Makaburi ya jadi Misri na vitu vya kushangaza vilivyogunduliwa ndani

Baada ya wataalamu kugundua mumiani wa paka na wadudu katika makaburi karibu na Cairo, Hivi ni vitu vingine vya ajabu vilivyozikwa katika miaka ya nyuma Misri.

mummified cats

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua mkusanyiko wa mumiani wa paka wanaodhaniwa kuwa na umri wa miaka 4000. Paka walikuwa na umuhimu mkubwa katika utamaduni wa jadi Misri.
Ancient Egyptian art and mirror
Maelezo ya picha, Kioo ukutani: Wamisri wa jadi walikuwa wakiweka mapambo katika makaburi yao, yaliotumika na wanaume na wanawake, matajiri kwa maskini. Mojawapo mashuhuri ulikuwa wanja wa machoni ambao ulikuwa pambo kuu wakati huo.
King Tutankhamun tomb

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mnamo 1922 kaburi la Tutankhamun lilifunguliwa. Alifahamika pia kama mfalme Tut kifupi, lilikuwa kaburi la kwanza kugunduliwa likiwa karibu kamili. Lilikuwa na vitu takriban 5,398 vikiwemo viti viwili vya ufalme, mabehewa sita yalioendeshwa kwa farasi, barakoa za dhahabu, fuko la vipodozi, manukato na jeneza lililokuwa na mumiani. Kulikuwa na zaidi ya vikapu 100 vya ngano, tende,na matunda, na majagi ya mvinyo.
A restored boat that was one of a pair buried in pits next to Pharaoh Khufu final resting place

Chanzo cha picha, Shutterstock

Maelezo ya picha, Unadhani mfalme Tut alikuwa na utajiri wa kupita kiasi? Firauni Khufu alizikwa na boti. Kaburi lake lilipofukuliwa karibu na mnara mkubwa Giza, wanaakiolojia walifukuwa zaidi ya vipande 1200 vya boti kubwa karibu na eneo hilo. Leo wamevikusanya na kuinda meli ambayo inaonekana Misri yenye urefu wa futi 144.
Ancient Egyptian board game

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zamani Misri watu walikuwa wakipenda kucheza michezo ya bao na ilibebwa hadi katika maisha yao ya baadaye. Mojawapo maarufu uliitwa senet, inayofasiriwa kama "kupita."
Ancient Egyptian organ jars

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuishi maisha ya baada ya kifo, ni lazima marehemu wazikwe na sehemu zao za mwili, lakini sehemu za ndani ya mwili zilitolewa wakati wa kugeuzwa mumiani, alafu sehemu hizo (maini, utumbo, na mapafu) zilihifadhiwa ndani ya majagi kama haya.
Ancient Egyptian servant statues

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kila Firauni mzuri alihitaji watumwa katika maisha ya baadaye, lakini badala ya kumzika mtumwa aliye hai ndani ya kaburi, walitengeneza sanamu wadogo walioitwa ushabti. Ilidhaniwa Ushabti wangefufuka kuwatumikia wafalme wao katika maisha ya baadaye.