Kenya: Maafisa 8 wa polisi wauawa katika mlipuko wa bomu Wajir

Picha ya faili: Maafisa wa nne wa polisi wa Kenya walipoteza maisha yao katika eneo la Liboi baada ya gari la kulipulia na bomu lililotegwa ardhini

Chanzo cha picha, AFP

Maafisa wanane wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya gari la polisi lililokuwa likipiga doria mjini Wajir Kaskazni mwa Kenya kukanyaga bomu.

Inspekata jenerali a polisi Hillary Mutyambai ametoa taarifa iliosema kuwa gari hilo llikuwa imewabeba maafisa 11 na ilikuwa ikipiga doria katika mpaka wa Kenya na Somalia.

Tayari vikosi vya usalama ikiwemo wale wa anagni wamepelekwa katika eneo hilo kufuatia kisa hicho.