Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi: Antony, Shaw wagombaniwa Uarabuni

Chanzo cha picha, Getty Images
Vilabu viwili vinavyoongoza kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia vinataka kumsajili Antony kutoka Manchester United huku uwezekano wa kurejea Real Betis, ambako winga huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 alicheza kwa mkopo msimu uliopita, ukiwa mdogo (Sky Sports).
Beki wa kushoto wa England Luke Shaw pia yuko tayari kusikiliza ofa kutoka vilabu vya Saudi Arabia huku akiwa tayari kuondoka Manchester United baada ya misimu 11 akiwa Old Trafford. Shaw ana umri wa miaka 30 (Sun).
Manchester United wamekataliwa ombi lao la mkopo kwa ajili ya kipa wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez mwenye umri wa miaka 32 (Sun).
Newcastle United wanamtaka mshambuliaji wa Wolves raia wa Norway mwenye umri wa miaka 25, Jorgen Strand Larsen, kama mbadala wa mshambuliaji wa Sweden Alexander Isak, 25, endapo ataondoka msimu huu wa kiangazi (Express & Star).

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa England Callum Wilson, 33, amekubaliana masharti binafsi na West Ham baada ya kuondoka Newcastle baada ua mkataba wake kumalizika mwezi uliopita (Talksport).
Manchester City wametoa ombi jipya kwa beki wa pembeni wa Newcastle, Tino Livramento, na wako tayari kutoa zaidi ya pauni milioni 50 kwa ajili ya mchezaji huyo wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 22 (TBR Football).
Bayern Munich wameanza tena mazungumzo na Liverpool kuhusu mpango wao wa kumsajili Luis Diaz, lakini klabu hiyo ya Bundesliga bado haijatoa ofa ya pili kwa winga huyo wa Colombia mwenye umri wa miaka 28 (Athletic).
Chelsea wamekataliwa ofa yao ya zaidi ya pauni milioni 60 na Juventus kwa ajili ya mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz mwenye umri wa miaka 20 (La Gazzetta dello Sport).

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Fulham wako mbioni kukamilisha usajili wao wa kwanza wa majira haya ya kiangazi kwa kumchukua kipa Mfaransa Benjamin Lecomte, 34, kutoka Montpellier (Standard).
Everton wameongeza jina la winga wa Southampton mwenye umri wa miaka 19 raia wa England, Tyler Dibling, kwenye orodha yao ya wachezaji wanaowalenga ili kuimarisha safu ya wachezaji wa pembeni (Times).
Leeds United wamewasilisha ofa ya zaidi ya pauni milioni 26 kwa winga wa Feyenoord Igor Paixao, lakini Roma na Marseille ni kati ya vilabu vinavyomtaka mchezaji huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 25 (Sky Sports).
Tottenham wamekubali kwa shingo upande kumruhusu Mikey Moore, 17, kujiunga na timu nyingine kwa mkopo msimu ujao, huku Birmingham City na West Brom zikiwa na nia ya kumsajili winga huyo wa Kiingereza (Football Insider).
Burnley waliopanda Ligi Kuu ya EPL msimu huu wameulizia upatikanaji wa kiungo wa kati wa Sweden Jens Cajuste, 25, kutoka Napoli ambaye alicheza kwa mkopo Ipswich Town msimu uliopita (Gianluca di Marzio).















