Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 16.11.2024

Muda wa kusoma: Dakika 3

Pep Guardiola afanya uamuzi kuhusu mustakabali wake Manchester City, Manchester United wanamtaka mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani na timu mbili za London zinamtaka mchezaji wa kimataifa wa Brazil.

Pep Guardiola, 53, amefikia makubaliano ya kimsingi ya kuongezwa kwa mwaka mmoja mkataba wake Manchester City. (Football Insider)

Manchester United itakabiliana na ushindani kutoka kwa Union Berlin kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Leon Goretzka, 29, ambaye anatatizika na hali yake katika klabu ya Bayern Munich. (Team Talk)

Ruud van Nistelrooy ametuma ombi la kuwa kocha mkuu wa Coventry City baada ya kuacha nafasi yake kama kocha msaidizi wa Manchester United. (Talksport)

Fulham wameungana na wapinzani wao wa London Brentford kumwinda mshambuliaji wa Botafogo na Brazil Igor Jesus, 23. Newcastle United na Nottingham Forest pia wanavutiwa na mchezaji huyo. (TBR)

Juventus wanakamia kumnunua beki wa Fulham na Denmark Joachim Andersen, 28, na mlinzi wa Chelsea na Ufaransa Benoit Badiashile, 23. (La Gazzetta dello Sport)

West Ham wanamfuatilia kwa karibu beki wa Brighton Tariq Lamptey, 24, na wako katika nafasi nzuri ya kushinda Everton katika mbio za kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana msimu ujao kwa uhamisho wa bure. (Football Insider)

Tottenham pia wanataka kumnunua Lamptey kwa nia ya kuimarisha safu ya ulinzi ya Ange Postecoglou wakati wa uhamisho wa wacheziji wa Januari. (Teamtalk)

Barcelona wanavutiwa na winga wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anakadiriwa kuwa na thamani ya euro milioni 67. (Repubblica, kwa Kiitaliano - usajili unahitajika)

Beki wa Ujerumani Mats Hummels, 35, huenda akaamua kustaafu ikiwa hatapata nafasi ya kuondoka Roma mwezi Januari. (Sky, kwa Kijerumani)

Manchester United wanaamini kuwa huenda wakahitaji kufanya uamuzi wa kumnunua mchezaji wa Rosenborg Sverre Nypan,17, haraka iwezekanavyo ili wapate saini ya kiungo huyo wa kati wa Norway. (Givemesport)

Bayern Munich wanafikiria kumsajili mshambuliaji wa Lille na Canada Jonathan David. Mkataba wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 unamalizika msimu ujao na hana mpango wa kusaini mkataba mpya. (Anga, kwa Kijerumani)

Beki wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 24, anajua Real Madrid wako tayari kukubali masharti yake na makubaliano ya awali ya kandarasi yanasubiriwa tarehe 2 Januari. (Marca)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi