Boko Haram waanza 'kujisalimisha'

Chanzo cha picha, AFP
Wapiganaji wengi wa kundi la Boko Haram wameanza kujisalimisha nchini Chad. Hii ni kwa mujibu wa Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari.
Boko Haram walianzisha maasi kaskazini mwa Nigeria mwaka wa 2009, na kusambaza operesheni zao katika nchi jirani ya Chad katika miaka ya karibuni.
Akiongea katika mkutano wa amani na usalama wa kanda ya Afrika Magharibi mjini Dakar, Senegal, Rais Buhari amesema wanachama wa Boko Haram kutoka Nigeria na Chad wamekua wakijisalimisha kwa jeshi la kanda linalokabiliana na wapiganaji hao.
Bwana Buhari amesema mwisho wa Boko Haram umekaribia huku wakipganaji hao wakipoteza uthibiti wa maeneo yao nchini Nigeria.








