Amchumbia mpenzi wake katika picha za siri kwa mwezi mzima

Chanzo cha picha, Edi Okoro
Mwanamume mmoja amepiga picha za siri za mpenzi wake na pete ya uchumba katika msururu wa kinachoonekana kuwa ni kumchumbia kwa siri kwa muda wa mwezi mmoja mpenzi wake huyo pasi yeye kujua.
Edi Okoro, mwenye umri wa miaka 30, kutoka huko Hertfordshire, aliichomoza pete ya uchumba katika picha alizopiga na mchumba wake Cally Read, ambaye mara nyingi akiwa ameipa kamera mgongo.
Walipigwa picha pamoja pia katika duka moja wakati akitazama kwenye darubini na wakati mwingine Okoro alifanikiwa pia kuiweka pete hiyo mkononi mwake pasi Cally kujua.
Wakati hatimaye alimuomba mpenzi wake huyo amuoe, Cally alijibu "ndio".

Chanzo cha picha, Edi Okoro
Okoro amesema ilikuwa "changamoto" kutafuta mbinu ya kumchumbia Bi Read, mwenye umri wa miaka 28.
"Baadhi hupanga mialiko ya kushtukiza , mtoko wa jioni kupata chakula katika hoteli za kifahari , au hata kuweka kibao chenye ujumbe nioe," aliandika katika ujumbe wake kwenye Facebook.
"Sikuweza kufanya hivi kwasababu 'Edi hapangi'... mimi ni mtu wa papo kwa hapo."

Chanzo cha picha, Edi Okoro

Chanzo cha picha, Edi Okoro
Alisema pia huenda mpenzi wake angesusia iwapo angefanya mipango ya kumchumbia katika likizo au mtoko wa pamoja kwenda kupata chakula.
"Fikra ilikuwa ni kupiga picha nyingi iwezekanavyo, katika mandhari tofauti, mpaka nitakapo pata sehemu nzuri ya kumuomba anioe, au mpaka anishtukie, ambapo kwa wakati huo ingebidi niwasilishe ombi langu," aliandika.
Picha hizo ikiwa ni pamoja na baadhi alizompiga Cally akiwa kitandani anatuma ujumbe mfupi wa simu, na pia kuiacha pete kwenye sahani pamoja na pete nyingine na mikufu yake Cally kwa siku mbili.

Chanzo cha picha, Edi Okoro
Ujumbe wa Okoro umesambazwa mara 56,000 kwenye Facebook na video yake akiwa anaishikilia pete hiyo huku akicheka na Cally akiwa anapiga mswaki imetazamwa mara milioni moja na nusu.
Baadaye alituma picha akiwa pamoja na mchumba wake aliyeonekana kuivaa pete hiyo, lakini hajafichua hatimaye alivyomuomba kumuoa Bi Read.

Chanzo cha picha, Edi Okoro













