Kwa nini mchungaji wa Nigeria alibeba bunduki aina ya AK-47 kwenye mimbari?

.

Chanzo cha picha, HOUSE OF THE ROCK CHURCH

Kubeba bunduki katika mimbari? Mchungaji mwandamizi wa Nigeria alikua mjadala katika mitandao mingi ya kijamii wikendi iliopita baada ya kubeba bunduki wakati alipokuwa akifanya mahubiri.

Mchungaji huyo wa kanisa la House on the Rock mjini Abuja Uche Aigbe, alizua tafrani wakati wa Ibada ya Jumapili alipopanda juu ya mimbari akiwa amebeba bunduki aina ya AK-47.

Hi haikuwa kawaida wakati ambapo alipaswa kubeba biblia, mafuta ya upako au bakuli ya maji matakatifu ambapo wahubiri wengi kawaida hubeba wanaposimama juu ya mimbari.

Lakini ni kwanini mhubiri Uche alibeba bunduki aina ya AK47 kanisani?

‘Chunga Imani yako’

Hii ndio iliokuwa mada kuu ya mahubiri ya Jumapili, kulingana na kile kanisa lilichapisha kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwa hivyo mchungaji Uche alibeba bunduki kanisani ili atumie kama kielelezo juu ya kwa nini washiriki wa kanisa ‘wanahitaji kutumia bunduki na kutetea imani yao’

Alipopanda mimbara kwa mara ya kwanza, washiriki wa kanisa walicheka kwa sura isiyo ya kawaida ya bunduki aliyoifunga kwa nyuma, lakini mchungaji huyo aliwaambia “wasiondoke wakae walipo, nimekuja nikiwa tayari asubuhi ya leo kwa sababu nahitaji kulinda imani”, alisema huku akiinua bunduki juu kuwaonyesha alichokuwa anamaanisha.

‘’Tunaishi katika nyakati ambazo tunahitaji kulinda Imani yetu lakini tunahitaji kulinda imani yetu dhidi ya majambazi , maharamia , dhidi ya watu waovu ambao hawataki Mungu aongoze Maisha yetu’’, aliongezea.

Hatahivyo kuonekana kwa bunduki kanisani kuliwafanya watu kuwa na mjdala katika mitandao ya kijami huku wengine wakitetea kitendo hicho , lakini wengine walishangaa iwapo ni sawa kumiliki bunduki au kuingia nayo kanisani kwa mahubiri.

Jinsi watu walivyotoa maoni yao katika mitandao ya kijamii

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 1

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 2

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe, 3

Je, ni halali kubeba bunduki nchini Nigeria?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Sheria ya bunduki ya Nigeria inasimamiwa na Sheria ya Silaha sura ya 146 ya Sheria za Jamhuri ya Shirikisho ya Nigeria 1990.

Sheria hiyo ya kumiliki bunduki inazungumzia jinsi ya kumiliki bunduki risasi au silaha

Kulingana na sheria hii , hakuna mtu anayepaswa kubeba bunduki binafsi ijapokuwa tu iwapo ana leseni kutoka kwa inspekta mkuu wa polisi.

Inspekta jenerali wa polisi ana uwezo a kutoa au kukataa kutoa leseni kulingana na kile kilichoamuliwa na baraza la kitaifa la mawaziri. Kulingana na sheria hii hakuna aliye na haki ya kumiliki silaha au bunduki.

"Kwa kuzingatia masharti ya kifungu kidogo cha (5) cha kifungu cha 5 cha Sheria hii, hakuna mtu ambaye, kama ana haki, atakuwa na haki ya kutoa leseni au kibali chochote chini ya Sheria hii, na mamlaka inayopewa jukumu la kutoa leseni hiyo. au kuruhusu kustahiki bila kulazimishwa kutoa sababu yoyote, kwa hiyo kukataa kutoa leseni au kibali hicho au, kwa kuzingatia masharti ya kanuni yoyote chini ya kifungu cha 33 cha Sheria hii, inaweza kuweka masharti au masharti kama ni sababu, na inafaa kufutwa leseni hiyo au kibali kwa sababu kama inavyoona inafaa.

Kifungu cha 7, kifungu kidogo cha 2 (a- e) cha sheria kinasema:

Bila ya kujali masharti ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki, hakuna leseni au kibali chini ya masharti ya Sheria hii kitakachotolewa ikiwa kuna sababu ya kuamini kuwa mwombaji au mwenye leseni-

(a) Ana chini ya umri wa miaka kumi na saba;

(b) Hana akili timamu

c) Hafai kuwa na bunduki inayohusika kwa sababu ya ulemavu wa macho;

(d) Ni mtu ambaye hawezi kujizuia

(e) Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita alitiwa hatiani kwa kosa linalohusisha vurugu au tishio la vurugu.

Sheria hiyo inasema.