Tetesi za soka Jumapili 07.04.2019:Hazard,Neymar,Ndombele

Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eden Hazard

Chelsea wametupilia mbali ofa ya £100m kutoka kwa Real Madrid ili kumnasa kiungo wa Ubelgiji Eden Hazard, 28. (Independent on Sunday)

Kiungo wa kati wa Ufaransa, Paul Pogba,26, na mlinda mlango David de Gea, 28, ni sehemu ya wachezaji saba wa Manchester United wanaofikiria kukiacha kilabu hicho.(Sunday Times )

Mlinda mlango wa Everton Jordan Pickford, 25, na wa Atletico Madrid Jan Oblak, 26, ni machaguo ya Manchester United ikiwa watampoteza De Gea, ambaye pia anawaniwa na PSG.(Sunday Express)

Manchester United imekua ikimuwinda beki wa kulia wa PSG Thomas Meunier, 27, tangu mwanzo wa msimu. (Sun on Sunday)

Kiungo wa kati wa Lyon Tanguy Ndombele anawindwa na Manchester United, lakini iko kwenye mpambano na PSG kumnyakua mchezaji huyo mwenye miaka 22.(L'Equipe - in French)

Memphis

Chanzo cha picha, Jean Catuffe

Maelezo ya picha, Memphis Depay

Liverpool huenda ikamchukua mshambuliaji wa Lyon Memphis Depay, 25, kama winga wa Senegal Sadio Mane, 26, ataondoka Anfield kipindi cha majira ya joto.(L'Equipe, via Mail on Sunday)

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, 27,anasikitika' sana' kuondoka Barcelona, anasema aliyekua mchezaji mwenzie ndani ya kikosi hicho Adriano. (Cadena Ser)

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino anafikiria kumfanya Aaron Wan-Bissaka wa Crystal Palace kuchukua nafasi ya winga wa kulia wa England Kieran Trippier, 28,. (Sunday Express)

Kocha wa Chelsea Maurizio Sarri anamtaka mshambuliaji Olivier Giroud aendelee kubaki kwenye klabu.Mkataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 32 unafikia tamati mwezi Juni lakini klabu hiyo inataka kuongeza mkataba kwa miezi 12.(Star on Sunday)

Leicester City,Everton, Southampton, Tottenham na West Ham wanawania sahihi ya mshambuliaji wa Fulham Aleksandar Mitrovic.(Sportski Zurnal, via Leicester Mercury).

Ndombele

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tanguy Ndombele

Klabu ya nchini china Guangzhou Evergrande pia inamtaka Mitrovic na iko tayari kulipa pauni mililoni 50 inayotakiwa na Fulham pamoja na kumlipa mchezaji huyo pauni 300,000 kila wiki. (Sunday Express)

Everton itapata pauni milioni 5 ikiwa mshambuliaji wao wa zamani Romelu Lukaku ataondoka Manchester United majira haya ya joto.Mchezaji huyo mwenye miaka 25 anahitajika na Inter Milan.(Sunday Telegraph)

Kocha wa Bournemouth Eddie Howe amesema winga wa Scotland Ryan Fraser huenda asiwe na klabu hiyo msimu ujao.Mchezaji huyo mwenye miaka 25 anawaniwa na Arsenal.(Sun on Sunday)

QPR have made contact with Rui Almeida, Kocha wa club Troyes, wakati wakiendelea kutafuta mbadala wa Steve McClaren .(Football.London)

Mtoto wa nguli wa chezo wa soka Ronaldinho mwenye umri wa miaka 14 ametia saini mkataba wa miaka mitano na klabu ya Cruzeiro.(Cruzeiro - in Portuguese)