Nzige wavamia mashamba ya vyakula Bolivia

Ripoti zilianza kusambaa kuwa nzige walikuwa wakionekana mashambani

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Ripoti zilianza kusambaa kuwa nzige walikuwa wakionekana mashambani

Maafisa wa Bolivia wameanza kunyunyiza kemikali za dawa ya kukabiliana na nzige ambao wamevamia eneo la mashariki mwa nchi hiyo linalozalisha chakula kwa wingi.

Nzige hao wamevamia kwa makundi kutoka Argentina, na maafisa wanataka kuwahi kuwadhibiti kabla ya kuharibu maelfu ya helktari za mimea ya vyakula mashambani.

Tisho hilo la uvamizi wa nzige liliripotiwa mwezi jana ambapo tayari wameharibu mimea katika eneo la zaidi ya hektari elfu huko mkoa wa Santa Cruz.

Jinsi nzige wanavyoathiri mimea

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jinsi nzige wanavyoathiri mimea

Rais wa Bolivian , Evo Morales aliyetembelea eneo hilo amesema hii ni mara ya kwanza nchi yake kuingiliwa na nzige.

Sasa amewaomba maafisa wa Argentina kuwasaidia kwa maarifa ya vipi kukabiliana na wadudu hao waharibifu.

Argentina iliwahi kukumbwa na tatizo kama hilo katika miaka ya 1920.

Serikali inasema itawasaidia wakulima kunyunyiza dawa

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Serikali inasema itawasaidia wakulima kunyunyiza dawa