Mwanamume ameza visu 40 nchini India

Chanzo cha picha, CORPORATE HOSPITAL
Madaktari katika mji wa Amritsar kaskazini mwa India wamesema, wametoa visu 40 kutoka kwa tumbo la mwanamume mmoja.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa amevimeza visu hivyo kwa muda wa miezi mitatu.
Daktari Jatinder Malholtra, ameambia BBC kwamba alikutana na mwanamume huyo wiki iliyopita alipokuwa akihisi maumivu makali kwenye tumbo lake.
Alisema mwanamume huyo hakuwafahamisha madaktari hao kwamba alikuwa akimeza visu.

Chanzo cha picha, CORPORATE HOSPITAL
'Tuligundua mwanamume huyo alikuwa akitafuna visu baada ya kumfanyia uchunguzi .'Dkt. Malholtra alisema.
Mwanamume huyo anaendelea kupata nafuu na yuko katika hali dhabiti.
Operesheni hiyo iliwahusisha madaktari watano na ilichukua saa tano kukamilika
Kwa sasa madaktari hao wanajaribu kutafuta sababu ya mwanaume huyo kumeza visu hivyo.












