Okoth Obado: Gavana wa Migori afikishwa mahakamani Kenya katika kesi ya mauaji ya Sharon Otieno

Sharon

Chanzo cha picha, SHARON OTIENO/FACEBOOK

Maelezo ya picha, Marehemu Sharon Otieno
Muda wa kusoma: Dakika 1

Mwansiasa mkuu nchini Kenya leo amefikishwa mahakamani katika mji mkuu Nairobi kwa mashtaka ya kusaidia na kupanga mauaji.

Gavana wa jimbo la Migori nchini Kenya Okoth Obado amesomewa mashtaka katika kesi ya mauji ya mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu , Sharon Atieno.

Obado amekana mashtaka na mahakama imeamuru arudishwe rumande mpaka kesho Jumanne ambapo ombi lake la kutaka kuachiwa kwa dhamana litasikizwa.

Obado akiwa na wenzake wanatuhumiwa kuhusika katika mauaji ya kikatili ya mwanafunzi huyo.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Miongoni mwa waliofika mahakamani asubuhi hii ni pamoja na mamaake Sharon Otieno, Melida Auma.

Washukiwa wengine waliokamatwa katika kesi hiyo ni pamoja na msaidizi binafsi wa Gavana Obado Michael Oyamo, na afisa anayeaminika kumiliki gari lililotumika kumteka Sharon.

Polisi ilimkamata Gavana Obado siku ya Ijumaa wakati uchunguzi ukiendelea kuhusiana na kifo cha Sharon Otieno.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Katika siku za nyuma, Obado amekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye inasadikiwa alikuwa mpenzi wake.

Wiki mbili zilizopita, Obado aliwaambia polisi mjini Kisumu kwamba yeye binafsi angelipenda kuwajua wauaji wa Sharon ni kina nani.

Wakili wake Obado, Cliff Ombeta anasema mteja wake hana hatia na kwamba amewaeleza polisi kila kitu alichofahamu kuhusiana na kesi hiyo.

Kuuawa kwa kudungwa visu

Mtaalamu mkuu wa upasuaji wa maiti Kenya Johansen Oduor, baada ya kuuchunguza mwili wa marehemu, alisema huenda Sharon Otieno alifariki kutokana na kuvuja damu sana.

Alikuwa amedungwa kisu mara nane.

Mwili huo pia ulikuwa na alama za kukabwa shingoni, na alama nyingine zinazoashiria kwamba alijaribu kujiokoa.

Dkt Oduor alisema kuna uwezekano kwamba Sharon alibakwa.

Kesi ingali inaedelea mahakamani.