Misri yagundua makaburi ya kale yenye miili huko Luxor

Chanzo cha picha, EPA
Wana akiolojia nchini Misri wameonyesha vitu kadhaa ukiwemo mwili wa binadamu uliohifadhiwa kutoka kwa moja ya makaburi ambayo hayakuwa yamekaguliwa kwenye mji wa kale wa Luxor
Mwili huo wa binadamu unaaminiwa kuwa ule wa afisa kutoka ufalme wa Misri wa miaka 3,500 iliyopita.
Makaburi hayo yako eneo la Draa Abul Naga necropolis, eneo ambalo ni maarufu kwa mahekalu yake na makaburi.
Eneo hilo liko karibu na bonde la wafalme ambapo wengi wa Pharao wa Misri walizikwa.
Wizara inayohusika mambo ya kale nchini Misi ilisema kuwa makaburi hayo yalikuwa yamegunduliwa na mwanaakiolojia wa Ujerumani miaka ya tisini lakini ilibaki imefungwa hadi hivi karibuni.

Chanzo cha picha, AFP

Chanzo cha picha, EPA








