Tumbili apatikana akifanya mapenzi na Paa

Tumbili mmoja kutoka Japan amerekodiwa katika kanda ya video akijaribu kufanya mapenzi na paa.
Watafiti walimuona mnyama huyo akijaribu kufanya mapenzi na paa wawili mnamo mwezi Novemba 2015 wakati wa msimu wa uzalishaji wa tumbili.
Tumbili huyo amekuwa akionekana akijaribu kuwapandia paa hao.
Tabia hiyo imeorodheshwa katika utafiti uliochapishwa katika jarida la nyani.
Tumbili huyo wa kiume asiye na hamu ya kufanya mapenzi na tumbili wenzake amekuwa akiwafukuza tumbili wengine ambao wamekuwa wakimkaribia.
Mwanzilishi mwenza wa utafiti huo Alexandre Bonnefoy alisema: Tumbili huyo alimpanda paa huyo na kuonyesha tabia za kujamiana zilizoshirikisha tabia 15 tofauti za kufanya tendo la ngono katika kipindi cha sekunde 10 kabla ya kufanya mapenzi.
Aidha, inasemekana tumbili huyo sio mnyama wa kwanza tofauti kutekeleza tendo hilo.
Mwaka 2014, ripoti ya Seal kujamiana na Penguin iligonga vichwa vya habari.












