Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi 5 kubwa za soka Jioni hii: Man City kumnunua Reijnders wa Milan kwa £52m
Manchester City wanaripotiwa kuandaa ofa ya euro milioni 60 (£52m/$66m) ili kupata huduma ya kiungo wa AC Milan Tijjani Reijnders, kulingana na Calciomercato.
Ingawa Reijnders alijitolea hivi majuzi tu kuongeza mkataba ambao unamfunga San Siro hadi 2030, Milan inaweza kuzingatia ofa hiyo ambayo inahsisha kiwango kikubwa ch kifedha.
Ada hiyo ya uhamisho inaweza kuwa ya faida kubwa zaidi kwa upande wa Italia kwa Milan kuipuuza.
Liverpool ina imani Van Dijk, MoSalah watasalia Anfield
Fabrizio Romano ameeleza kwamba Liverpool 'ina imani kubwa kwamba Virgil Van Dijk na Mohamed Salah watasalia, huku klabu hiyo ikitaka mikataba mipya ya nyota hao isainiwe haraka iwezekanavyo , wakati huu Trent Alexander-Arnold akikaribia kutimkia Real Madrid.
Kumekuwa na mjadala kwa muda mrefu kuhusu mustakabali wa nyota hao watatu hao, baada ya kusifiwa kama wachezaji watatu muhimu zaidi katika kikosi cha Arne Slot katika kipindi chote cha kampeni msimu huu.
Kutosaini mikataba mipya kunaongeza hofu ya kuondoka kwao, ambapo tayari inaonekana Madrid wakikaribia kukamilisha usajili wa bure wa Alexander-Arnold.
Waarabu wao wanamtaka bado Mo Salah
Man United yamtaka Ederson kwa
Manchester United wanaripotiwa kujiandaa kumnunua Ederson, kiungo mahiri wa Brazil anayeng'ara kwa sasa Atalanta, kwa mujibu wa GiveMeSport.
Wasiwasi unaongezeka juu ya hali ya Kobbie Mainoo huko Old Trafford, kwani kijana huyo bado hajaamua kama atabaki na kuongeza mkataba mpya ama ataondoka United. Huku uwezekano wa kuondoka kwake ukiongezeka, United sasa wanaoingeza jitihada zao za kumnunua Ederson huku wakitarajia kujiimarisha kabla ya kampeni mpya mwezi Agosti.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ataelekea majira ya kiangazi akiwa na bei ya pauni milioni 52.
"Nina ofa kila kona"- Pogba
Nyota wa zamani wa Manchester United Paul Pogba anasema ana hamu ya kurejea uwanjani na kwamba amekuwa akipokea "ofa nyingi kutoka kila upande".
Pogba alifungiwa kucheza soka baada ya kugundulika anatumia dawa za kusisimua misuli.
Mfaransa huyo aliiambia GQ: "Kwanza kabisa, nna hamu ya kucheza. Unajua, ni muda mrefu sana tangu nicheze soka. Sikuwahi kufikiria ningekuwa huru wakati huu wa msimu. Sijawahi kushuhudia uhamisho kama huu. Leo, kuna ofa. Zinatoka pande zote. Kutoka pande zote. Nataka kuona ni ipi inanifaa zaidi. Kwa sababu niko kwenye kipindi muhimu cha maisha yangu na kufanya maamuzi' mazuri ni muhimu."
Pogba alifungiwa miaka minne baada ya kupimwa na kukutwa akitumia dawa iliyopigwa marufuku - dehydroepiandrosterone , baada ya mechi kati ya Juventus na Udinese mwaka 2023. Hata hivyo, adhabu hiyo ilipunguzwa baada ya mchakato mrefu wa kukata rufaa.
Chelsea na Newcastle zapigana vikumbo kwa
Chelsea na Newcastle zinaongoza mbio za kumsajili mshambulizi wa Benfica Vangelis Pavlidis, katika dirisha la msimu huu wa joto, ambaye ana kipengele cha kuachiliwa kwa €100m.
Mchezaji wa kimataifa wa Ugiriki, amefunga mabao 24 katika michezo 46 katika michuano yote na pia ametoa pasi za mabao 10. Mkataba wake unamalizika 2029, akiwa amewasili hivi karibuni kutoka AZ Alkmaar kwa mkataba wa €20m (£17m) msimu wa joto.
Mchezaji huyo anaelezwa na kuaminika kuwa anaweza kutoa ushindani kwa Nicolas Jackson pale Chelsea, huku Magpies wakiripotiwa kuvutiwa naye iwapo Alexander Isak ataondoka (goal.com)