Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Man City na Man Utd wanamtaka Donnarumma

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Manchester City zote zinavutiwa na mlinda mlango wa Paris St-Germain wa Italia Gianluigi Donnarumma, 26, huku timu hiyo ya Ligue 1 ikiwa tayari kumnunua kipa wa Lille Mfaransa Lucas Chevalier, 23, kama mbadala wake. (L'Equipe - in French)
Galatasaray pia wanatazamiwa kumtafuta Donnarumma, ambaye anakaribia kuingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake huko Paris St-Germain. (Footmercato - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images
Arsenal wanatumai kufikia dili la pauni milioni 60 kwa ajili ya Eberechi Eze wa Crystal Palace, huku mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 27 akitaka kuhamia katika kikosi cha Mikel Arteta. (Footmercato - in French)
Everton wako kwenye mazungumzo na Bayern Munich kuhusu uhamisho wa pauni milioni 7.8 kwa ajili ya beki wa kushoto wa Morocco Adam Aznou, 19. (Athletic - subscription required)

Chanzo cha picha, PA Media
Flamengo wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Brazil na Arsenal Gabriel Jesus, 28. (RTI Esporte - in Portuguese)
Benfica wanashinikiza kumsajili Joao Felix kutoka Chelsea, huku mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 25 akiwa na matumaini ya kurejea katika klabu yake ya utotoni. (Florian Plettenberg)

Chanzo cha picha, Getty Images
Fulham wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho ya kutaka kumsajili tena winga wa Arsenal Muingereza Reiss Nelson, 25, ama kwa mkopo wakiwa na chaguo la kumnunua au kwa mkataba wa kudumu. (Athletic - subscription required)
Everton wako kwenye mazungumzo na Lyon kuhusu mpango wa kumnunua winga wa Ubelgiji Malick Fofana, 20. (Fabrizio Romano)
Toffees wametoa ofa ya takriban £31m kwa Fofana, lakini Lyon wanataka angalau £35m. (L'Equipe - in French)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Burnley sasa wameonyesha nia yao kama Brentford, Southampton na Borussia Dortmund wote wakivutiwa na mshambuliaji wa Metz wa Senegal Idrissa Gueye, 18. (Sun)
West Ham na Benfica wanapanga kutuma ofa kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Cagliari wa Italia Roberto Piccoli, 24, ambaye thamani yake ni karibu £26m. (Calciomercato - in Italian)
Leeds wako tayari kulipa pauni milioni 28 pamoja na nyongeza kwa ajili ya Igor Paixao wa Feyenoord, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Marseille na Roma ambao pia wanataka kumnunua mshambuliaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 26. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wanatazamia kutoa ruzuku ya mshahara wa winga wa Uingereza Raheem Sterling ili kukamilisha uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 kwenda Fulham. (Football Insider)
West Ham wanafikiria kumnunua Romano Schmid wa Werder Bremen, ambaye thamani yake ni takriban £13m. Aston Villa na Fulham pia wanamfuatilia kiungo huyo mshambuliaji wa Austria mwenye umri wa miaka 25. (Guardian)















