'Kuwaambia nyuki kifo cha Malkia' na mila nyingine zisizo za kawaida katika Familia ya Kifalme

Chanzo cha picha, Getty Images
Kifo cha Malkia Elizabeth II wa Uingereza na kutawazwa kwa Mfalme Charles III vimethibitisha kwa mara ya kwanza katika vizazi asili ya sherehe kubwa ya Familia ya Kifalme.
Lakini baadhi ya mila na mavazi yanaweza kuwashangaza hata wale wanaojiona kuwa wajuzi wa mambo ya kifalme.
Hii ni baadhi ya mifano isiyo ya kawaida zaidi.
Habari za kusikitisha zilitumwa kwa nyuki
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Licha ya vyombo vya habari vikubwa na mitandao ya kijamii kutangaza kifo cha Malkia, kundi binafsi lilibidi "kuambiwa ana kwa ana" kuhusu kifo cha mfalme: nyuki wake.
John Chapple amekuwa mfugaji nyuki katika familia ya kifalme kwa miaka 15. Alitumia utamaduni wa karne nyingi kwa kufahamisha mizinga iliyohifadhiwa katika uwanja wa Buckingham Palace na Clarence House (makazi rasmi ya Charles kama Prince of Wales) kuhusu habari hiyo ya kusikitisha.
Katika mahojiano na gazeti la Daily Mail, Chapple alieleza kuwa pia aliwaomba nyuki kuwa wema kwa mfalme huyo mpya. Utamaduni huo ni sehemu ya imani za jadi kwamba nyuki wanaweza kuacha kutoa asali ikiwa hawataambiwa mabadiliko ya mmiliki.
"Mtu aliyefariki ni bwana au bibi wa mizinga, mtu muhimu katika familia ambaye anafariki na huna umuhimu wowote kuliko Malkia, sivyo?", mfugaji nyuki alisema.
"Unagonga kila mzinga na kusema, 'Mkuu amefariki, lakini msiondoke. Mkuu wako mpya atakuwa kiongozi mzuri kwako.'
Je, mfalme atakuwa na siku ya kuzaliwa mara mbili pia?

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Miongoni mwa maamuzi mengi ambayo Mfalme Charles III atachukua kuhusu utaratibu wa sherehe, moja ni ya binafsi kabisa: sherehe zake za kuzaliwa.
Malkia Elizabeth II alikuwa na siku mbili za kuzaliwa zilizojulikana: alizaliwa tarehe 21 Aprili, hayati malkia alikuwa na sherehe zake rasmi siku ya Jumamosi ya pili ya Juni na gwaride lililojulikana kama Trooping the Colour.
Kwa nini? Kweli, Aprili kawaida ni mwezi wa baridi nchini Uingereza kwa hafla za nje, wakati kiangazi huanza mnamo Juni.
Tamaduni hii ni ya zamani zaidi, ingawa kwa mara ya kwanza ilianza na George II mnamo 1748. Ni yeye aliyeamua kufanya sherehe za kuzaliwa kwa gwaride la sherehe lililokuwa tayari.
Je! Charles III ataendeleza mila hiyo? Hatujui bado, lakini ni muhimu kutambua kwamba mfalme mpya alizaliwa Novemba, ni mwezi unaojulikana kwa juakali na hali ya hewa ya joto.
"Nahisi kwamba mfalme huyo mpya ataacha mambo kama yalivyo, ikizingatiwa alizaliwa katika mwezi wa vuli na Trooping the Colour ni tamasha maarufu," mwanahistoria wa kifalme Richard Fitzwilliams anaiambia BBC.
Fitzwilliams, hata hivyo, anaonyesha kwamba mila nyingine ya Uingereza ni kutotabirika kwa hali yake ya hewa, kwa kutumia kama mfano kutawazwa kwa Malkia Elizabeth II, mnamo Juni 1953.
"Hali ya hewa ilikuwa mbaya siku hiyo," anasema.
"Malkia na wafalme hawawezi kudhibiti hali ya hewa."
Nguvukazi dhidi ya nguvu ya farasi

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu mwaka wa 1901, mazishi ya Kifalme nchini Uingereza yamekuwa yakiadhimishwa na jeshi la kifalme la majini Royal Navy wakitumia kamba kuvuta jeneza la mfalme, lililowekwa kwenye gari la kubebea bunduki.
Chaguo hili la wafanyakazi dhidi ya farasi linaweza kuonekana kuwa la kutatanisha, lakini ni mila iliyoanza mnamo 1901 wakati wa mazishi ya Malkia Victoria.
Katika kipindi hicho, bado ilikuwa kawaida kwa farasi kuvuta gari lenye jeneza la mfalme.
Lakini msafara huo ulikuwa na wakati wa kuogofya kutokana na wanyama kukimbia kwa hofu.
"Farasi hawakuitikia vyema siku ya baridi kali na ikawa kwamba jeneza la Malkia Victoria lilikuwa karibu kudondoshwa," mwanahistoria wa kifalme Kelly Swab aliambia BBC.
Kwa agizo la Mfalme Edward VII, mrithi wa Victoria na mfalme mpya, mabaharia walioshiriki katika shuhuli ya mazishi waliingia.
"Kulikuwa na watu mashuhuri kutoka kote ulimwenguni na jambo zima lingeweza kuwa aibu kubwa."
"Badala yake, mila ya kifalme ilizaliwa kutokana na machafuko," Swab anaongeza.
Wakati wa mazishi ya Mfalme George VI, mnamo 1952, mara ya mwisho sherehe ya aina hii ilifanyika, wanaume 138 walisimamia kazi hiyo.
Mila ya fimbo iliyovunjika

Chanzo cha picha, Getty Images
Miongoni mwa fahari na sherehe zinazotarajiwa kuonyeshwa katika sherehe za kifalme, kuna watu wachache watakuwa wamesikia.
Tamaduni huamuru kazi kwa Lord Chamberlain, cheo anachopewa afisa mkuu wa Kaya ya Kifalme na ambaye majukumu yake ya kiibada ni pamoja na kuandamana na mfalme kwenye ziara ya kila mwaka ya bunge.
Lazima avunje fimbo yake nyeupe ya sherehe juu ya kaburi la kiongozi wa Kifalme aliyefariki ili kuashiria mwisho wa huduma yake kwao.
Bwana Chamberlain wa sasa ni Andrew Parker, mkuu wa zamani wa MI5, moja ya mashirika ya kijasusi ya Uingereza. Alichukua wadhifa huo Aprili 2021.
Sherehe hiyo ilianza karne nyingi zilizopita
Mara ya mwisho ilifanyika zaidi ya miaka 70 iliyopita wakati Earl of Clarendon alipovunja fimbo yake juu ya kaburi la George VI, babake Malkia Elizabeth II.
Na Richard Fitzilliams anasema desturi hizo zinaupa ufalme wa Uingereza uzuri wake.
"Ni kwa sababu ya mila kama hii kwamba Familia ya Kifalme ya Uingereza ni ya kipekee."















