Mchezaji wa Real Madrid Sergei Ramos amuoa Pilar Rubio

Harusi ya Sergio na Rubio iligubikwa na soka kwani nyota wengi wa soka walihudhuria

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Harusi ya Sergio na Rubio iligubikwa na soka kwani nyota wengi wa soka walihudhuria

Umati wa watu ulikusanyika katika kanisa kuu la Seville nchini Uhispania Jumamosi 15, Juni 2019, kushuhudia sherehe ya harusi ya mchezaji soka wa Real Madrid -Sergio Ramos aliyekuwa akifunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Pilar Rubio, ambaye ni mtangaza Televisheni.

Sergio mwenye umri wa miaka 33-alikuwa nadhifu huku akiwa amevalia suti ya vipande vitatu nyeusi(three piece) iliyokuwa imeshonwa kwa mtindo wa aina yake pamoja na tai ya rangi ya kijivu iliyotulia huku bibi harusi mwenye umri wa miaka 41- akionekana kwa gauni lenye mvuto lililoiacha shingo na na mabega yake wazi kiasi cha haja.

Marco Asensio na mkewe Sandra Garal waling'ara kwa ajili ya harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marco Asensio na mkewe Sandra Garal waling'ara kwa ajili ya harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio

Gauni lake refu lililogusa sakafu lililikuwa limerembeshwa kwa shanga na juu alikamilisha urembo wake kwa shela iliyowekwa nakshi.

Aliamua kusuka nywele zake na akaweka kibanio kikubwa cheusi, mtindo ambao ni wa kipekee ambao haujashuhudiwa katika harusi za watu maarufu.

Pilar Rubio na baba yake Manuel Rubio wakati wa harusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pilar Rubio na baba yake Manuel Rubio wakati wa harusi

Mrembo Rubio aliamua kuvalia heleni ndeefu zilizobuniwa na kampuni ya vipuli na mavazi ya bracelet na kidole chake cha kati kikapambwa na pete ya almasi.

Baada ya ibada ya harusi kanisani, wageni waalikwa 500 walikaribishwa kwa hafla kubwa kwenye makazi ya bwanaharusi yanayoitwa "Happiness of SR4" yaliyopo eneo la Seville.

Sergio Ramos na mama yake Paqui García wakati wa sherehe ya harusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sergio Ramos na mama yake Paqui García wakati wa sherehe ya harusi

Na kwa mujibu wa gazeti la Uingereza Daily Mail, wageni waliruhusiwa kuingia katika baada ya kuacha simu zao na vifaa vingine kama kamera au vinasa sauti.

Harusi iligubikwa na soka kwani nyota wengi wa soka walihudhuria kama vile mchezaji wa zamani wa Real Madrid David Beckham na mkewe Victoria Beckham, nyota wa sasa na wa zamani wa La Liga Jordi Alba, Luka Modric, Keylor Navas, Roberto Carlos na Alvaro Morata, pamoja na matador El Cordobes na wengine wengi.

David Beckam na Mkewe Victoria Beckam katika sherehe ya harusi ya Sergio Ramos na mkewe Pilaar Rubio walipokuwa wakielekeakatika kanisa la Seville ,Uhispania

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, David Beckam na Mkewe Victoria Beckam katika sherehe ya harusi ya Sergio Ramos na mkewe Pilaar Rubio walipokuwa wakielekeakatika kanisa la Seville ,Uhispania

Hata hivyo Cristiano Ronaldo hakuhudhuria kwani hakualikwa kwasababu ya kile kilichoripotiwa kuwa wawili hao walikosana wakati Ronaldo alipoondoka Real Madrid msimu uliopita kujiunga na Juventus kwa mkataba wa pauni milioni 100 .

Christiano Ronaldo hakualikwa kutokana na ripoti kuwa alikosana na Sergio alipohamia Juventus

Chanzo cha picha, Getty Images/AFP

Maelezo ya picha, Christiano Ronaldo hakualikwa kutokana na ripoti kuwa alikosana na Sergio alipohamia Juventus

Pia , Gerard Pique na Shakira hawakuhudhuria harusi ya Sergio kwa sababu ambazo hazikujulikana, licha ya kwamba alialikwa.

Bwana harusi aliamua kumzawadia bibiharusi onyesho la muziki wa bendi maarufu ya Australia AC/DC, inayopiga muziki wa ambayo alifahamu fika mkewe anaipenda sana.

Wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012 na wanawatoto watatu wanaoitwa Sergio, Marco na Alejandro.

Segio na Rubio wamekuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012 na wanawatoto watatu wanaoitwa Sergio, Marco na Alejandro

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Segio na Rubio wamekuwa wakiishi pamoja tangu mwaka 2012 na wanawatoto watatu wanaoitwa Sergio, Marco na Alejandro

Katika mahojiano aliyoyafanya wakati wa harusi yake, Ramos alifichua kuwa siku yao ya harusi ilikuwa ni ya kipekee si kwao tu bali pia kwa watoto wao.

Nahodha huyo wa Real Madrid alinukuliwa akisema , "Ni wakati wa kipekee sana kwetu baada ya kuwa pamoja kwa muda mrefu na kuunda familia nzuri sana yenye watoto wadogo watatu ambao wanayajaza maisha yetu furaha na malengo''. Aliongeza," Tulihisi kuwa ulikuwa ni muda unaofaa na tulitaka watoto wetu waifurahie kwasababu walikuwa ni wadogo sio kitu ambacho wangekielewa sana ."

Kiungo wa kati wa zamani wa Aarsenal Santi Carzola na mkewe Ursula walitinga kwa mavazi haya katika harusi ya Sergio na Rubia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kiungo wa kati wa zamani wa Aarsenal Santi Carzola na mkewe Ursula walitinga kwa mavazi haya katika harusi ya Sergio na Rubia

Baadhi ya wageni waliohudhuria harusi:

Mlindalango wa Real Madrid Keylor Navas na mke wake Andrea Salas pia hawakukosa kwenye harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mlindalango wa Real Madrid Keylor Navas na mke wake Andrea Salas waliamua kuvalia rangi hizi kwenye harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio
Luka Modric wa Real Madrid na mkewe Vanja Bosnic walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika harusi ya Sergio na Rubio

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Luka Modric wa Real Madrid na mkewe Vanja Bosnic walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika harusi ya Sergio na Rubio
Marco Asensio na mkewe Sandra Garal waling'ara kwa ajili ya harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marco Asensio na mkewe Sandra Garal waling'ara kwa ajili ya harusi ya Sergio Ramos na Bi Pilar Rubio