Malkia Elizabeth II na Afrika: Uhusiano wa muda mrefu

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia Elizabeth alipigwa picha akicheza na Rais wa zamani wa Ghana Kwame Nkrumah mwaka 1961 huko Accra.

Inasemekana kwamba Malkia Elizabeth II alikuwa na nafasi maalum moyoni mwake kwa ajili ya Afrika, na alikuwa barani humo katika nyakati muhimu za maisha yake. Binti Mfalme Elizabeth wa wakati huo alikuwa akiishi katika Hoteli ambayo imefungwa sasa ya Treetops katika sehemu ya mashambani ya Kenya, iliyozungukwa na miti ya kijani kibichi, mirefu na wanyamapori, wakati babake, Mfalme George wa Sita, alipofariki na akawa Malkia akiwa na umri wa miaka 25 tu.

Wakati wa utawala wake wa miaka 70 alitembelea zaidi ya nchi 20 za Kiafrika, na aliwahi kusema kwa mzaha mbele ya Nelson Mandela aliyekuwa akitabasamu kwamba amekuwa Afrika zaidi kuliko "karibu mtu yeyote", na kusababisha vicheko vikali kutoka kwa wale walio karibu naye.

Malkia huyo alikuwa na uhusiano mzuri binafsi na Mandela - kiongozi wa Afrika Kusini ambaye aliongoza vita dhidi ya utawala wa wazungu wachache nchini humo.

Taasisi yake ilionyesha kusikitishwa kwake na kifo chake, ikisema: "Pia walizungumza kwenye simu mara kwa mara, wakitumia majina yao ya kwanza kama ishara ya kuheshimiana na vile vile upendo."

Hata alikuwa na jina maalum la Malkia, Motlalepula, ambalo "linamaanisha Malkia wa mvua", kwa sababu ziara yake ya 1995 nchini wakati wa utawala wake iliambatana na mvua ya kumkaribisha.

Baada ya kurithi himaya kubwa iliyoenea katika bara la Afrika baada ya kuwa Malkia, enzi zake zilishuhudia makoloni yote 14 ya Waingereza katika nchi za Afrika yakipata uhuru wao, kuanzia na Ghana mnamo 1957.

Na bado Malkia aliweza kudumisha uhusiano wake na Afrika, kwa sehemu kupitia uundaji wa Jumuiya ya Madola mwaka 1961, alipigwa picha akicheza na Kwame Nkrumah, ambaye aliongoza kampeni ya uhuru wa Ghana na kuwa rais wake wa kwanza.

Hasa, neno himaya liliachwa wakati wa kiapo chake cha kutawazwa mnamo 1953.

Sasa, viongozi kutoka barani kote wametoa salamu za pole kwa Uingereza

Rais wa nchi ambako safari yake kama Malkia ilianza, Uhuru Kenyatta wa Kenya, aliomboleza kifo chake katika taarifa, akimtaja kama "Alama ya juu ya utumishi wa kujitolea kwa ubinadamu na kiongozi mkuu wa sio tu Uingereza na Jumuiya ya Madola ambayo Kenya ni mwanachama mashuhuri lakini ulimwengu mzima."

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mnamo 1983, Malkia alitembelea tena Hoteli ya Treetops nchini Kenya, ambapo alikuwa Malkia baada ya kifo cha baba yake.

Ingawa uhusiano kati ya Zimbabwe na Uingereza umekuwa sio mzuri kwa miaka mingi, jambo lililosababisha hayati Rais Robert Mugabe kujiondoa katika Jumuiya ya Madola, mrithi wake Emmerson Mnangagwa aliandika haraka kwenye Twitter kwamba anatoa "pole ya dhati" kwa Familia ya Kifalme na "watu wa Uingereza, na Jumuiya ya Madola".

Kiongozi wa Nigeria, koloni kubwa zaidi la zamani la Uingereza barani Afrika, Muhammadu Buhari alimwandikia salamu za pole ndefu kwenye Twitter, akisema amepokea kifo chake kwa "huzuni kubwa".

"Hadithi ya Nigeria ya sasa haitakamilika bila ukurasa wa Malkia Elizabeth ll, mtu mashuhuri duniani na kiongozi bora. Alijitolea maisha yake kufanya taifa lake, Jumuiya ya Madola na dunia nzima kuwa mahali pazuri." Pia alikaribisha kutwaa kwa mrithi wake Mfalme Charles III kwenye kiti cha enzi.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Na Ali Bongo, rais wa mwanachama mpya zaidi wa Jumuiya ya Madola, Gabon, koloni la zamani la Ufaransa ambalo lilijiunga na jumuiya hiyo mwezi Juni, pia ametuma salamu zake za rambirambi. Licha ya kumiminika kwa salamu za rambirambi kutoka kwa viongozi wa bara hilo, baadhi ya Waafrika wengine wamezungumzia mateso yao chini ya utawala wa Waingereza, wakieleza kuwa ukoloni mwingi ulifanywa kwa jina la familia ya kifalme.

Baadhi ya Falme zenyewe za Kiafrika pia wameelezea masikitiko yao. Prince Mangosuthu Buthelezi alitoa heshima zake kwa niaba ya Mfalme Misuzulu KaZwelithini, kiongozi wa Wazulu wa Afrika Kusini. Aliangazia "urafiki wake wa kuthaminiwa" na Mfalme Charles III, akimtumia salamu binafsi za rambirambi.

Mfalme Misuzulu yuko katika nafasi nzuri ya kuelewa kile ambacho Mfalme Charles anapitia, kwani baba yake mwenyewe, Zwelithini, alifariki mwaka jana, baada ya miaka 50 ya kiti cha enzi.

Malkia alikuwa kwenye ziara ya Afrika Kusini aliposherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 21 mwaka wa 1947. Katika hotuba yake maarufu ya redio kutoka Cape Town, alijitolea maisha yake kwa Jumuiya ya Madola na kusema alijisikia "nyumbani" nchini Afrika Kusini kana kwamba alikuwa akiishi hapo maisha yake yote.

Akiwa maarufu duniani kote kwa uwezo wake wa nkubaki kwenye siasa, alitoa kauli kali mwaka 1995, akizuru Afrika Kusini mwaka mmoja tu baada ya Mandela kuwa rais na kumaliza mfumo wa ubaguzi wa rangi uliohalalishwa unaojulikana kama ubaguzi wa rangi.

Aliipongeza nchi kwa maendeleo yake: "Mmekuwa taifa moja ambalo roho yake ya upatanisho ni mfano mzuri kwa ulimwengu, na nimerudi kujionea mwenyewe kile ambacho si muujiza mdogo."

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Malkia huyo anaripotiwa kuwa na urafiki mkubwa na Nelson Mandela, ambaye hapa walikuwa Cape Town mwaka 1995.