiaria jina tutakalompatia," Mwanamfalme Harry aliwaambia wanahabari.
"Nadhani tutakuwa na tumepata jina katika kipindi cha siku mbili - kama ilivyopangwa - na kama familia tutawafahamisha jina lake na kila mtu amuone mtoto."
Aliipoulizwa jinsi alivyojihisi kushushuhudia mtoto wake akizaliwa , alicheka na kusema:
"Sijawahi kushuhudia mtu akijifungua. Hii ilikuwa mara yangu ya kwanza na na kwa kweli siwezi kuelezea najivunia mke wangu''.

Chanzo cha picha, AFP

Matoto wao amepata moja kwa moja urai wa Marekani kupitia mamake Meghan, ambaye ni mzaliwa wa taifa hilo.
Akizungumza na na gazeti la Speaking to the Sun, baba yake Meghan, Thomas Markle, aliwapongeza wazazi hao wapya na kuelezea furaha yake kwa kuzaliwa mwana mfalme.
"Najivunnia kuwa mjukuu wangu amezaliwa katika familia ya ufalme wa Uingereza, naamini atakuwa mkubwa na ataweza kuwahudumia watu wa Uingereza kwa taadhima kuu," alisema hivyo kutoka nyumbani kwake nchini Mexico.
Charles Spencer - Ndugu wa Diana, na mjomba wa Harry - alituma risala zake za pongezi kwa kupitia mtandao wake wa Twitter.
Aliandika: "Hii ni ni habari njema sana siku ya leo - pokeeni pongezi tele kutoka kwangu!"
Wiki kadhaa zilizopita Buckingham Palace ilikua imetangaza kwamba haitatoa taarifa zozote kuhusu kuzaliwa kwa mwana mfalme zaidi ya kufahamisha tu kwamba mtoto atazaliwa.

Baada ya kupokea taarifa za kuzaliwa kwa mwana mfalme, Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May aliandika katika mtandao wake wa Twitter: "Pongezi nawatakia kila la heri na maisha ya furaha ya uzazi."
Kiongozi wa chama cha Labour Jeremy Corbyn, waziri wa kwanza wa Uskochi Nicola Sturgeon pia wametuma pongezi zao kwa Mwanamfalme Harry na mkewe.
Askofu mku wa Canterbury Justin Welby, ambaye aliwafungisha ndoa wapenzi hao mwezi Mei mwaka jana, amesema: "Nawaombea maisha ya baraka, amani, afya na furaha tele."

Uhusiano wa Harry na Meghan

Chanzo cha picha, Reuters
8 Novemba 2016 - Kensington Palace ilitoa taarifa kuthibitisha kuwa Prince Harry amekuwa katika uhusiano wa kimapenzi na Meghan Markle "kwa miezi kadhaa" na kuomba vyombo vya habari kuheshimu faragha yao.
28 Novemba 2017 - Harry na Meghan walitangaza kuwa wamechumbiana na kwamba watafunga ndoa.
15 December 2017 - Kensington Palace ilithibitisha kuwa wapenzi hao wamechagua kunfunga ndoa yao Winsor Castle May 19 makauliofuata.
19 May 2018 - Harry na Meghan walioana mbele ya wageni 600 katika kanisa la St George na kupewa cheo cha Mtawala wa Sussex naye Bi Markle akapewa wadhifa wa Mke wa Mtawala wa Sussex.
15 October 2018 - Kensington Palace ilitangaza kuwa Mke wa Mtawala wa Sussex atajifungua msimu wa machipuko 2019
6 May 2019 - Meghan ajifungua amtoto wa kiume, ambaye atakuwa wa saba katika orodha ya watawala wa ufalme wa Ungereza.













