Ni nini kitakachofuata baada ya Gachagua kuondolewa madarakani?

Chanzo cha picha, EPA
Bunge la Seneti nchini Kenya limepiga kura kwa kauli moja kumvua madaraka Naibu wa Rais Rigathi Gachagua.
Maseneta waliendelea kujadili hoja ya kumuondoa mamlakani licha ya kufahamishwa kuwa Gachagua amelazwa hospitali akiugua maumivu makali kifuani.
Mawakili wake wakiongozwa na Paul Muite waljiondoa katika mchakato huo wakihoji kuwa hawawezi kuendelea bila uwepo wa mteja wao bungeni.
Walipigia kura hoja zote 11 zilizowasilishwa dhidi ya Bw. Gachagua na hatimaye kuidhinisha hoja tano kati ya hizo.
Baada ya utaratibu huo ulioendelea bungeni hadi karibu saa sita usiku Alhamisi sasa macho yote sasa yanaelekezwa kwa ni nani atakayechukua nafasi yake.
Rais atahitajika kumteua Naibu Rais mpya ndani ya siku 14 na kuwasilisha jina lake katika Bunge la kitaifa.
Tangu mchakato wa kumuondoa mamlakani kuanza katika bunge la kitaifa wiki iliyopita na hatimaye kuishia katika Bunge la Seneti vyombo vya habari vya Kenya vimekuwa vikiripoti kuhusu uwezekano wa viongozi kadhaa kuchukuwa nafasi ya Gachagua:
- Gavana wa Kaunti ya Murang'a Irungu Kang'ata
- Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru
- Waziri wa Mambo ya Ndani Kithure Kindiki
- Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi.
Rais William Ruta hajatoa tamko lolote hadharani kuhusu masaibu yaliyomkumba naibu wake.
Hata hivyo Bunge la Kitaifa litahitajika kufuata taratibu za kikatiba zilizoainishwa katika Kifungu cha 149 kumuidhinisha mchakato huo.
Rais lazima amteue mgombea atakaechukua nafasi hiyo ndani ya siku 14 baada ya Naibu wa rais kuondolewa madarakani.
Bunge la Kitaifa linatarajiwa kuwa na kikao maalum siku ya Ijumaa, ambacho huenda kitajumuisha kusailiwa kwa Naibu Rais aliyeteuliwa.
Jina Naibu wa Rais Mtarajiwa likiwasilishwa, Bunge litakuwa na siku 60 kuidhinisha uteuzi wake."
Kwa mujibu wa Katiba, baada ya kuidhinishwa na Bunge, Naibu wa Rais mteule lazima aapishwe mbele ya Jaji Mkuu au, ikiwa haipo, jaji mwingine.
Kuapishwa kwa Naibu wa Rais Mpya hakuhitaji uwepo wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC)
siku tofauti lazima iteuliwe kwa ajili ya mchakato huo.
Kumekuwa na ripoti kwamba Naibu wa Rais Mteule anaweza kuapishwa siku ya Siku Kuu ya Mashujaa lakini wataalamu wa kisheria wanahoji kuwa hilo haliwezi kufanyika wakati wa likizo ya umma na kuongezakwamba lazima tarehe maalum itengwe kwa ajili ya kuapishwa kwa Naibu Rais.
Kwa mujibu wa Katiba, Naibu Rais atachukua madaraka baada ya kula kiapo na ana ukomo wa kuhudumu usiozaidi mihula miwili.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Kenya kwa naibu wa rais kuondolewa madarakani.
Bw Rigathi Gachagua alipangiwa kujitetea mapema Alhamisi, lakini wakili wake alifahamisha Bunge la Senet kuwa amelazwa hospitalini.
Seneti ilikataa pendekezo la kuahirisha vikao vya bunge kwa siku mbili - na kuamua kuendelea kujadili hija ya kumuonda malakani bila uwepo wake .
Uamuzi huo unamzuia kuhudumu katika wadhifa wa umma na kumnyima mafao yake ya kuhudumu kama Naibu wa Rais wa Kenya.
Bw Gachagua alikabiliwa na mashtaka 11 yakiwemo ya ufisadi, kudhoofisha mamlaka ya rais na kuchochea migawanyiko ya kikabila - mashataka ambayo aliyokanusha yote.















