Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 10.11.2018: Sanchez, Mata, Heaton, Darmian, De Ligt, Mignolet, Jagielka

Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 29
Maelezo ya picha, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 29, mshambuliaji wa klabu ya Manchester

Inaripotiwa kuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ya Uingereza raia wa Chile, Alexis Sanchez mwenye umri wa miaka 29, anataka kuachana na klabu hiyo ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tangu ajiunge nayo akitokea klabu ya Arsenal. ( Times).

Beki wa kulia wa klabu ya Manchester United, Muitaliano Matteo Darmian ana uwezekano mkubwa wa kuondoka kwenye klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi January, ambapo klabu za Inter Milan na AS Roma zimeonesha nia ya kumtaka. (Sun).

Mlinda mlango wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Ubelgiji Simon Mignolet mwenye umri wa miaka 30 anawindwa na kocha wa klabu ya Nice ya Ufaransam Patrick Viera. (Het Belang van Limburg, via Mirror).

Tom Heaton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tom Heaton

Klabu ya Huddersfield inajiandaa kutoa ofa kwa mlinda mlango wa klabu ya Burnley, Tom Heaton mwenye umri wa miaka 32, ambaye amepoteza nafasi kwenye timu yake baada ya raia mwenzake wa Uingereza Joe Hart kupewa nafasi. (Sun).

Klabu za Manchester City na FC Barcelona huenda zikakosa kumsajili beki wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya Ajax mwenye umri wa miaka 19, Matthijs de Ligt ambaye anahusishwa sana na kukubali ofa ya klabu ya Juventus ya Italia. (Calciomercato).

Klabu ya Chelsea ya Uingereza itashindana na timu kadhaa za Italia ikiwemo Juventus kutaka kupata saini ya kiungo wa klabu ya Brescia, Sandro Tonal ambaye thamani yake inatajwa kufikia Euro milioni 20. Kiungo huyu mwenye umri wa miaka 18 tayari amefananishwa na kiungo wa zamani wa Italia Andrea Pirlo. (Goal).

Wamiliki wa klabu ya Aston Villa ya Uingereza watafikiria uwezekano wa kuubadili uwanja wa wao ifikapo mwaka 2019 wakati huu wakiendelea na mipango ya baadae ya klabu hiyo, mipango ambayo huenda ikahusisha pia uuzaji wa haki za jina la uwanja ambao umekuwa uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 1897. (Birmingham Mail).

Beki wa kati wa kimataifa wa Morocco, Mehdi Benatia

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Beki wa kati wa kimataifa wa Morocco, Mehdi Benatia

Beki wa kati wa kimataifa wa Morocco, Mehdi Benatia mwenye umri wa miaka 31, anatakiwa kusajiliwa na vilabu vya Manchester United na Arsenal, lakini huenda akajiunga kwa mkopo na klabu ya AC Milani mwezi January, kukiwa na kipengele cha Euro milioni 15 kumnunua wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Sport Mediaset, via Calciomercato).

Nahodha wa klabu ya Everton, Philip Jagielka anaendelea kukabiliana na changamoto ya kushindwa kulazimisha kuwa chaguo la kwanza la mwalimu, amesema kocha wa klabu hiyo Marco Silva. Jagielka raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 36, hajachezea timu yake tangu kuanza kwa msimu mpya wa ligi wakati walipocheza na Wolves, ambapo alitolewa kwa kadi nyekundu katika dakika za mwisho za kipindi cha kwanza. (Liverpool Echo).

Kiungo wa klabu ya Tottenham, Harry Winks mwenye umri wa miaka 22, amesema kuwa mshambuliaji wa Crystal Palace mwenye umri wa miaka 27 na raia wa Uingereza, Andros Townsend, ambaye atacheza dhidi ya klabu yake Jumamosi hii, amekuwa akimpa mchango mkubwa wa kumsaidia kuzoea mazingira ya White Hart Lane kama mchezaji Kinda. (London Evening Standard).

Kocha wa klabu ya Newcastle United, Rafael Benitez
Maelezo ya picha, Kocha wa klabu ya Newcastle United, Rafael Benitez

Kocha wa klabu ya Newcastle United, Rafael Benitez amesisitiza kuwa mshambiliaji wake wa pembeni mwenye umri wa miaka 27 ambaye hivi karibuni aliomba kutochaguliwa katika kikosi cha timu ya taifa cha Scotland kwa sababu binafsi, hajastaafu soka la kimataifa. (Newcastle Chronicle).

Kiungo wa klabu ya Manchester United kinda Aidan Barlow mwenye umri wa miaka 18, amepandishwa jadhi na kushiriki katika mazoezi la timu ya kwanza kabla ya mechi yao na klabu ya Manchester City kwenye dimba la Old Trafford. (Manchester Evening News).

Mlinda mlango wa kimataifa wa Australia Mathew Ryan mwenye umri wa miaka 26, amesema amekuwa mlinda mlango tofauti tangu ajiunge la timu ya Brighton akitokea Valencia mwaka uliopita. (The Argus.)