Uraibu wa Kamari: Namna gani unaweza kupambana na uraibu wa kamari

Gambling addict
Maelezo ya picha, Kimberley Wadsworth alianza kucheza kamari mwaka 2015

Mama mmoja nchini Uingereza alipoteza mtoto wake kwa sababu ya kamari mara baada mtoto huyo kucheza kamari ya kiasi cha fedha cha paundi 36,000 ambayo ni sawa na dola 45,000 .

Kimberley Wadsworth aliamua kujiua mara baada ya kumaliza fedha zote katika mchezo wa kamari.

Binti huyo alimuomba mama yake fedha za kulipa madeni yake katika mchezo huo lakini mwisho wa siku fedha zote alizichezea tena kamari na kumuacha mama yake bila sehemu ya kuishi.

Slot machines in a uk pub

Chanzo cha picha, Getty Images

Kimberley ambaye alikuwa na umri wa miaka 32,alianza kucheza kamari katika sehemu za starehe na kwenye mitandao mnamo mwaka 2015.

Alianza kupata uraibu wa kamari baada ya kupata sonona mara baada ya kifo cha baba yake na kuwa na ndoa isiyokuwa na furaha.

Mtoto huyo alijaribu kumficha mama yake juu ya hali yake ya sonona.

Binti huyo alitumia zaidi ya paundi 44,000 katika kamari pamoja na paundi 17,000 kutoka katika urithi wa bibi yake .

Bi Wadsworth, mwenye umri wa miaka 65, ambaye ndiyo mama yake alidai kuwa ilimbidi auze nyumba ya familia ili ampe fedha ya kulipa madeni ya kamari ingawa hakuyalipa mpaka alipojiua.

"Hakulipa deni hata moja bali aliendelea kucheza kwa muda wa wiki mbili mfululizo hivyo nikabaki bila mahali pa kuishi" alieleza bi.Wadsworth .

Kay Wadsworth
Maelezo ya picha, Mtoto wa Kay Wadsworth's alicheza kamali kwa paundi 36,000

Mama huyo anasema kwamba alijaribu kumtafutia mtaalamu wa afya ya akili ili aweze kupata msaada wa tatizo la uraibu wa kucheza kamari lakini hakwenda.

Badala yake aliandika ujumbe " tumechelewa sana mama" kabla hajajiua.

Bi.Wadsworth alisema kuwa kama msaada ungetolewa mapema zaidi basi mtoto wake angekuwa hai bado.

Presentational grey line
A gambler playing on a machine

Chanzo cha picha, PA

"Kuna wataalamu ambao wanajua namna ya kukabiliana na watu ambao wana uraibu wa kucheza kamari na wanajua dalili za mtu ambaye ameanza kupata tatizo hilo".

"Wataalamu wanajua dalili za watu wenye uraibu wa kamari lakini wanaficha , Wanaendelea kutudanganya kuwa si rahisi kuacha," Wadsworth alisema.

Kuna watu ambao wanapata uraibu kwa kiwango kikubwa sana mpaka kuhatarisha maisha yao kwa kujiua.

Watu wapatao 340,000 nchini Uingereza wana tatizo kubwa la uraibu wa kamari kwa muhimu wa tume ya mchezo wa kamari.

Vituo kadhaa vya afya vimeanzishwa nchini humo ili kuwasaidia watu walioathirika na tatizo la kamari."

Presentational grey line

Uraibu wa kucheza kamari huwa unaongezeka kadri mtu anapozidi kupata fedha nyingi.

Kijana mmoja kwa jina la Chris Murphy,alianza kupata uraibu alipopata paundi 350 akiwa na umri wa miaka 17.

Tangu wakati huo mpaka alipofika miaka 23, ametumia zaidi ya paundi 100,000 katika kamari

Kijana mwenye miaka miaka 33 na ameweza kujizuia kucheza kamari kwa miezi nane.

Ukiangalia upande wa matatizo ya kiafya, hali yake sio nzuri na anahitaji msaada.

Kwa mujibu wa mtaalamu wa afya anasema kwamba, Jambo la muhimu ni kumtaka yeye mwenyewe kupambana kuacha kucheza mchezo huo wa kamari ambao anadhani kuwa hawezi kuacha.

Inawezekana kuacha kucheza kamari ni jambo gumu zaidi ya mtu kuamua kuacha madawa ya kulevya au pombe.

Hakuna ubaya kwa mtu kukubali kuwa anahitaji msaada.

Online gambling

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni muhimu watu wanaoanza kupata tatizo hili kutafuta msaada mapema kwa sababu madhara au matokeo yake huwa sio mazuri.

Kamari inaweza kumfanya mtu afilisike, kupoteza uhusiano mzuri na wapendwa wake, kupoteza ajira na kupata msongo wa mawazo.

Presentational grey line