Korea Kusini kuichukulia China hatua za kisheria

Korea Kusini imetishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya China, kufuatia ripoti kuwa China inakandamiza biashara za Korea Kusini
Korea Kusini inaamini kuwa China inajibu baada ya Korea Kusini kuruhusu kuweka kwa mitambo ya makomboa ya kujikinga kwenye ardhi yake, matamshi ambayo China inayapinga.
Ripoti za vyombo vya habari zinasema kuwa China imewashauri watoa huduma za usafiri, kuwacha kutoa huduma hizo kwa Korea Kusini.
Kampuni ya Korea Kusini ambayo iliuza ardhi ambapo mitambo hiyo ya makombora imejengwa nayo inasusiwa nchini China
Korea Kusini sasa inasema kuwa itapeleka suala hilo wa shirika la biashara duniani WTO.

Chanzo cha picha, Reuters








