Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Jumapili: Nkunku anataka kuondoka Chelsea
Mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, ameamua kuondoka Chelsea msimu huu wa joto. (Sky Sports Ujerumani)
Beki wa Kiukreni Oleksandr Zinchenko, 28, huenda akaondoka Arsenal msimu huu wakati Borussia Dortmund ikionesha nia ya kumnyakua. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Marekani Weston McKennie, 26, amefikia makubaliano ya mdomo na Juventus kusalia katika klabu hiyo hadi 2028. (Fabrizio Romano)
Manchester United, Chelsea na Tottenham Hotspur ni miongoni mwa vilabu kadhaa vinavyotaka kumsajili beki wa kati wa Bournemouth Dean Huijsen, 20. (CaughtOffside)
Aston Villa watakuwa na shida kumnunua mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, kwa mkataba wa kudumu kutoka Manchester United ikiwa hawatafuzu Ligi ya Mabingwa. (Football Insider)
Maskauti kutoka Aston Villa walikuwa kwenye umati wa watu kumtazama mshambuliaji wa Uhispania na Porto Samu Aghehowa, 20, huku kukiwa na nia ya kumsajili msimu huu wa joto. (Record , externalvia Sports Witness)
Everton wanatafakari kuhusu kumrejesha mshambuliaji wa zamani Richarlison, 27, katika klabu hiyo, huku Tottenham Hotspur ikiripotiwa kuwa tayari kukubali ada ya pauni milioni 40. (GiveMeSport)
Real Madrid wanafikiria kumnunua mlinzi wa kulia wa Real Sociedad Jon Aramburu, 22. (Fichajes)
Leeds United wamemuongeza mshambuliaji wa AZ Troy Parrott, 23, kwenye orodha ya washambuliaji wao kufuatia kupandishwa kwao kwenye Ligi ya Premia. (TeamTalk)
Fiorentina wanakaribia kuongeza mkataba wa beki mwenye umri wa miaka 20 Pietro Comuzzo huku wapinzani wao wa Serie , Napoli wakimtaka. (Tuttomercato)
Liverpool wanaweza kufanya uhamisho wa mshambuliaji wa Real Madrid Rodrygo, 24, huku Mbrazil huyo akiwa tayari kuhama Uhispania. (GiveMeSport)
Ajax wako tayari kumuuza mlinzi wa Uholanzi Jorrel Hato, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 akivutiwa na vilabu kama Chelsea. (Kick-off podcast)