Polisi Uingereza haitoi tena taarifa za shambulio kwa Marekani

Chanzo cha picha, New York Times
Polisi wanaochuguza shambulio la bomu katika ukumbi wa burudani wa Manchester Arena wameacha kutoa taarifa kwa Marekani baada ya taarifa kuvuja katika vyombo vya habari , BBC imefahamu.
Maafisa Uingereza walighadhabishwa wakati picha zinazo onekana kuonyesha masalio kutoka shambulio hilo zilipochapishwa katika gazeti la New York Times.
Hili linajiri baada ya jina la mlipuaji Salman Abedi lilipofichuliwa kwa vyombo vya habari vya Marekani saa chache baada ya shambulio hilo lililosababisha vifo vya watu 22 wakiwemo watoto, na kuwajeruhi wengine 64.
Theresa May anatarajiwa kumuelezeaDonald Trump wasiwasi wake katika kikao ha jumuiya ya kujihami Nato baadaye.
Polisi Manchester inatarajia kurudi katika uhusiano wa kawaida wa kubadilishana intelijensia hivi karibuni, lakini kwa sasa kuna "hasira kubwa" BBC inafahamu.
Kikosi hicho kinachoongoza uchunguzi kinawasilisha taarifa kwa taasisi ya kitaifa ya kupambana na ugaidi, ambacho nacho kinasambaza taarifa serikalini na kwasababu ya makubaliano ya kubadilishaa intelijensia inasambaza pia kwa Marekani, Australia, Canada na New Zealand.
Kwa jumla watu 8 wanauziwa kufuatia shambulio hilo lililotekelezwa na raia mzaliwa Manchester Abedi, mwenye umri wa miaka 22 kutoka familia walio na asili kutoka Libya.
Imeibuka pia watu wawili waliomtambua Abedi akiwa katika chuo kikuu walipiga simu tofuati kuonya polisi kuhusu misimamo yake ya itikadi kali.

Chanzo cha picha, PA
Kuvuja kwa picha za ushahidi.
Waziri wa mambo ya ndani Uingereza Amber Rudd amesema ameudhika kwa kufichuliwa taarifa kumhusu Abedi's kinyume na ombi la UIngereza na aliionya Washington kwamba " halipaswi kutokea tena".
Hatahivyo, picha za masalio ya mlipuko, zinazo onyesha damu na begi lililotumika kuficha bomu hilo zilivuja katika gazeti la New York Times na kusababisha hisia ya hasira kutoka serikali ya Uingereza na wakuu wa polisi nchini.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya usalama anasema maafisa Uingereza wanaamini kuwa kikosi cha sheria Marekani huenda ndicho kilichozivujisha picha hizo na sio ikulu ya Marekani.
Duru kutoka serikali ya Uingereza ametaja uvujaji wa pili kama ulio wa "kiwango kingine" na kusema umesababisha "mshtuko na wengi kutoamini" katika serikali ya Uingereza.
Uchunguzi umefikia wapi?

Wanaume 8 na mwanamke mmoja wamekamatwa UIngereza tangu Jumatatu usiku akiwemo kakake mkubwa wa Abedi, Ismail, mwenye umri wa miaka 23. Mwanamke aliyezuia ameachiliwa huru.
Kakake mdogo Abedi, aliye na umri wa miaka 20, alizuiwana kikosi maalum kinachohusiana na wizara ya mamabo ya ndani katika mji mkuu Tripoli, Libya.
Akizungumza Jumatano Afisa mkuu wa polisi Manchester Ian Hopkins amesema: "Ni wazi kwamba tunachunguza mtandao.
"Na kama nilivyosema, uchunguzi unaendelea kwa kasi. Kuna uchunguzi wa kina unaoendeela na shughuli nyingi kote Manchester."
Kama sehemu ya uchunguzi, polisi ilivamia nyumba kadhaa karibu na Manchester Piccadilly kati kati ya mji, ambapo walihitajika kulipua bomu kwa udhibiti na kufunga kituo cha reli kwa muda.
Polisi wamelipua bomu jingine Alhamisi alfajiri katika makaazi katika eneo la Moss Side Manchester.












