Wataalamu wanasema uraibu huanzia kwenye maumivu

Gabor Mate
Maelezo ya picha, Dokta Mate, mtaalamu wa masuala ya uraibu

Unafikiri nini kuhusu uraibu?

Daktari nchini Canada Gabor Mate anaamini kuwa tunapaswa kufikiri upya kuhusu namna tunavyoshughulikia waraibu.

Kwanza kabisa anaamini kuwa uraibu huanzia kwenye maumivu'' anasema.

Hizi ni njia tano ambazo dokta Mate anaamini hatulielewi tatizo.

'Hatutibu mzizi wa tatizo'

Ubongo
Maelezo ya picha, Ubongo wa mwanadamu

Ikiwa unataka kutazama sababu za uraibu, unapaswa kuangalia faida za uraibu: uraibu ulikufanyia nini?

Watu wanasema , ''ulinipunguzia maumivu, uliniondolea msongo wa mawazo, ulinifanya nijihisi kuwa hai.

Kwa maneno mengine uraibu hukidhi mahitaji muhimu ya binaadamu ambayo vinginevyo visingekuwa msaada kwenye maisha ya mtu.

Haya yote hutokana na kutokuwepo kwa mawasiliano, kutengwa au kuwa na msongo wa mawazo katika maisha-haya yote ni maumivu ya hisia.

Kwa hiyo swali si kuwa ''kwa nini umekuwa na uraibu?'' swali ni je ''kwa nini unapata maumivu?''

Ukitazama idadi ya watu wenye uraibu, unachogundua ni kuwa wengi walioyapitia utotoni kwa kiasi kikubwa yakaababisha uraibu.

Hivyo uraibu mara zote huanzia kwenye maumivu na magumu ya wakati wa utotoni-hatua ambayo haimaanishi kula mtu anayeteseka atakuwa na uraibu, lakini ina maana kuwa kila mraibu alipitia mateso.

Lakini hilo halitokei sana katika ulimwengu huu,

Uraibu si chaguo la mtu

Hakuna anayependa kuwa kwenye maumivu
Maelezo ya picha, Hakuna anayependa kuwa kwenye maumivu

Imani potofu nyingine kuhusu uraibu ni imani kuwa mtu huchagua kuwa mraibu.

Hakuna mtu anayeamka asubuhi na kusema: ''matamanio yangu nikuwa mraibu.''

Kuwa na uraibu si uchaguzi ambao mtu hufanya, ni matokeo ya maumivu ya hisia.

Na hakuna anayechagua kuwa na maumivu hayo.

Uraibu si tatizo la kijenetiki

chupa
Maelezo ya picha, Chupa

Moja kati ya imani potofu kuhusu uraibu ni kuwa uraibu ni tatizo la kijenetiki.

Ni kweli huwa ndani ya familia. Lakini kwa nini liwe tatizo ndani ya familia?

Kama nikiwa mlevi na mtu wa kuwafokea watoto wangu na wakakua nao wakawa walevi, je wameipata tabia hii kwa njia ya kijenetiki?

Au ni tabia ambayo wamekuwa nayo kwa sababu mimi niliwatengenezea mazingira hayohayo ambayo nilikua nayo?

Hivyo basi tatizo kuwa ndani ya familia hakina uhusiano wowote na sababu za kijenetiki.

Uraibu ni tabia iliyoenea

Imani nyingine kuhusu uraibu ni kuwa ni tabia ya watu wasiofaa kwenye jamii yetu.

Nikitazama kwenye jamii hii katika nyanja zote kuna

Unaweza kuwa mraibu wa chochote hata muziki

Santuri za muziki
Maelezo ya picha, "Siku moja nilitumia dola za marekani 8,000 kwa ajili ya santuri za muziki '' dokta Mate amekiri

Kwa maoni yangu, uraibu huwa kwenye tabia yoyote ambayo mtu hupata furaha ya muda mfupi au nafuu , hivyo huwa katika hali ya kutamani kitu hicho, lakini hupata madhara hasi mwisho wa yote na hawawezi kuachana na uraibu huo pamoja na kuwa huwa na madhara.

Inaweza kuwa dawa, tumbaku, kilevi chochote.

Inaweza kuwa ngono, kamari, ununuzi , kufanya kazi, masuala ya siasa, michezo ya mtandaoni, shughuli yoyote inaweza kuwa uraibu, inategemea mahusiano na shughuli yenyewe, iwapo inakupa unafuu, lakini chenye madhara mabaya na kigumu kukiacha-basi una uraibu.

Dokta Mate anasema alikuwa na uraibu mkubwa na mambo mawili, kwanza kazi hata ikamfanya apuuze mahitaji yake na familia yake, ili kuleta ufanisi kazini.

''Uraibu wa kazi ulianzia kutokana na hisia kuwa sikuwa mfanyakazi mzuri, na hivyo nilijitahidi kufanya kazi kuthibiisha kuwa ni mfanyakazi mzuri na pia nilikuwa nafikiri sipendwi.

Pia alikuwa na uraibu wa manunuzi, alinunua santuri za muziki wa classic zenye thamani ya dola 8,000 kwa siku moja.

Si kuwa hakuwa na uraibu na muziki, ndio alipenda muziki lakini uraibu ulikuwa kwenye manunuzi.

Unaweza kufikiri ni kichekesho- utawezaje kufananisha uraibu wako na wale waraibu wa heroin?

''Lakini wagonjwa wangu wa uraibu nilipowaambia kuhusu uraibu wangu, hawakucheka, walitikisa vichwa wakisema. ''ndio daktari hauna tofauti na sisi.

Presentational grey line