Kinachofuata ni kipi baada ya IEBC kumtangaza William Ruto kama mshindi?

tg

Chanzo cha picha, William Ruto/William Ruto

Baada ya kutangazwa kwa William Ruto kama rais mteule wa Kenya ,wengi wanajiuliza kinachofuata ni kipi? Katiba imeweka mud awa kila hatua kuchukuliwa katika hali tofauti baada ya uchaguzi .

Haya hapa matukio yatakayofuata katika kila hali tofauti kulingana na maamuzi yatakayofanywa na kila upande wa kisiasa na mahakama .

Kwanza ,kuna vidhibiti vya muda kwa-

Maelezo ya video, Matokeo ya uchaguzi Kenya 2022: Kitu gani kinaweza kutokea baada ya matokeo kutangazwa

• Kuwasilisha ombi la kupinga uchaguzi wa urais: Kikomo cha Siku 7 baada ya kutangazwa kwa matokeo

• Uamuzi wa ombi: Kikomo cha Siku 14 baada ya kuwasilisha

• Uchaguzi mpya baada ya kubatilishwa: kina Kikomo Siku 60 baada ya uchaguzi wa kwanza

• Kipindi cha marudio: Ndani ya Siku 30 baada ya uchaguzi wa kwanza

Rais mteule anachukua madaraka lini?

 -Iwapo hakuna Ombi Lililowasilishwa anafaa kuapishwa Jumanne ya Kwanza, siku 14 baada ya kutangazwa kwa matokeo.

 -Iwapo rufaa ya kupinga matokeo itawasilishwa ataapishwa Jumanne ya Kwanza, siku 7 baada ya mahakama kutangaza uchaguzi kuwa halali.

 -Matokeo kutangazwa ndani ya siku 7

-Rais Mteule Kuapishwa

Hali ya 2:Kuna mshindi aliyeafikia vigezo vyote/Matokeo

-Matokeo yatatangazwa ndani ya siku 7

-Rufaa imewasilishwa ndani ya siku 7 baada ya matokeo kutangazwa

- Mahakama ya Juu kuamua ombi hilo ndani ya siku 14

-Rais Mteule Aapishwa iwapo uchaguzi utaidhinishwa na Mahakama ya Juu

Hali ya 3: Rufaa kuwasilishwa/ Matokeo kufutiliwa mbali (Uchaguzi mpya)

-Uchaguzi kufanyika Agosti 9

-Matokeo kutatangazwa ndani ya siku 7

-Ombi kuwasilishwa siku 7 baada ya mshindi kutangazwa

- Mahakama ya Juu kuamua ombi hilo ndani ya siku 14

-Uchaguzi mpya baada ya siku 60 tangu tarehe ya kufutwa kwa uchaguzi

-Matokeo ya uchaguzi kutangazwa ndani ya siku 7

-Rais mteule kuapishwa

Hali ya 4: Iwapo matokeo ya duru ya kwanza yatafutiliwa mbali na mahakama

-Uchaguzi Mpya kufanyika siku 60 baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa kwanza

-Matokeo Mapya ya Uchaguzi kutangazwa

-Kesi kuwasilishwa ndani ya siku 7 baada ya kutangazwa kwa matokeo Mapya ya uchaguzi

- Mahakama ya Juu kuamua ombi hilo ndani ya siku 14

-Rais Mteule Aapishwa

Maelezo ya video, Uchaguzi wa Kenya 2022:Kutana na Linet Chepkorir ‘Toto’ mbunge wa umri mdogo zaidi Kenya