Peru: Daraja la kamba iliyotengenezwa kwa nyasi

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Kila mwaka mabaki ya mwisho ya daraja la kamba la Inca hubadilishwa na nyingine mpya kuwekwa katika mto Apurimac uliopo katika eneo la Cusco nchini Peru.
Daraja la Q'eswachaka ambalo linatengenezwa kwa kamba inayotengenezwa kwa mikono limetumika kwa karibu miaka 600.
Daraja hilo ambalo linaunganisha miji muhimu ya Peru na ufalme wa Inca, lilitangazwa kuwa moja ya vivutio vya urithi wa dunia na Unesco mwaka 2013.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Huo ni tamaduni uliopitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine na watu wote walio pande mbili zinazounganishwa na daraja hilo wakichangia ''ujenzi'' wake.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Kulingana na utamaduni wa jamii ya Waperu wanaoishi karibu na kivukio hicho ni wanaume pekee wanaoruhusiwa kujihusisha na utengenezaji wake.
Wanawake wanasaidia kusuka kamba ndogo za mwanzo lakini zile zinazosemekana kuwa madhubuti zaidi zinaachiwa wanaume kutengeneza.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Siku ya kwanza wa kufanyia ukarabati daraja hilo wanaume hukusanyika pamoja kufungua kamba zilizozeka na kuanza kuweka zingine mpya hadi wahakikishe zimekuwa kubwa na imara.
Udhabiti wa mkuu wa daraja hilo unatokana na kamba sita ambazo zinakadiriwa kuwa na upana wa futi moja, na kila moja imeunganishwa kwa ustadi kwa kutumia kamba zingine 120 spesheli zilizotengenezwa makhusi kwa shughuli hiyo.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Kila familia inachangia sehemu ya kamba hizo ambazo zinazotengenezwa kutokana na aina fulani ya nyasi ngumu inayojulikana kama aqoya ichu.
Ili iweze kutumika nyasi hizo hulainishwa kwa kungongwa na jiwa maalum na kisha kutowekwa kwa maji.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Wakati kila mmoja anaendelea na shughuli hiyo maalum wanavijiji kadhaa huwapikia wenzao kwa kutiumia jiko maalum walilokuja nalo kwa ajili ya sherehe hiyo.
Baada ya kuweka daraja mpya ile ya zamani hukatwa na kuachwa ining'inie hadi ioze na kukatika .

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Nne kati ya kamba sita zilizotengenezwa kutokana na nyasi hutumika kama njia ya kupitia na mbili zilizobakia hutumiwa kama sehemu ya kujishilia usianguke aukitembea.
Kama hizo sita hufungiwa kwenye miamba mikubwa ilioko pande zote mbili na kazi ya wanaume ni kuhakikisha kamba hizo zimevutwa hadi zikawa madhubuti kabisa kutembelewa na watu bila hofu.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Siku ya tatu wanaume wachache wanatembea juu ya kamba hizo bilo hohu ya kuanguka mtoni huku wakifunga kamba zingine nyembamba zinazoungaznisha sehemu ya watukujishikilia wanapotembea juu ya daraja hilo, ili wavuke salama.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Hakuna vitu vya kisasa kama mashini zinazotumika katika mchakato mzima wa utengenezaji wa daraja hili isipokuwa nyasi na uwezo wa binadamu.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Ukarabati wa daraja la Q'eswachaka hufanyika mara moja kwa mwaka, na kilele chake ni sherehe inayojumuisha vyakula vya kila aina na burudani la muziki siku ya nne ambayo huangukia jumapili ya pili ya mwezi Juni.

Chanzo cha picha, Jordi Busque
Picha zote ni za All photographs by Jordi Busqué












