Ni kipi tunachojua kuhusu rasi ya Panama ambayo Trump ametishia kuchukua udhibiti wake?

gg

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 6

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametishia kuichukua na kudhibiti rasi ya Panama iwapo serikali ya Panama haitapunguza ushuru wa forodha kwa meli za marekani zinazopitia njia hiyo.

''Ushuru wa forodha katika rasi ya Panama uko juu mno.Sio wa haki,''Trump alisema haya akiwa katika hafla eneo la Arizona. ''Kutozwa gharama kubwa kwa Marekani kunafaa kukoma haraka.''

Kauli ya Trump ilimuudhi rais wa Panama Jose Raul Molino, kila mjazo wa maji wa panama na maeneo yanayoizunguka ni ya Panama'' akiongezea kuwa uhuru wa nchi yake ni jambo lisiloweza kujadiliwa.

Ni kipi tunajua kuhusu mlangobahari wa Panama ambayo Trump ametishia kuidhibiti? Na ina umuhimu gani kwa taifa la Marekani?

Eneo la kijiografia na umuhimu wake

Rasi ya Panama ni mkondo wa maji wa pili kwa umuhimu duniani baada ya rasi ya Suez, na ni moja ya mafanikio makubwa ya uhandisi ya karne ya 20.

Iko katika nchi ya Panama, kati ya Bahari ya Pasifiki na Bahari ya Atlantiki, na ina urefu wa kilomita 77.

mlangobahari huu umezungukwa pande zote na ziwa kadhaa, kama vile ziwa Gatun,ambayo ni hazina ya maji yanayohitajika kwa rasi kuendesha shughuli za kawaida.

Mazingira katika eneo hili yana sifa ya asili tajiri katika misitu ya mvua na utofauti wa mazingira.

Rasi hii ina umuhimu mkubwa kimkakati kwani imeshikilia nafasi muhimu kwa biashara ya kimataifa, kwa kupunguza umbali wa safari za meli kutoka karibu kilomita 13,000 hadi 8,000.

Kabla ya ujenzi wa rasi hii, meli zililazimika kupita Cape Horn huko Chile, njia hatari na ndefu zaidi.

Mabadiliko haya makubwa yalichangia kuokoa muda na juhudi na kupunguza gharama za usafirishaji, na kufanya rasi kuwa jambo la lazima na muhimu katika biashara ya kimataifa.

Skip Pia unaweza kusoma: and continue readingPia unaweza kusoma:

End of Pia unaweza kusoma:

Marekani ni mtumiaji mkubwa wa rasi ya Panama

Rasi hiyo hupokea zaidi ya meli 14,000 kila mwaka - hasa meli za Marekani, China na Japan - zinazobeba bidhaa zenye thamani ya zaidi ya dola bilioni 270 za Marekani.

Vibeba magari, meli za gesi asilia, na meli za kivita hupitia kwenye rasi hiyo, pamoja na meli zilizosheheni bidhaa za kilimo kama vile mahindi na soya zinazotoka Marekani na kuelekea Asia, na bidhaa na magari ya kielektroniki kutoka Asia hadi Ulaya na Marekani.

Meli kubwa ya kwanza ya kontena inapitia rasi ya Panama uliopanuliwa.

Rasi ya Panama imekuwa muhimu kwa uchumi wa Marekani, ambayo ni mtumiaji mkubwa wa rasi hiyo, huku asilimia 73% ya trafiki ya rasi ikitokea Marekani.

Sababu kuu zilizopelekea kuongezeka kwa ushuru wa forodha ambao ulikoselewa vikali na rais mteule wa Marekani Donald Trump ni kutokana na mabadiliko ya tabianchi unaoleta changamoto kupitisha meli katika rasi hiyo.

"Ushawishi wa China unamtia wasiwasi Trump''

Picha ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Picha ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, alizungumzia China katika mazungumzo yake Jumamosi iliyopita, akisema, "Rasi hii inamilikiwa na Panama pekee, si China wala mtu mwingine yeyote. Hatujawahi, wala hatutakubali, rasi hiyo iingie mikononi mwa watu wasiofaa."

Kutokana na kauli hiyo, Trump anahofia nini?

Kwa mujibu wa tovuti ya Marekani Politico, kauli za Trump zinaonekana kuhusiana na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ushawishi wa China katika biashara ya kimataifa na miundombinu ya kimkakati.

Katika miongo miwili iliyopita, China imeongeza uwepo wake kwa kiasi kikubwa katika Marekani ya Kusini kupitia uwekezaji katika bandari, miradi ya miundombinu, na makubaliano ya kibiashara.

Ingawa China haimiliki wala kuendesha rasi ya Panama, kampuni tanzu ya CK Hutchison Holdings yenye makao yake Hong Kong imekuwa ikifanya kazi ya kuendesha bandari mbili kwenye milango ya rasi hiyo katika Bahari ya Kariba na Pasifiki.

Kwa kuzingatia ushindani wa kiuchumi kati ya China na Marekani, rasi ya Panama inaweza kutazamwa kama eneo lingine la migogoro kati yao.

Kwa mujibu wa Politico, China haijatoa ishara yoyote ya hadharani kuhusu kuchukua hatua ya kununua rasi hiyo au kupanua ushawishi wake katika shughuli zake, na kauli za Trump zinaweza kuwa ni hatua ya kuzuia, katika juhudi za kuzuia China kutekeleza upanuzi wowote uliopangwa katika Marekani ya Kusini.

Wazo lililoibuka katika karne ya 16

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Wazo la kujenga rasi inayounganisha Bahari ya Atlantiki na Pasifiki lilianza katika karne ya 16 wakati Mfalme wa Hispania, Charles V, alipopendekeza kuchimba njia ya maji kupitia eneo la Panama.

Hata hivyo, ndoto hii haikutimia kutokana na changamoto za kiufundi zilizokuwepo wakati huo.

Mwishoni mwa karne ya 19, Ufaransa ilichukua jukumu la kujenga rasi ya Panama chini ya uongozi wa diplomasia wa Ufaransa, Ferdinand de Lesseps, ambaye alisimamia ujenzi wa rasi ya Suez.

Ujenzi wa rasi ulianza mwaka 1881 na maisha ya wafanyakazi takriban 22,000 waliangamia kutokana na mazingira yake, lakini ulikamilika mwaka 1914, na meli za kwanza ziliruhusiwa kupita.

Baada ya kushindwa kwa mradi wa kwanza, kampuni mpya ya Kifaransa ilianzishwa mwaka 1894, lakini haikufanya maendeleo yoyote makubwa, na shughuli zake zilikuwa za kudumisha eneo hilo tu.

Baadaye, kampuni hiyo iliamua kuuza haki za mradi huo kwa Marekani kwa dola milioni 40.

Mwaka 1903, Marekani ilisaini mkataba na Panama, kuruhusu kuendelezwa kwa mradi wa rasi na kudhibiti ardhi zinazozunguka.

Mwaka 1904, Marekani ilianza kazi tena na Rais Theodore Roosevelt alileta timu ya wahandisi kubuni mradi na kushughulikia changamoto za kiafya.

Zaidi ya wafanyakazi 50,000 walifanya kazi, na vifo vilipunguzwa kutoka 22,000 hadi 5,000 kwa kudhibiti mbu na kuondoa kinamasi.

Rasi ya Panama ilifunguliwa rasmi 1914 kwa meli ya kwanza ya Marekani, SS Ancon.

Mapambano ya Ushawishi na Ukuu: Makubaliano na Uvamizi

Rais wa Marekani Jimmy Carter na Rais wa Panama Omar Torrijos walitia saini Mkataba wa Panama mwaka 1977

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais wa Marekani Jimmy Carter na Rais wa Panama Omar Torrijos walitia saini Mkataba wa Panama mwaka 1977

Mgogoro wa udhibiti wa rasi ulitokana na mkataba wa 1903, na ilisababisha mvutano kati ya Marekani na Panama.

Baada ya maandamano ya 1964, Marekani na Panama zilitafuta suluhu kwa mgogoro wa rasi.

Mkataba wa Torrijos-Carter uliotiwa saini 1977 na aliyekuwa rasi wa Marekani Jimmy Carter na rais Omar Torrijos ukieleza uhamisho wa rasi kwa Panama ifikapo 1999 na uhuru wake kudumishwa.

Marekani na Panama walidhibiti rasi hiyo kwa pamoja kutoka 1977 hadi 1999, wakati Panama ilichukua udhibiti kamili.

Marekani ilivamia Panama 1989 ili kumwondoa Jenerali Noriega, aliyeshutumiwa kwa biashara ya ulanguzi wa dawa za kulevya na utakatishaji fedha.

Operesheni ilimalizika kwa Noriega kujisalimisha na kusafirishwa Marekani, ambapo alitiwa hatiani kwa makosa hayo.

Uvamizi huu ulisababisha vifo na ukosoaji mkubwa, lakini ulileta demokrasia na kumaliza utawala wa Noriega.

Baada ya utawala wa Noriega kutamatika alichaguliwa rais Guillermo Endara kushika madaraka, na hivyo kufungua njia ya kurejea kwa demokrasia nchini Panama.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Imetafsiriwa na Mariam Mjahid