Urusi inataka kuzalisha droni elfu 6 za Iran - Washington Post

gf

Chanzo cha picha, Maxar

Maelezo ya picha, Kiwanda cha Yelabuga ambako droni za Iran zinageuzwa na kuwa za Urusi

Gazeti la Marekani la Washington Post limeripoti kwamba limepokea nyaraka za siri zinazohusiana na utengenezaji wa ndege zisizo na rubani huko Tatarstan.

Gazeti hilo limepokea nyaraka zinazoeleza kipindi cha msimu wa baridi 2022 hadi vuli 2023, kutoka kwa mfanyakazi wa zamani wa kiwanda cha Yelabuga. Kwa maneno yake mwenyewe, mtu huyu alitaka kuvuruga uzalishaji na kuleta mwisho wa vita vya Ukraine.

Nyaraka hizo zinaeleza - kufikia msimu wa joto wa 2025, Wizara ya Ulinzi ya Urusi inakusudia kupokea droni elfu 6, zinazopangwa kuzalishwa na Urusi yenyewe katika kiwanda cha Yelabuga.

Tunazungumzia droni za kizazi cha 2, zitakazoundwa kutokana na droni za Shahed-136 za Irani. Zina uwezo wa kubeba takribani kilo 50 za vilipuzi na zina injini isiyotoa sauti kali sana.

Nchi za Magharibi zinajua kuhusu mkataba wa kijeshi wa mabilioni ya dola kati ya Moscow na Tehran, na Iran yenyewe ilikiri kwamba iliipatia Urusi kundi la ndege zisizo na rubani, ingawa inadai ilifanya hivyo kabla ya kuanza kwa vita.

Awamu tatu

• Kuanzia Januari hadi Juni 2023, Urusi imepanga kukusanya vifaa 100 kwa mwezi, ili kutengeneza ndege zisizo na rubani kama zile za Iran.

• Kuanzia Aprili, Urusi ingezalisha droni zenye injini za Irani na vifaa vya elektroniki. Wakati wa awamu hii, ambayo ilipaswa kudumu hadi mwisho mwa 2023, ilipangwa kuzalisha droni 170-180 kwa mwezi.

• Wakati wa awamu ya tatu, ambayo inapaswa kuwa ianze Januari 2024, kiwanda hicho kitazalisha zaidi ya droni 220 kwa mwezi, na kufikisha droni elfu 6 ifikapo Septemba 2025 na hivyo kutimiza agizo la Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Changamoto

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na uchambuzi wa Taasisi ya Marekani ya Sayansi na Usalama wa Kimataifa (ISIS), mpango wa uzalishaji unaweza kufaulu, lakini kuna dosari nyingi zinazoweza kusababisha kuvurugika au kucheleweshwa kwa utekelezaji.

Moja ya sababu kuu ni kwamba, kama Iran yenyewe inavyokiri katika nyaraka hizo, zaidi ya 90% ya vifaa vidogo na vya elektroniki vya Shahedah-136 ni vya Magharibi, haswa kutoka Marekani.

Hapo awali, vifaa hivi havikujumuishwa kama teknolojia ya siri au ya kijeshi, na ilikuwa rahisi kuvipata. Lakini baada ya Marekani kuweka marufuku ya usafirishaji wa vifaa hivyo kwenda Urusi, hali imebadilika.

Shida nyingine ni injini, ambazo zimekuwa ngumu kupatikana nchini Urusi. Droni za Shahed-136 inaendeshwa kwa injini ya Ujerumani ya Limbach Flugmotoren L550E - ambayo Iran iliinunua kwa njia isiyo halali miongo miwili iliyopita. Walakini, wahandisi wa Urusi watalazimika kuunda toleo lao la injini, ambayo, kulingana na mawasiliano ya ndani, ni moja ya kazi ngumu sana.

Wafanyikazi waliohitimu ni wa chache. Kulingana na mpango huo, wafanyakazi 810 katika zamu tatu kwa siku wanapaswa kufanya kazi huko Yelabuga. Lakini kwa sababu ya uhaba mkubwa wa wataalamu, sio tu wasimamizi wa uzalishaji na wahandisi, lakini hata wanafunzi walilazimika kutumwa Irani kwa mafunzo.

Mamlaka za mitaa pia huwarubuni vijana kwa ahadi za makazi na ruzuku, mishahara ya $ 550 kwa mwezi, wakati wanafunzi wanatumwa tu kiwandani kwa mafunzo kama sehemu ya mchakato wa kujifunza. Wakati huo huo, wasimamizi wanajaribu kwa kila njia kuwaweka karibu wale ambao tayari wameanza uzalishaji.

Shida nyingine ni kwamba 25% ya ndege zisizo na rubani zinazotolewa na Iran zina kasoro, na hii inajumuisha ndege kubwa (Shahed-136) na ndogo (Shahed-131). Urusi haikuhitaji ndege ndogo, lakini Iran ilisisitiza, na upande wa Urusi haukuweza kukataa.

Kulingana na nyaraka hizo, wafanyakazi wa Urusi hawana ujuzi wa kutosha na vipuri vya kukarabati ndege zisizo na rubani zilizoharibika au zinazofanya kazi vibaya.