Safari ya mwisho ya Malkia Elizabeth II na simulizi ya aina yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati mwili wa Malkia Elizabeth II ukiwa njiani ukitokea Balmoral kwenda kwenye kasri la kifalme la Holyroodhouse huko Edinburgh, hii ni hatua za kwanza za safari ambayo itachukua zaidi ya wiki moja, kabla ya kilele cha mazishi ya kitaifa Jumatatu ijayo.
Ni safari ya sherehe na simulizi ya aina yake. Inatoka kwenye mazingira ya nyumbani kwa wahudumu na walizni wa Balmoral kubeba jeneza lake, hadi kwenye eneo lenye hadhi yake la Westminster Abbey mjini London, ambapo viti vitajazwaa na ujio wa viongozi kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Wakati baba wa Malkia, George VI alikufa mnamo 1952 walinzi huko Sandringham walilipa gwaride la heshima jeneza lake.

Chanzo cha picha, Getty Images
Balmoral ilikuwa moja ya sehemu alizopenda Malkia, labda kwa sababu ilimpa faragha zaidi. Mawaziri wakuu waliokuwa wakizuru huko walisemekana kushangazwa kumuona akiosha vyombo baada ya kula.
Ameondoka katika eneo hilo kwa mara ya mwisho, huku jeneza lake likiwekewa mashada ya maua yaliyochumwa kutoka kwenye hifadhi za himaya yake, ambyo mengi alikuwa akiyapenda wakati wa uhai wake.
Waombolezaji sasa wamekusanyika katika miji iliyo kando ya njia unakopitishwa mwili wake, wengine wamewekwa kando ya barabara kutazama safari hiyo, na vikundi hivi vidogo vidogo vya watu vinatarajiwa kuwa umati mkubwa zaidi, wakati safari ya mwili wake ikikaribia kufika Edinburgh na kisha London.

Watu wamekuwa wakikusanyika kandokando ya barabara huko Dundee, wakitarajia kushuhudia jeneza lake na kutoa heshima zao kwa Malkia Elizabeth II.



Chanzo cha picha, Getty Images












