Uchaguzi wa Zimbabwe: Waandamanaji walivyopambana na polisi

Jeshi na polisi wamepambana na wafuasi wa MDC walioingia mitaani baada ya shutuma kutokea kuwa chama tawala Zanu-PF kuiba kura za urais na ubunge zilizopigwa siku ya Jumatatu

Siku ya Jumatano, matokeo ya nafasi ya ubunge yalionyesha kuwa Rais Emmerson Mnangagwa wa Zanu-PF alikuwa akiongoza kwa wingi wa viti, huku matokeo ya ura za urais bado hazijatangazwa rasmi.

MDC inadai kuwa mgombea wake,Nelson CHamisa, alishinda uchaguzi wa Jumatatu.

Raia wakisambaratishwa wakati wafuasi wa MDC walipoanza kuwasha moto kwenye mitaa ya mji wa Harare nchini Zimbabwe.

Polisi walitumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi kudhibiti vurugu wakati makundi ya watu walipochoma magurudumu na kushambulia magari ya polisi kwa mawe.

Polisi wakiwa na ngao na fimbo, mwanzoni waliweza kuwadhibiti waandamanaji lakini vurugu zilipoanza walianza kuwafukuza watu kwenye mitaa mbalimbali.

Maafisa wa kutuliza vurugu waliitwa kusaidia kuwasambaratisha waandamanaji kwenyE mitaa,hofu iliongezeka