Malkia Elizabeth II: Ni lini na ni wapi mazishi yatafanyika ?

Chanzo cha picha, PA Media
Mwili wa Malkia utaweza kutazamwa kwa siku nne mfulurizo kwa siku nne kamili kabla ya mazishi yake Juamatatu, tarehe 19 Septemba.
Umma utaruhusiwa kutazama jeneza katika kipindi hicho.
Kabla ya hili kufanyika Malkia atakuwa amepumzika katika St Giles Cathedral Edinburgh, kwa saa 24 kuanzia tarehe 12 Septemba, huku watu wakiweza kutoa heshima zao za mwisho.
Familia yake, wanasiasa na viongozi wa dunia watahudhuria mazishi yake ya kitaifa saa 11:00 BST siku hiyo, ambayo itakuwa ni siku ya mapumziko inayofahamika kama Bank holiday.

Chanzo cha picha, Reuters
Kutoka From Balmoral, Aberdeenshire, ambako alifariki, Jeneza la Malkia lililotengenezwa kwa ,ti aina ya mwaloni liliondoka Jumapili kuelekea Edinburgh, likiondoka taratibu kuelekea katika Kasri la Holyroodhouse ambapo liliwasili 16:00 BST.
Jumatatu mchana, litaelekea katika Kanisa kuu la St Giles, Edinburgh, likiambatana na wanafamilia ua Ufalme. Kutakuwa na ibada na jeneza litalazwa hapa kwa saa 24 kwa ajili ya watu kutoa heshima zao za mwisho.
Siku itakayofuatia Bintimfalme atasindikiza mwili w amama yake wakati utakapokuwa ukisafirishwa kwa ndege kurudi London. Jeneza la Malkia litachukuliwa kutoka uwanja wa ndege wa Edinburgh na kupelekwa katika Buckingham Palace.
Jumatano mchana, litapelekwa katika Westminster Hall, na kuwasili huko saa 15:00 BST. Siku nne kamili za kutazamwa na waombolezaji zitaanza kuanzia Alhamisi, kabla ya mazishi kufanyika.
Mazishi ya kitaifa yatafanyika saa tano asubuhi tarehe 19, kwa maandamano yatakayofanyika katika Windsor Castle, mkiwemo matembezi marefu- Long Walk. Malkia atazikwa katika kanisa dogo linalofahamika kama King George VI Memorial Chapel lililopo Windsor.

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Wakuu wa nchi kutoka maeneo yote ya dunia wataalikwa kujiunga na wanafamilia ya Ufalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.
Wanasiasa wa ngazi ya juu wa Uingereza wa sasa na wa zamani na mawaziri wa kuu pia wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya mazishi itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni.
Hakuna sharti kwa waandalizi la kufuta mipango iliyopangwa katika siku ya mazishi lakini muongozo wa serikali unasema kuwa waandalizi wa michezo au matukio yaliyopangwa mapema wanaweza kubadili ratba zao ili kuepuka kugongana na huduma au maandamano ya kuuaga mwili.
Baadhi ya matukio yalifutwa au kuahirishwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Malki.a
Mechi za soka katika Primia Ligi, Ligi ya soka ya England au katika Uskochi na Ireland Kaskazini zimeahirishwa hadi Jumanne, huku michezo ya kombe la wanawake la Super Ligi, Kombe la washindi la Wanawake na kombe la dunia la wanawake la FA ikiwa imezuiwa kwa muda, na ratiba ya michezo ya mashindano ya farasi, gofu na masumbwi zimefutwa.
Migomo mikubwa iliyokuwa imepangwa kufanyika wiki ijayo ilifutwa mara moja, na muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Uingereza ulisema kuwa umeahirisha mkutano wake wa mwaka katika Brighton.
Mfalme alithibitisha mapema Jumapili kwamba siku ya mazishi itakuwa ni siku ya mapumziko ya bank holiday, wakati alipotangazwa rasmi kama mfalme katika Kasri la St James, London.
Katika hotuba yake, aliisifu ‘’enzi isiyo na kifani’’.
Mfalme kutemmbelea mataifa
Kabla ya mazishi Mfalme Uskochi, Scotland, Ireland Kaskazini na Wales.
Kipndi cha maombolezo ya kitaifa kitadumu hadi kufikia siku ya mazishi ya kitaifa, serikali imetangaza. Familia ya Ufalme itaendelea kuomboleza kwa siku saba zaidi baada ya mazishi.
Westminster Abbey ni kanisa la kihistoria ambapo wafalme wa Uingereza na Mamalkia hutawazwa – lakini hapajawahi kufanyika mazishi pale tangu karne ya 18. Mazishi ya baba yake Malkia, babu yake na bibi mzaa baba yake, MalkiaQueen Victoria, katika miaka ya 1900, yalifanyika katika Kanisa dogo la St George, Windsor.
Wakuu wa nchi kutoka maeneo yote ya dunia wataalikwa kujiunga na wanafamilia ya Ufalme kukumbuka maisha na huduma ya Malkia.
Wanasiasa wa ngazi ya juu wa Uingereza wa sasa na wa zamani na mawaziri wa kuu pia wanatarajiwa kuhudhuria ibada ya mazishi itakayopeperushwa kwa njia ya televisheni.
Hakuna sharti kwa waandalizi la kufuta mipango iliyopangwa katika siku ya mazishi lakini muongozo wa serikali unasema kuwa waandalizi wa michezo au matukio yaliyopangwa mapema wanaweza kubadili ratba zao ili kuepuka kugongana na huduma au maandamano ya kuuaga mwili.
Baadhi ya matukio yalifutwa au kuahirishwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Malki.a
Mechi za soka katika Primia Ligi, Ligi ya soka ya England au katika Uskochi na Ireland Kaskazini zimeahirishwa hadi Jumanne, huku michezo ya kombe la wanawake la Super Ligi, Kombe la washindi la Wanawake na kombe la dunia la wanawake la FA ikiwa imezuiwa kwa muda, na ratiba ya michezo ya mashindano ya farasi, gofu na masumbwi zimefutwa.
Migomo mikubwa iliyokuwa imepangwa kufanyika wiki ijayo ilifutwa mara moja, na muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Uingereza ulisema kuwa umeahirisha mkutano wake wa mwaka katika Brighton.
Mfalme alithibitisha mapema Jumapili kwamba siku ya mazishi itakuwa ni siku ya mapumziko ya bank holiday, wakati alipotangazwa rasmi kama mfalme katika Kasri la St James, London.
Katika hotuba yake, aliisifu ‘’enzi isiyo na kifani’’.

Hakuna sharti kwa waandalizi la kufuta mipango iliyopangwa katika siku ya mazishi lakini muongozo wa serikali unasema kuwa waandalizi wa michezo au matukio yaliyopangwa mapema wanaweza kubadili ratba zao ili kuepuka kugongana na huduma au maandamano ya kuuaga mwili.
Baadhi ya matukio yalifutwa au kuahirishwa mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Malkia.
Mechi za soka katika Primia Ligi, Ligi ya soka ya England au katika Uskochi na Ireland Kaskazini zimeahirishwa hadi Jumanne, huku michezo ya kombe la wanawake la Super Ligi, Kombe la washindi la Wanawake na kombe la dunia la wanawake la FA ikiwa imezuiwa kwa muda, na ratiba ya michezo ya mashindano ya farasi, gofu na masumbwi zimefutwa.
Migomo mikubwa iliyokuwa imepangwa kufanyika wiki ijayo ilifutwa mara moja, na muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini Uingereza ulisema kuwa umeahirisha mkutano wake wa mwaka katika Brighton.
Mfalme alithibitisha mapema Jumapili kwamba siku ya mazishi itakuwa ni siku ya mapumziko ya bank holiday, wakati alipotangazwa rasmi kama mfalme katika Kasri la St James, London.
Katika hotuba yake, aliisifu ‘’enzi isiyo na kifani’’.

Chanzo cha picha, Reuters
Mfalme alikuwa mfalme baada ya kifo cha mama yake, lakini mkutano na baraza la wanasiasa, maafisa na viongozi wa kidini ulithibitisha rasmi kutawazwa kwake.
Chumba kilichokuwa kimejaa, wakiwemo mawaziri wote wakuu sita wa zamani wa Uingereza sita, walirudia sentensi. Kutawazwa kulisomwa kwa sauti ya juu kwenye veranda juu ya Mahakama ya Friary katika Kasri la Court in St James.
Karani wa baraza la Privy Richard Tilbroo alimtangaza Charles "Mfalme, mkuu wa Jumuiya ya Madola, mlinzi wa imani ",kabla ya kutangaza "God Save the King".