Uchaguzi wa Zimbabwe: Waandamanaji walivyopambana na polisi

Maafisa wa Polisi wakidhibiti waandamanaji

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa polisi wanaodhibiti vurugu wakifunga lango la Rainbow Towers mahali ambapo matokeo yalikwua yakitangazwa, huku wafuasi wa upinzani wa chama cha MDC wakiandamana mjini Harare kuonyesha kutokubaliana na vitendo vinavyodaiwa kuwa vya udanganyifu, 1 Agosti, 2018

Jeshi na polisi wamepambana na wafuasi wa MDC walioingia mitaani baada ya shutuma kutokea kuwa chama tawala Zanu-PF kuiba kura za urais na ubunge zilizopigwa siku ya Jumatatu

Siku ya Jumatano, matokeo ya nafasi ya ubunge yalionyesha kuwa Rais Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF alikuwa akiongoza kwa wingi wa viti, huku matokeo ya ura za urais bado hazijatangazwa rasmi.

MDC inadai kuwa mgombea wake,Nelson CHamisa, alishinda uchaguzi wa Jumatatu.

Wafuasi wa Chama cha MDC wakiandamana mjini Harare

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wafuasi wa Chama cha MDC wakiandamana mjini Harare
Presentational white space
Wafuasi wa MDC chama cha Nelson Chamisa wakichoma moto vizuizi vya barabarani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wafuasi wa MDC chama cha Nelson Chamisa wakichoma moto vizuizi vya barabarani

Raia wakisambaratishwa wakati wafuasi wa MDC walipoanza kuwasha moto kwenye mitaa ya mji wa Harare nchini Zimbabwe.

Mfuasi wa upinzani akioyesha ishara kwa polisi walipokuwa wakimwaga maji kuwasambaratisha waandamanaji

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mfuasi wa upinzani akioyesha ishara kwa polisi walipokuwa wakimwaga maji kuwasambaratisha waandamanaji

Polisi walitumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi kudhibiti vurugu wakati makundi ya watu walipochoma magurudumu na kushambulia magari ya polisi kwa mawe.

Wafuasi wa chama cha upinzani, MDC wakiimba na kucheza wakati wakiandamana kwenye mitaa ya mjini Harare

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wafuasi wa chama cha upinzani, MDC wakiimba na kucheza wakati wakiandamana kwenye mitaa ya mjini Harare
Presentational white space
Wafuasi wa chama cha upinzani, MDC wakiimba na kucheza wakati wakiandamana kwenye mitaa ya mjini Harare tarehe 1 mwezi Agosti

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wafuasi wa chama cha upinzani, MDC wakiimba na kucheza wakati wakiandamana kwenye mitaa ya mjini Harare tarehe 1 mwezi Agosti

Polisi wakiwa na ngao na fimbo, mwanzoni waliweza kuwadhibiti waandamanaji lakini vurugu zilipoanza walianza kuwafukuza watu kwenye mitaa mbalimbali.

Mfuasi wa MDC akiongea huku akionyesha ishara kwa polisi wa kudhibiti fujo

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mfuasi wa MDC akiongea huku akionyesha ishara kwa polisi wa kudhibiti fujo
Presentational white space
Maafisa wa polisi wa utuliza ghasia wakimtazama mfuasi wa MDC anayeshiriki maandamano yanayolenga kupinga vitendo vinavyoaiwa kuwa wizi wa kura uliofanywa na mamlaka za uchaguzi na chama tawala

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wa polisi wa utuliza ghasia wakimtazama mfuasi wa MDC anayeshiriki maandamano yanayolenga kupinga vitendo vinavyoaiwa kuwa wizi wa kura uliofanywa na mamlaka za uchaguzi na chama tawala

Maafisa wa kutuliza vurugu waliitwa kusaidia kuwasambaratisha waandamanaji kwenyE mitaa,hofu iliongezeka

line