Wanaakiolojia waugundua mskiti wa miaka 1,200 chini ya ardhi jangwani Israel

An ancient mosque found in the Israeli desert

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mskiti huo uligunduliwa katika mji wa Bedouin Israeli - Rahat katika jangwa la Negev

Mojawapo ya misikiti ya kwanza iliyotambulika duniani, uliojengwa takriban miaka 1,200 iliyopita, umegunduliwa na wanaakiolojia katika jangwa la Negev nchini Israel.

Masalio hayo, ya kutoka karne ya 7 au ya 8 yaligunduliwa katika mji wa Bedouin - Rahat.

Mamlaka inayosimamia vitu vya kale Israel (IAA) inasema msikiti huo uligunduliwa chini ya ardhi wakati wa ujenzi katika enoe hilo.

The ruins of a mosque found in Israel

Chanzo cha picha, Israel's Antiquities Authority

Maelezo ya picha, Mskiti uligunduliwa wakati wa ujenzi
Muslims pray at the site of an ancient mosque in Israel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waislamu wanaswali katika enoe hilo kulikogunduliwa masalio ya mskiti

Ni mskiti wa kwanza unaotambulika katika eneo hilo kutoka wakati huo, ukishindana kwa umri na yale yaliogunduliwa Makka na Jerusalem, IAA limesema.

Watafiti Jon Seligman na Shahar Zur wanasema mskiti, wa kutoka karne ya 7 au 8 ni jambo adimu kuligundua kokote.

Watafiti wanaamini huenda wakulima wa eneo hilo ndio waliokuwa waumini waliosali katika msikiti huo.

A worker from Israel's Antiquities Authority at the site of an ancient mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Shahar Tzur wa mamlaka ya vitu vya kale Israel atoa maelezo ya walichokigundua

Jengo hilo lilikuwa la wazi, lenye umbo la mstatili na lilikuwa na "Mihrab" - au upembe anaosimama muongoza sala linaloelekea mji mtukufu wa Makka au Qibla.

"Huu ni ushahidi wa lengo la jengo hili na lilivyotumika miaka mia kadhaa iliyopita," amesema Seligman.

A worker from Israel's Antiquities Authority at the site of an ancient mosque

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Yaser Alamor anaonyesha jiwe lililogunduliwa katika msikiti huo

Ni mojawapo ya misikiti ya kwanza baada yakuwasili kwa Uislamu katika inayojulikana hii leo kama Israel wakati waraabu walipolitawala jimbo la Byzantine mnamo mwaka 636, kwa mujibu wa Gideon Avni, mtaalamu wa historia ya kale ya uislamu.

"Ugunduzi wa kijiji na msikiti katika eneo hilo ni mchango muhimu katika uchunguzi wa historia ya nchi hiyo wakati wa kipindi hicho kigumu," amesema.

Getty na Mamlaka ya vitu vya kale Israeli, zinamiliki haki zote miliki za picha hizi.