Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Villa yajiunga na mbio za kumsaka Calvert-Lewin

Lewin

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Aston Villa iko tayari kuchuana na AC Milan na Newcastle katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 28, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Everton. (Sun)

Newcastle inatarajia kupokea ofa rasmi kutoka kwa Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, wiki ijayo. (Mail)

Manchester United imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, ambaye pia anawaniwa zaidi na Juventus. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Winga wa Ecuador Jeremy Sarmiento, 23, yuko tayari kuondoka Brighton msimu huu wa kiangazi lakini anataka kubaki Ulaya. (Athletic - usajili unahitajika)

Leeds imewasilisha ofa ya pili ya euro 32m (£28m) kumsajili winga wa Feyenoord wa Brazil Igor Paixao, 25. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Burnley inamfukuzia mlinda lango wa Uingereza Sam Johnstone, 32, kutoka Wolves huku wakimtafuta mchezaji atakayechukua nafasi ya James Trafford, 22, ambaye amejiunga na Manchester City. (Sun)

 Gabriel Jesus,

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Klabu za Barcelona, AC Milan na Inter Milan zinamuwania mchezaji wa Arsena Gabriel Jesus

Klabu za Newcastle na Tottenham zinavutiwa na mchezaji wa Arsenal Gabriel Jesus, 28, lakini mshambuliaji huyo wa Brazil pia anasakwa na Barcelona, AC Milan na Inter Milan. (Caught Offside)

West Ham wanamfuatilia kipa wa Sheffield United Muingereza Michael Cooper, 25. (Sun)

Toulouse wameanza mazungumzo na Brighton kuhusu kiungo wa Malick Yalcouye mwenye umri wa miaka 19. (Fabrizio Romano)

Wolves inafuatilia mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Morocco Amine Adli, 25, lakini Bayer Leverkusen inataka euro 30m (£26.2m). (Bild - kwa Kijerumani)

Mshambulizi wa Everton na Guinea-Bissau Beto, 27, anapigiwa upatu kujiunga na Atalanta. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Fulham imewasilisha ombi la kumsajili kiungo wa Chelsea Muingereza Kiernan Dewsbury-Hall, 25. (GiveMeSport)

Manchester United, Newcastle na Tottenham zitachuana kuwania saini ya mshambuliaji wa Serbia na Al-Hilal Aleksandar Mitrovic, 30. ( Caught offside).

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi