Meli kubwa ya vita ya Iran au njama za China: Ni nini siri ya ndege zisizo na rubani zinazoonekana katika anga za Marekani?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 5

Kuonekana kwa ndege nyingi zisizo na rubani katika anga la NewJersey na majimbo mengine ya Marekani kwa karibu mwezi mmoja limekuwa ni jambo lisilo la kawaida na ni siri ambayo bado haijafichuka.

Suala la mamlaka za nchi hiyo kutotoa maelezo au jibu thabiti juu ya ndege hizi zisizo na rubani, linafanya siri hii kuwa ya kushangaza zaidi.

Maafisa wa Marekani wanasema ndege hizo zisizo na rubani (droni) hazina tisho kwa umma wala sio suala la kutishia usalama wa taifa.

Siku ya Jumapili, Waziri wa Usalama wa Ndani Alejandro Mayorkas alithibitisha kuwa baadhi ya ndege zisizo na rubani zinafanya doria katika anga hiyo, wakati pia kuna baadhi ya ndege ambazo zinadhaniwa kuwa ni ndege zisizo na rubani.

Alisema kuwa "hakuna mtu nje ya nchi anayehusika" katika suala ndege zisizo na rubani (UAVs), zinaoonekana zikipaa angani kwa wingi.

Baadhi ya wabunge wameikosoa serikali kutokana na ripoti za ndege zisizo na rubani zinazotiliwa shaka, na kuibua pingamizi kwamba taarifa katika suala hili hazipatikani hadharani.

Unaweza pia kusoma:

Je, tunajua nini kuhusu ndege hizi zisizo na rubani hadi sasa?

Swali la kwanza ni je, ndege hizi zimeonekana wapi?

Ndege kadhaa zisizo na rubani (droni) zimeonekana angani katika jimbo la New Jersey tangu Novemba 18. Aidha, taarifa za safari hizo pia zimepokelewa kaskazini mashariki mwa Marekani.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Baadhi ya ripoti zimetoka katika tovuti nyeti ya utafiti wa kijeshi Picatinny Arsenal, wakati droni hizo pia zimeonekana karibu na uwanja wa gofu wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump huko Bedminster, New Jersey.

Mamlaka ya usafiri wa anga nchini humo (FAA) imepiga marufuku kwa muda ndege zisizokuwa na rubani katika miji ya Bedminster na Picatinny.

Wakati huo huo, ndege kadhaa zisizo na rubani zilionekana pia katika eneo la Bronx borough mjini New York mnamo Desemba 12. Kwa mujibu wa Gavana Kathy Hochul, uwanja wa ndege wa Stewart ulilazimika kufungwa kwa takriban saa moja mnamo tarehe 13 Disemba kutokana na shughuli za ndege zisizo na rubani.

Polisi mjini Connecticut pia wamethibitisha kushuhudia 'ndege zisizo na rubani.' Mfumo wa kugundua droni sasa umewekwa karibu na maeneo ya Groton na New London.

Gavana wa zamani wa Republican Larry Hogan wa Maryland alisema kuwa inaonekana kuwa 'makumi ' ya ndege zisizo na rubani zilipaa juu ya nyumba yake.

Kwa mujibu wa polisi huko Massachusetts, watu wawili walikamatwa mnamo Desemba 14 kwa mashtaka ya "operesheni hatari ya droni" katika anga la uwanja wa ndege wa kimataifa wa Logan huko Boston.

Pia ndege hizo zimeonekana mara kadhaa mashariki mwa Pennsylvania, ikiwa ni pamoja na Philadelphia. Kwa mujibu wa jarida la -Wall Street Journal, shughuli za ndege zisizokuwa na rubani zilionekana kwa siku 17 karibu na vituo vya kijeshi vya Marekani huko Virginia mwezi Oktoba.

Droni zilionekana katika vituo vitatu vya jeshi la anga la Marekani nchini Uingereza mwishoni mwa mwezi Novemba. Vyanzo vya ulinzi vya Uingereza vimeiambia BBC kuwa wanashuku kuwa "makundi yanayoungwa mkono na serikali" yalikuwa nyuma yake.

Droni pia zilionekana karibu na kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Ujerumani mapema mwezi Disemba.

h

Chanzo cha picha, Mark Kerrison/Getty

Wachunguzi wamesema nini kuhusu ndege hizo zisizo na rubani?

Maafisa kutoka mashirika ya ujasusi ya Marekani wamewaambia waandishi wa habari kwamba bado hawajapata ushahidi wowote kwamba ndege hizo zisizo na rubani ni tisho kwa umma.

"Nadhani hii inaweza kuwa na athari kubwa," afisa wa FBI alisema.

Siku ya Jumapili, waziri wa usalama wa ndani aliliambia shirika la habari la ABC News kwamba "hakuna ufahamu wa ushiriki wa nchi nyingine yoyote katika ripoti (ya kuona droni) kaskazini mashariki."

Hatahivyo, alisema, "Tuko macho kuchunguza suala hili."

"Kama kungekuwa na sababu yoyote ya wasiwasi, kama tungetambua kuhusika kwa nchi nyingine au shughuli za uhalifu, tungeuarifu umma wa Marekani," alisema Meyakas.

Kwanini ndege zisizo na rubani zinaongezeka nchini Marekani?

Baada ya mkutano wa Wizara ya usalama wa ndani mnamo Disemba 11, mbunge wa New Jersey Dawn Fantasia alisema kuwa ndege hizi zisizo na rubani zinaonekana kukwepa helikopta au ishara za redio zinazotumiwa kuzichunguzwa.

Fantasia alisema ndege hizo zina urefu wa kuruka futi sita "kulingana na ratiba ya kawaida" huku taa zikionekana kuzimwa.

Waziri Muikas aliliambia shirika la habari la ABC kwamba sheria ya shirikisho ilibadilishwa mwaka jana na ndege zisizokuwa na rubani ziliruhusiwa kuruka usiku.

Anaamini kuwa hiyo ndiyo sababu kumekuwa na ongezeko la ripoti za ndege zisizo na rubani. "Kuna sababu kadhaa kwanini watu wanaona droni zaidi sasa kuliko hapo awali, hasa kati ya alfajiri na jioni."

h

Chanzo cha picha, Mark Kerrison/Getty

Maelezo ya picha, Kwa mujibu wa Pentagon, ndege hizi zisizo na rubani zinasafirishwa kutoka ndani ya Marekani

Ndege nyingi zisizo na rubani zinatoka wapi?

Haijulikani ni nani anaziongoza

Mbunge wa Republican Jeff Van Drew wa New Jersey alidai kuwa ndege hizo zisizokuwa na rubani zilikuwa zikisafirishwa kutoka kwa "meli " kubwa ya Iran katika bahari ya Atlantic, wakati Mdemokrat Raja Krishnamurthy alisema kuna uwezekano kwamba China ilikuwa nyuma yake.

Pentagon, White House na Usalama wa Ndani wamesisitiza kuwa hakuna raia wa kigeni anayejihusisha na vitendo hivi vinavyotiliwa shaka.

Mnamo Novemba 30, mtu mmoja wa Kaskazini mwa California alikamatwa kwa kuruka ndege isiyo na rubani na kupiga picha kwenye kambi ya Vandenberg Space Force Base karibu na Santa Barbara.

Raia huyo wa China mwenye umri wa miaka 39 alikamatwa wakati akipanda ndege kuelekea China.

Haijulikani ikiwa tukio hilo linahusiana na ndege zisizo na rubani zinazoshukiwa katika maeneo mengine ya nchi.

Je, ndege hizi zinaweza kuzuiwa

Rais mteule wa Marekani Trump amesema kuwa kuna marufuku ya ndege zisizokuwa na rubani bila ruhusa ya serikali. Anasema juu ya Ukweli wa Jamii, "Acha umma ujue kuhusu hili mara moja. Vinginevyo, piga ndege hizi zisizo na rubani."

Mamlaka zimepiga marufuku ufyatuaji risasi wa ndege zisizo na rubani kwa sababu ni kinyume cha sheria. FAA imewaonya waendeshaji wa ndege zisizo na rubani katika taarifa kwamba operesheni zisizo salama na hatari zinaweza kusababisha faini ya hadi dola 75,000 na kuondolewa kwa vyeti vyao vya majaribio ya ndege zisizo na rubani.

Gavana wa jimbo la New York Hochul ametoa wito kwa serikali ya shirikisho kuruhusu majimbo kuchukua hatua kali dhidi ya ndege zisizo na rubani.

Kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti Chuck Schumer amezitaka mamlaka za shirikisho kutuma mifumo ya kugundua ndege zisizo na rubani katika miji ya New York na New Jersey.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi