Prince Harry atembea katika ardhi ya mabomu yaliyofukiwa ardhini Angola

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika sehemu ya ziara yake kusini mwa Afrika, Mwana mfalme Harry ametembelea nchini Angola ili kuendeleza jitihada za kuondoa mabomu yaliyo ardhini.
Mwana mfalme huyo ameamua kufuata nyayo za mama yake, Princess Diana ambaye mwaka 1997 alitembelea maeneo hayohayo na kutaka kuondoa mabomu yaliochimbwa ardhini.
Picha za ziara yake zilipendwa na wengi duniani kote.
Eneo hilo hatari bado linaendelea kumaliza maisha ya watu wengi katika nchi nyingi.
Je, sehemu hizo ziko katika maeneo gani duniani na hatua gani zimechukuliwa?
Jinsi Prince Harry anavyofuata nyayo za mama yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Princess Diana alijulikana sana kwa kujitolea kwa wahitaji ingawa mafanikio yake hakuyaweka hadharani.
Kwa mfano Diana alifungua kliniki ya kwanza Uingereza kwa ajili ya waathirika wa virusi vya ukimwi mwaka 1987, na kuweza kufanikiwa kubadili tabia za waathirika
Kuhamasisha uwelewa juu ya mabomu yaliyochimbwa ardhini, ni miongoni mwa kosa kubwa lililosababisha apewe talaka na mume wake Prince Wales mwaka 1996.
Kwa miongo kadhaa mabomu ya ardhini yalikuwa yamaetumika katika migogoro mingi.
Mabomu mengi ambayo hayajalipuka yaliachwa wakati wa vita, kipindi ambacho mauaji ya watu yalifanyika kwa wingi au yalilipuka bila kutarajiwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Picha inaonyesha namna wakazi wa Angola walivyoathirika na vilipuzi hivyo.
Wakati wa ziara yake Prince Harry ameelezea mabomu hayo yaliyochimbiwa ardhini ni kovu la vita lisilopona .
Vilipuzo hivyo vimesababisha mauaji ya watu wa ngapi na wangapi wameumia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabomu hayo ambayo yaliyofukiwa ardhini huwa yanalipuka kwa makubaliano fulani au bila kulipuka bila kutarajiwa.
Kuna aina mbili ya mabomu: Mabomu yaliyofukiwa yakiwa yanalenga kujeruhi watu au kuwauwa na aina ya pili ya mabomu yametengenezwa kwa ajili ya kuteketeza magari.
Vilipuzi hivyo vilitumika katika vita ya kwanza ya dunia, lakini yalianza kulipuka kuanzia mwaka 1960 na kuendelea.
Kuchimbia mabomu ardhini ilikuwa miongoni mwa mbinu za kivita zilizotumika, na kusababisha madhara katika maisha ya wengi.
Nchi kama 60 bado zinakabiliwa na changamoto za mabomu hayo yaliyofukiwa ardhini.
Utafiti umebaini kuwa watu zaidi ya 120,000 waliuwawa au kujeruiwa na mabomu hayo ya ardhini kati ya mwaka 1999-2017.
Karibu nusu ya waathirika ni watoto, asilimia 84 ni watoto wa kiume.
Nchi zipi zina mabomu yaliyofukiwa ardhini?
Maelfu ya mabomu hayo yaliyofukiwa ardhini yapo duniani kote.
Angola ikiwa ni miongoni mwa taifa lililoathirika zaidi duniani kwa sababu ya vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1975 mpaka 2002.
Asasi ya kusaidia wahitaji ya Halo inasema kuwa sio rahisi kujua ni mabomu mangapi yamefukiwa katika nchi hiyo lakini ni zaidi ya 100,000 yamelipuka tangu mwaka 1994.
Mamlaka ya uchibaji madini nchini Angola imesema kuwa mabomu hayo yalikuwa kama 1200.
Kuondoa migodi ni gharama na kazi ya hatari.Kwa sasa , inaweza kuchukua miaka mia moja kukabiliana na hali hiyo duniani kote.
Maeneo mengine ambayo yana vilipuzi vilivyofukiwa kwa wingi ni Chad, Afghanistan, Cambodia, Thailand, Azerbaijan, Bosnia-Herzegovina, Croatia, Uturuki, Iraq, Yemen na magharibi mwa jangwa la Sahara.
Jitihada gani zimefanyika kukabiliana na changamoto hiyo?
Princess Diana alitaka duniani kote kupiga marufuku watu kufanya uchimbaji wa madini katika maeneo ambayo yalifukiwa mabomu.
Mwaka 1997, miezi mitatu tu baada ya kifo chake, nchi 122 zilisaini mkataba wa Ottawa, ambao ulikataza kutumiwa wa maeneo ambayo yalikuwa yamefukiwa mabomu.
Nchi hizo zilipewa jukumu za kutokomeza mabomu yote yaliyofukizwa ardhini kwa kipindi cha miaka 10 na miaka minne ya kuteteteza.
Sasa ni nchi zaidi ya 164 ambazo zimesaini mkataba huo, Uingereza ikiwa miongoni mwa nchi hizo.
Ingawa Marekani, China, India na Urusi - ni miongoni mwa nchi 32 ambazo hazikusaini makubaliano hayo.
Mataifa mengi hayakufikia makubaliano hayo kwa wakati na mengine bado yanafukia mabomu ardhini.
Mabomu hayo ya ardhini yameripotiwa Myanmar ambayo haikusaini makubaliano hayo.
Vilevile makundi mengine ya wanamgambo yasiyokuwa ya serikali kama Boko Haram wamekuwa wakiyatumia kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu mwaka 2014.













