Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Nzige wavamia mashamba ya vyakula Bolivia
Maafisa wa Bolivia wameanza kunyunyiza kemikali za dawa ya kukabiliana na nzige ambao wamevamia eneo la mashariki mwa nchi hiyo linalozalisha chakula kwa wingi.
Nzige hao wamevamia kwa makundi kutoka Argentina, na maafisa wanataka kuwahi kuwadhibiti kabla ya kuharibu maelfu ya helktari za mimea ya vyakula mashambani.
Tisho hilo la uvamizi wa nzige liliripotiwa mwezi jana ambapo tayari wameharibu mimea katika eneo la zaidi ya hektari elfu huko mkoa wa Santa Cruz.
Rais wa Bolivian , Evo Morales aliyetembelea eneo hilo amesema hii ni mara ya kwanza nchi yake kuingiliwa na nzige.
Sasa amewaomba maafisa wa Argentina kuwasaidia kwa maarifa ya vipi kukabiliana na wadudu hao waharibifu.
Argentina iliwahi kukumbwa na tatizo kama hilo katika miaka ya 1920.