Harusi ya Kifalme ya Prince Harry na Meghan Markle: Mwanamfalme Harry na Meghan wafunganishwa katika ndoa Windsor Castle

Chanzo cha picha, PA
Bi Meghan Markle na Mwanamfalme Harry wamevishana pete na kutangazwa kuwa mume na mke Windsor Castle katika sherehe inayofuatiliwa na mamilioni ya watu kupitia runinga, mtandao na redio.
Wawili hao walifunganishwa katika ndoa mbele ya Malkia na wageni 600 waliokuwemo ndani ya kanisa la St George, katika Windsor Castle.
Bi Markle alikuwa amevalia vazi la harusi lililoshonwa na fundi mbunifu wa mitindo Mwingereza Clare Waight Keller.
Bi Meghan alitumia gari aina ya Rolls Royce Phantom kufika kanisani ambapo alipokelewa kwa shangwe na nderemo aliposhuka kutoka kwenye gari hilo na kuingia kanisa la St George.
Miongoni mwa wageni waliofika ni nyota wa televisheni Marekani Oprah Winfrey na mwigizaji Idris Elba.
George na Amal Clooney, David na Victoria Beckham pamoja na Elton John pia wamewasili.
Mwanamfalme Harry na Meghan Markle baadaye walipitia kwenye mji wa Windsor kwa msafara kwa kutumia kigari maalum cha kuvutwa na farasi.
Mwanamfalme Harry amepewa cheo cha Mtawala wa Sussex na bibi yake Malkia Elizabeth II, naye Bi Markle sasa atakuwa Mke wa Mtawala wa Sussex.
Mwanamfalme Harry, ambaye ni wa sita kwenye orodha ya warithi wa ufalme, pia amepokezwa vyeo vya Earl wa Dumbarton na Baron Kilkeel.


Chanzo cha picha, PA

Chanzo cha picha, PA

Chanzo cha picha, Getty Images


Maelfu ya watu wamefika Windsor kufuatilia harusi hiyo, wengi walikesha kuhakikisha wanapata nafasi nzuri ya kujionea yaliyokuwa yanajiri.

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, PA
Mwanamfalme Charles, babake Mwanamfalme Harry, ndiye aliyeyemsindikiza Bi Markel kwenda kwenye madhabahu baada ya babake Thomas kushindwa kuhudhuria harusi hiyo kutokana na sababu za kiafya.
Mkesha wa harusi, Mwanamfalme Harry, 33, aliambia umati wa watu Windsor kwamba anajihisi "mtulivu" na kwamba Bi Markle, 36, anajihisi "vyema sana".
Katika kiapo chake cha ndoa, Bi Markle hakuahidi "kumtii" mume wake. Mwanamfalme Harry ameamua kuwa na pete ya ndoa.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, PA
Wageni 600 walifuatilia harusi hiyo, ambayo iliongozwa na Askofu Mkuu wa Canterbury, Justin Welby, katika kanisa la St George.

Chanzo cha picha, PA

Chanzo cha picha, PA


Chanzo cha picha, PA

Chanzo cha picha, PA
Umati wa watu wakiungana na waandishi wa habari kutoka maeneo mengi duniani wamlikusanyika Windsor kwa sherehe hii kubwa.
Inakadiriwa kwamba watu hadi 100,000 walikuwa kwenye barabara za mji huo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe


Watu wa kawaida 1,200, wengi ambao wametambuliwa kwa juhudi zao za hisani katika jamii, walialikwa kuhudhuria harusi hiyo Windsor Castle.

Chanzo cha picha, Reuters
Bi Markle alikuwa na mabinti 10 wapamba harusi na wavulana, wote wa chini ya miaka minane, wakiwemo Mwanamfalme George na Bintimfalme Charlotte.
Bi harusi alilakiwa na Mwanamfalme Charles, ambaye alimtembeza hadi kwenye madhabahu.
Wakati wa ibada, wawili hao walikula kiapo kila mmoja akijitoa kwa mwenzake na kusema: "kwa mema, kwa mabaya, kwa ujatajiri, kwa umaskini, kwa ugonjwa na kwa afya, kukupenda na kukuenzi, tangu kifo kitutenganishe."

Chanzo cha picha, Reuters

Chanzo cha picha, PA















